Sudan Kusini

 1. Video content

  Video caption: Sudan Kusini: Mambo matano usiyoyajua kuhusu Sudan Kusini

  Ni miaka 10 tangu Sudan Kusini ilipokuwa taifa changa duniani

 2. Kiongozi wa Sudan Kusini amfuta kazi mkuu wa jeshi

  Rais wa Sudan Kusini Salvar Kiir

  Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amemfuta kazi mkuu wa jeshi na kumteua kama balozi wa nchi hiyo nchini Ubelgiji.

  Jenerali Johnson Juma Okot, ambaye alikuwa mkuu wa Jeshi la nchi hiyo ,South Sudan People’s Defence Forces (SSPDF) na nafasi yake kuchukuliwa na na Jenerali Santino Deng Wol.

  Rais hakutoa sababu ya hatua hiyo.

  Rais Kiir pia alimfuta kazi Jenerali Ruben Malek Riak kutoka nafasi yake kama naibu waziri wa ulinzi na kumteua Luteni Jenerali Chol Thon Balok katika nafasi hiyo .

  Katika mabadiliko madogo katika huduma za ujasusi, Rais Kiir pia alimbadilisha Jenerali Thomas Duoth Guet kama mkurugenzi mkuu wa mrengo wa ujasusi wa Huduma ya Usalama wa Kitaifa (NSS) na Jenerali Simon Yien Makuac.

  Rais alimpandisha cheo Akol Khor Kuc, mkuu wa mrengo wa usalama wa ndani wa NSS kwa cheo cha Luteni-mkuu wa kwanza, wakati akiendelea kuhudumu katika nafasi yake .

  Naibu waziri wa ulinzi na Jenerali Guet wameteuliwa kama mabalozi kwa Eritrea na Kuwait mtawaliwa.

 3. Gavana anusurika kifo katika shambulio Sudan Kusini

  Governor Luis Lobong survived the ambush in Eastern Equitoria state

  Karibu watu 20 wamefariki katika jimbo la Equatoria Mashariki mwa Sudan Kusini ambako Gavana Louis Lobong Lojore aliponea shambulio hatari, Katibu wake wa habari amesema.

  Alinadro Lotok alisema Bw. Lobong aliponea shambulio kali Jumatatu jioni kutoka kwa vijana wa jamii ya Buya waliokuwa wamejihami.

  “Gavana Lobong alikuwa katika kambi ya -15 kutuliza hali ya taharuki katika eneo hilo baada ya shambulio la siku ya Jumapili dhidi ya kituo hicho, kusababisha vifo vya watu 17 ," alisema.

  Vijana waliokuwa na hasira huku wakiwa wamejihami walimfuata gavana na kushambulia kambi ya kijeshi Camp-15, na kuongeza idadi ya vifo katika visa hivyo viwili kufikia karibu 20, aliongeza.

  "Baada ya makabiliano ya risasi ya saa mbili na vijana hao, kitengo cha ulinzi wa gavana na askari katika kambi ya jeshi ya Camp-15 walifanikiwa kuwarudisha nyuma."

  Miongoni mwa waliofariki ni walinzi wa gavana na mke wa askari. Wengine watatu walijeruhiwa vibaya.