Shirika la Biashara Duniani

 1. Okonjo-Iweala aanza rasmi kazi kama mkuu wa WTO

  Dkt Okonjo-Iweala ni mwanamke wa kwanza Mwafrika kushikilia nafasi hiyo.
  Image caption: Dkt Okonjo-Iweala ni mwanamke wa kwanza Mwafrika kushikilia nafasi hiyo

  Mnageria-Mmarekani, Ngozi Okonjo-Iweala, anaanza rasmi kazi kama mkuu mpya wa Shirika la Biahsara Duniani (WTO) Jumatatu ya leo.

  Dkt Okonjo -Iwela ambaye ni waziri wa zamani wa fedha na mambo ya nje wa Nigeria, ni mwanamke wa kwanza wa Afrika kuongoza WTO.

  Ngozi Okonjo-Iweala amesema kipaumbele chake ni kushughulikia masuala ya afya na athari za kiuchumi zinazotokana na majanga.

  Kuna wasiwasi huko Washington na miji mikuu mingine kuhusu sera za biashara za China na jinsi WTO inavyojiandaa kushughulikia masuala hayo.

  Dkt Okonjo-Iweala anafahamika kwa kuwa mwana -mageuzi, lakini atakabiliwa na mslahi ya nchi wanachama.

  Soma zaidi:

 2. Video content

  Video caption: Mvinyo 'Mkubwa' zaidi duniani aina ya Whiskey wauzwa

  Pombe iliyo kwenye chupa kubwa zaidi ya Whiskey imeuzwa kwa mnada kwa pauni elfu kumi na tano