Filamu

 1. Ron Jeremy: Nyota wa filamu wa Marekani alishtakiwa kwa uhalifu wa kingono

  Bwana Jeremy

  Nyota wa filamu ya watu wazima nchini Marekani Ron Jeremy ameshtakiwa kwa makosa 34 ya uhalifu wa kingono unaohusisha wanawake 21, kwa zaidi ya miaka 20, waendesha mashtaka wa Los Angeles wanasema.

  Bwana Jeremy, 68, alikana mashtaka hayo Jumatano.

  Ni mmoja wa majina tajika katika filamu ya watu wazima na ameshiriki katika zaidi ya filamu 1,700 tangu mwaka 1979.

  Shtaka la Agosti 19, ambalo lilikuwa limefungwa Jumatano, linamshutumu Bwana Jeremy kwa makosa 12 ya ubakaji, ikiwa ni pamoja na ile ya msichana wa miaka 17 mnamo 2008 na msichana wa miaka 15 mwaka 2004.

  Mashtaka ya hivi karibuni yanayomkabili ni ya Januari mosi 2020, ambapo mwanamke wa miaka 21 anamtuhumu kwa ubakaji na ulawiti.

  Wakili wake siku ya Jumatano alisema Bw. Jeremy anashikilia kuwa mteja wake hana hatia yoyote.

  Bwana Jeremy, ambaye jina lake halisi ni Ronald Jeremy Hyatt, anakaa gerezani kwa dhamana ya $ 6.6m (£ 4.81m).

  Mnamo Juni jmwaka jana, Bwana Jeremy alifikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kubaka wanawake wawili na kuwanyanyasa kingono wengine wawili kati ya 2014 na 2019.

  Wakati huo, wakili wake alikanusha mashtaka hayo, akidai kwamba Bwana Jeremy alikuwa "msaidizi wa wanawake" zaidi ya 4,000 na kwamba "wanawake hujitupa kwake."

  Mchekeshaji Bill Cosby amehukumiwa hadi miaka 10 jela kwa unyanyasaji wa kingono

  Bill Cosby: Wajue watu wengine maarufu waliofungwa na kuachiwa

 2. Terry Crews na mke wake Rebecca wanakiri kuwa kupona kwake kumetokana na usaidizi wa kisaikolojia

  Ni taarifa iliyowashangaza wengi hasa kutokana na umaarufu wa mchezaji filamu maarufu wa Hollywood Terry Crews. Hata hivyo nyota huyu wa filamu amekuwa wazi kuhusu ni kwanini ameamua kueleza yaliyomsibu kwa umma: Lengo ni kuwasaidia watu wengine wanaopitia matatizo kama aliyokuwa nayo.

  Soma Zaidi
  next
 3. Lupita atembelea Serengeti kwa mara ya kwanza

  lupita

  Nyota wa Hollywood kutoka nchini Kenya Lupita Nyong'o ametembelea kwa mara ya kwanza mbuga ya wanyama ya Tanzania ya Serengeti, Aprili 5, 2021,.

  Mwanamitindo huyo muigizaji alipiga picha na kuiweka kwenye mitandao yake ya kijamii na kuandika serengeti.

  Picha hiyo aliyojipiga mwenyewe yaani selfie inaonesha mazingira ya mbuga hiyo na kukiwa na tembo nyuma yake.

  View more on twitter

  Miezi michache iliyopita, kulitokea gumzo la kwanini Lupita hakupewa ubalozi wa utalii nchini Kenya na kupewa mwanamitindo wa Uingereza Naomi Campbell.

  Lakini waziri wa Utalii nchini Kenya Najib Balala alitetea uamuzi wa kumtaja mwanamitindo wa Uingereza Naomi Campbell kuwa balozi wa utalii kimataifa kwa nchi hiyo.

  Wakati wa hafla ya umma, Bwana Balala alisema anajua Wakenya wengi wameuliza kwanini muigizaji wa Hollywood Lupita Nyong'o hakuchaguliwa katika nafasi hiyo.

  Waziri akajibu kwamba wamekuwa wakimtafuta Bi. Nyong'o lakini hajapatikana kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

  Muigizaji huyo wa Kenya ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Oscar alipendekezwa na Wakenya katika mitandao ya kijamii kuwa mtu sahihi wa kushikilia nafasi ya balozi wa utalii kimataifa kuwakilisha Kenya.

  Bwana Balala alisema Bi. Campbell amechukua nafasi hiyo kwa maslahi ya umma na kwamba serikali inafanyia kazi namna ya kutumia ushawishi wake kutangaza utalii, kulingana na vyombo vya habari vya nchini Kenya.

 4. Mchekeshaji Eric Omondi akamatwa Kenya

  Erick Omonde

  Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi Filamu nchini Kenya (KFCB), Dkt Ezekiel Mutua, ametangaza kwamba mchekeshaji Eric Omondi, amekamatwa kwa kukiuka kanuni ya maadili ya bodi hiyo.

  ''Maafisa wa Ufuatiliaji wa Bodi ya Uainishaji wa Filamu Kenya wakishirikiana na Maafisa wa Polisi kutoka Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) leo mchana wamemkamata Eric Omondi kwa kukiuka masharti ya Sheria ya Filamu na Maonyesho ya Sura 222 ya Sheria za Kenya kwa kutengeneza na kusambaza filamu ambayo haijaidhinishwa kwa jina "Wife Material.",taarifa ya Dkt. Mutua ilisema.

  Kama hatua ya kutia mkazo tangazo hilo Dkt. Mutua pia ameweka tangazo hilo katika Twitter yake.

  View more on twitter

  Hii sio mara ya kwanza Dkt Mutua na Eric Omondi kutofautiana kuhusu maudhui ya filamu hiyo.

  Katika onyesho jipya la filamu hiyo, "Wife material" wa Eric Omondi inayojumuisha wahusika kutoka Kenya na Tanzania wanaonekana wakipigana hadharani na kulazimu polisi kuingilia kati.

  ''Vita hivyo'' vilianza wakati mmoja wa warembo hao aliangusha meza na kuvunja glesi zilizokuwa mezani na kumwaga vileo.

  Kanda ya filamu hiyo iliyosambazwa mitandaoni imeibua mjadala mkali baadhi ya mashabiki wake wakiuliza ikiwa ni uigizaji au ni uhalisia.

  Hatua hiyo imemghadhabisha Mkuu wa KFCB, Ezekiel Mutua, aliyetaja kuwa filamu “iliyooza"

  Aidha Bw. Mutua amesema Bodi itachukua hatua zote zinazowezekana za kisheria kuzuia utengenezaji na maonyesho ya filamu zisizoruhusiwa kwenye jukwaa lolote linalokusudiwa kuwa maonyesho ya umma.

 5. Video content

  Video caption: Swift ailamu filamu ya Netflix kwa 'unyanyasaji wa kijinsia' katika filamu ya ucheshi

  Mwanamuziki Taylor swift ameulaumu mtandao wa filamu wa Netflix kwa kuwadunisha wanawake.

 6. Video content

  Video caption: Najma Makena: Watu hufikiri kazi ninayofanya ni ya kishetani

  Najma Makena ni mwanamke wa Kisomali anayeishi Nairobi Kenya ambaye amekuwa akitengeza mapambo ya kuogofya tangu 2018.

 7. Video content

  Video caption: Netflix kuonyesha filamu ya Shawn Mendes itakapo kuwa tayari November 23

  Filamu inayoelezea maisha ya mwanazmiki Shawn Mendes ya "In Wonder" sasa itaonyeshwa kupitia mtandao wa Netflix

 8. Video content

  Video caption: Dwayne "the Rock" Johnson asema yeye na familia yake walipata Covid-19.

  Muigizaji maarufu Dwayne "the Rock" Johnson asema yeye na familia yake walipata ugonjwa wa Covid-19.