Chad

 1. Rais Paul Kagame azungumza na kaka wa Mahamat Idriss Déby

  Yves Bucyana

  BBC Swahili

  Kagame

  Rais Paul Kagame amempokea kwa mazungumzo Abdelkerim Déby Itno kama mjumbe maalum na mkuu wa ofisi ya rais wa Baraza la Jeshi la Mpito nchini Chad, kulingana na ofisi ya Rais wa Rwanda.

  Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu mazungumzo hayo ya Jumatano jioni.

  Bwana Kagame anajulikana kama mmoja wa wale ambao walikuwa na uhusiano mzuri na makubaliano juu ya maswala yanayohusu bara la Afrika na Rais wa zamani wa Chad Idriss Déby Itno.

  Utawala wa kijeshi nchini Chad sasa unatishiwa na shinikizo kutoka kwa jamii ya kimataifa na Jumuiya ya Afrika kutaka wanajeshi warudishe madarakani kwa raia.

  Barala kuu la kijeshi linaloongoza Chad pia liko kwenye vita na vikundi vya waasi,ikiwa ilidaiwa kuwa Rais wa zamani Idriss Deby Itno alipigwa aliuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa akipigana kwenye vita hivyo mwezi uliopita.

  Rais Kagame alipokea ujumbe wa Chad akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya nje Vincent Biruta na Meja Jenerali Joseph Nzabamwita, mkuu wa idara ya ujasusi (NISS).

  Kwenye mitandao ya kijamii, wengine walisema kuwa kuonekana kwa Abdelkerim Idriss Déby kama balozi wa kaka yake mkubwa Jenerali Mahamat Idriss Déby ilikuwa ishara kwamba "familia ya Déby inaendelea kuimarisha utawala wake’’ Kabla na baada ya kifo cha mzee Déby, kuliripotiwa malumbano kati wanawe kuhusu atakayemrithi.

  Abdelkerim Idriss Déby, 29, alihitimu kutoka Chuo cha Jeshi cha Marekani (USMA) huko West Point mnamo 2015. Mnamo mwaka wa 2019 aliteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa ikulu ya Rais wa Chad.

  Mnamo mwaka wa 2020, aliongoza ujumbe wa Chad uliokutana na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kujadili "kufungua" ubalozi wa Chad mjini Jerusalem.

 2. Mwanahabari wa Chad atoweka baada ya kuangazia maandamano

  Mwanahabari mmoja nchini Chad ametoweka siku kadhaa baada ya kuangazia taarifa ya maandamano, kundi la kutetea haki za binadamu nchini humo limesema.

  Moïse Dabsene alikamatwa wakati wa maandamano ya tarehe 20 na kuachiliwa siku hiyo hiyo.

  Familia yake imenukuliwa na kundi la Chad CTDDH ikisema kwamba mara ya mwisho yeye kuonekana ilikuwa tarehe 25 Machi.

  Kundi hilo linasema hayuko katika kituo chochote cha polisi na kutoa wito aachiliwe huru ikiwa amekamatwa.