Hillary Clinton

 1. Huma Abedin: Msaidizi wa Clinton aeleza jinsi alivyonyanyaswa kingono na senata

  m

  Msaidizi wa zamani wa Hillary Clinton ametoa ripoti ya maandishi kueleza namna alivyonyanyaswa na seneta.

  Huma Abedin alisema mwanasiasa huyo ambaye jina lake halikutajwa , alimsukuma kwenye kochi lake mnamo katikati mwa miaka ya-2000s baada ya kumkaribisha nyumbani kwake, kwa mujibu wa Guardian.

  Alikuwa akimkatalia wakati alipojaribu kumbusu na kufanikiwa kumtoroka.

  Madai hayo ameyaweka kwenye kitabu chake kipya, Both/And: A Life in Many Worlds, ambacho kinachapishwa wiki ijayo.

  Bi. Abedin alikuwa msaidizi aliyeaminika na mgombea wa urais mwaka 2016 kupitia chama cha Democratic bi. Clinton na alikuwa anamuelezea kama binti yake wa pili.

  Bi Abedin, ambaye ana miaka 45 sasa, hajasema jina la seneta wala chama chake.

  m

  Kwa mujibu wa the Guardian, gazeti ambalo linaonekana kuwa lilipewa nakala ya kile ambacho bi Abedin amekiandika:

  "Nilipata mshtuko mkubwa sana, nilimsukuma.Nilichokuwa nakitaka ni sekunde 10 za kumkimbia."

  m
  Image caption: Bi Abedin aliachana na mume wake baada ya kupata kashfa za ngono

  Bi Abedin anasema senata huyo aliomba radhi na kumueleza kuwa hakumwelewa kama alikuwa anataka kukaa au la.