Kujitosheleza kwa Chakula

 1. Juisi za Apple zaondolewa sokoni katika mataifa saba ya Afrika

  apple

  Juisi ya Apple (tufaha) inayotengenezwa na kampuni ya Afrika Kusini ya Ceres imeondolewa sokoni katika mataifa saba ya Afrika kwa sababu ya kuwa na kiwango cha juu cha sumu ambayo inaweza kusababishia mtu kutapika na kupata kichefuchefu.

  Juisi hizo zina aina ya sumu inayotolewa na baadhi ya kuvu{fungi} katika tufaha na bidhaa zake.

  Uchunguzi wa maabara unaonesha kuwa juisi za Ceres zina kiwango kikubwa cha sumu zaidi ya kiwango kinachoruhusiwa kisheria 50 microgrammes kwa lita moja.

  Juisi hizi zinauzwa Kenya, DRC, Zambia, Zimbabwe, Uganda, Seychelles na Mauritius.

  Juisi hii ina soko kuu katika nchi za Mashariki na Kusini (Comesa) na wateja wametakiwa kurudisha juisi zilizonunuliwa tangu tarehe 14 na 30 Juni 2021

 2. Video content

  Video caption: Fahamu jinsi mlo wa miguu ya kuku unavyopendwa na Watanzania

  Biashara ya miguu ya kuku imezidi kushika kasi hasa ukizingatia ni Chakula kinachopendwa sana na familia nyingi nchini Tanzania.

 3. Video content

  Video caption: Fahamu chakula cha Loshoroo, maarufu kaskazini mwa Tanzania

  Katika mfululizo wa makala za chakula eneo la Afrika mashariki leo tunaangazia Loshoro, chakula maarufu Kaskazini mwa Tanzania

 4. Video content

  Video caption: Je senene ni watamu kuliko Nyama?

  Wadudu hawa wanapatikana pia katika maeneo mengine ya Afrika Mashariki kama Uganda na Rwanda.

 5. Kim Jong-un akiri kuna 'uhaba' wa chakula Korea Kaskazini

  Kubadilika kwa muonekano wa Kim Jong-un imesababisha uvumi zaidi juu ya afya yake
  Image caption: Kubadilika kwa muonekano wa Kim Jong-un kumesababisha uvumi zaidi juu ya afya yake

  Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amekiri rasmi kuwa nchi hiyo inakabiliwa na uhaba wa chakula.

  Akiwahutubia maafisa wa ngazi ya juu nchini humo, Bw. Kim alisema "hali ya chakula majumbani mwa watu kwa sasa ni ya kutia wasiwasi".

  Alisema sekta ya kilimo imeshindwa kufikia malengo yake kutokana na tufani ya mwaka jana iliyosababisha mafuriko.

  Kuna ripoti kwamba bei ya chakula imepanda, huku shirika la habari la Korea Kaskazini likiripoti kilo moja ya ndizi inagharimu dola 45 za Kimarekani.

  Korea Kaskazini imefunga mipaka yake ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya Covid-19.

  Bishara kati yake na China imeporomoka sana kutokana na hatua hiyo. Korea Kaskazini inategemea China kwa chakula, mbolea na mafuta.

  Korea Kaskazini pia inalemewa na vikwazo vya kimataifa, vilivyowekwa kwa sababu ya mipango yake ya nyuklia.

  Kiongozi huyo wa kimabavu wa serikali ya chama kimoja alizungumzia hali ya chakula katika mkutano wa kamati kuu ya Chama cha Wafanyikazi ambayo ilianza wiki hii katika mji mkuu Pyongyang.

  Hadi kufikia sasa, Korea kaskazini inadai kuwa kufunga mipaka yake kumefanya waepuke ugonjwa wa virusi vya corona, ingawa wachambuzi wanatilia mashaka madai hayo.

  Soma zaidi:

 6. Video content

  Video caption: Mkoa wa katavi Tanzania waanzisha bucha maalumu ya kuuza nyama ya wanyamapori

  Mkoa wa Katavi kusini Magharibi mwa Tanzania , umeanzisha bucha maalumu ya kuuza nyama pori, biashara ambayo ni adimu Afrika Mashariki

 7. Watu 35 wafariki baada ya kula 'mimea ya porini' Msumbiji

  Ramani

  Watu 25 wa familia moja ni miongoni mwa watu 35 waliofariki kaskazini mwa Msumbiji baada ya kuripotiwa kula mimea na matunda ya mwituni, mamlaka zinasema.

  Maafisa wanasema hivi karibuni kumeripotiwa visa vya watu katika eneo hilo kula matunda ya mwituni, mizizi na hata nyasi.

  Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na televisheni ya kitaifa , TVM, wakazi wamekua wakisaga nyasi kupika xima – uji wa kienyweji wa Msumbiji, ambao hutengenezwa kutokana na unga wa mahindi.

  Uhaba wa chakula katika mkoa wa Nampula umechangiwa na ukosefu wa mvua.

 8. Video content

  Video caption: Wangeci Waruire: Mwanamke Mkenya anayewalisha Wakenya walipoteza kazi Dubai

  Mwanamke Mkenya amekuwa akipika chakula na kuwapatia Wakenya wenzake wanaoishi katika miliki za kiarabu UAE waliopoteza kazi kutokana na mlipuko wa corona