Dini

 1. إدوارد الثامن

  Miaka 100 iliyopita , Bombay (ambayo kwa sasa inafahamika kama Mumbai) ilishuhudia mojawapo ya fujo za ajabu katika historia ya India ambapo Watu wa madhehebu ya Kihindu na Waislamu waliungana pamoja na kushirikiana kupigana dhidi makundi mengine ya kidini, kulingana na Mwanahistoria Dinyar Patel, ambaye aliandika kuhusu funzo ambalo India ilijifunza hadi leo kutoka na tukio hilo.

  Soma Zaidi
  next
 2. Marekani yaiondoa Nigeria katika orodha ya wanaokiuka dini

  Nigeria haimo katika orodha ya 2021 ya nchi zinazochukuliwa kukiuka uhuru wa kidini
  Image caption: Nigeria haimo katika orodha ya 2021 ya nchi zinazochukuliwa kukiuka uhuru wa kidini

  Marekani imeiondoa Nigeria katika orodha ya wanaokiuka dini, kabla ya ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken nchini humo.

  Serikali ya Marekani mwaka jana iliiweka Nigeria katika orodha yake maalum ya waangalizi wa mataifa ambayo yaliendekeza ukiukwaji mkubwa wa uhuru wa kidini.

  Nigeria haimo katika orodha ya 2021 ambayo ina Myanmar, China, Eritrea, Iran, Korea Kaskazini, Pakistan, Russia, Saudi Arabia, Tajikistan na Turkmenistan.

  Algeria, Comoro, Cuba, na Nicaragua pia zimo kwenye orodha maalum ya serikali ambazo zimekiuka uhuru wa kidini, kulingana na idara ya masuala ya kigeni ya Marekani.

  Hata hivyo, makundi ya kijihadi ya Boko Haram na Iswap linaloendesha shughuli zake kaskazini-mashariki mwa Nigeria, bado yanatia wasiwasi.

  Bw Blinken anazuru Nigeria siku ya Alhamisi katika awamu ya pili ya safari yake ya mataifa matatu ambayo ni pamoja na Kenya na Senegal.

  Anatarajiwa kukutana na Rais wa Nigeria Muhamadu Buhari kujadili jinsi nchi zote mbili zinaweza kushirikiana zaidi katika afya ya kimataifa, usalama, kupanua upatikanaji wa nishati na ukuaji wa uchumi.

  Nigeria inapambana na vitisho vingi vya usalama, vikiwemo uasi wa muda mrefu wa Boko Haram, mapigano baina ya jamii na hivi karibuni, wimbi la utekaji nyara mkubwa shuleni unaofanywa na magenge yenye silaha.

  Soma:

  Fahamu dini mpya inayozua mjadala Mashariki ya kati

  Je waraabu wanaipuuza dini?

 3. m

  Katika maadhimisho ya miaka kumi ya nyumba ya familia ya Misri , kampeni ya umoja wa kidini ilianza nchini humo , lakini Imamu mkuu wa Al -Azhar, Ahmed Al Tayyib , aliikosoa dini mpya ya Abrahamu inayodaiwa kuzua mjadala katika eneo la mashariki ya kati.

  Soma Zaidi
  next
 4. GETTY IMAGES

  Afisa wa ngazi ya juu nchini India Ram Gopal Varma, aliibua utata baada ya taarifa yake yenye utata kugonga vichwa vya habari hivi karibuni na picha yake kusambazwa kwenye mitandao ya habari ya kijamii. Alikwenda katika eneo la Warangal kwa ajili ya kuchukua picha za filamu pamoja na pombe zilizotolewa kama sadaka hekaluni kwa ajili ya kumpelekea mama yake katika hekalu la Wahindu la Kotamayasamma nchini humo.

  Soma Zaidi
  next