Zanzibar

 1. Video content

  Video caption: Zanzibar:Ala ya muziki iliyobeba urithi wa visiwa hivi

  Maulid Mkadam amepiga chombo hiki toka mwaka 1983 na anafurahi kuona kwamba vijana nao wamejifunza kupiga chombo hiki

 2. Video content

  Video caption: Mabadiliko ya tabianchi: Upandaji miti unavyoweka kutunza mazingira

  Athari za mabadiliko ya tabia nchi zinajadiliwa kila kona ya dunia na maeneo mbalimbali duniani tayari yanaona athari na moja kwa moja.

 3. Video content

  Video caption: Serikali iliingia madarakani katika kipindi kigumu sana kiuchumi-Dkt Mwinyi

  Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dokta Hussein mwinyi amesema uchumi wa Zanzibar uliathiriwa kwa kiasi kikubwa na Covid 19.

 4. Video content

  Video caption: Zanzibar:“Baba aliniambia nilale chini kisha akaniingilia, na mama akasema ninyamaze'

  Kesi za udhalilishaji visiwani Zanzibar ni suala linalopigiwa kelele na viongozi wa kada mbalimbali.

 5. Video content

  Video caption: Virusi vya corona: Zanzibar yapinga kuwapa watu chanjo kisiri

  Serikali Visiwani Zanzibar imekanusha taarifa kwamba wameanza kutoa chanjo dhidi ya virusi vya corona

 6. Video content

  Video caption: Tanzania inajiandaa na tishio la wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya Corona

  Zanzibar ikiwa sehemu ya Tanzania ni miongoni mwa maeneo barani Afrika yanayopokea wageni wengi kutoka mataifa mbalimbali duniani

 7. Masheikh wa UAMSHO Tanzania wafanyiwa uchunguzi wa afya zao

  Dkt Saleh Ally
  Image caption: Dkt Saleh Ally akielezea hali ya Masheikh hao

  Mashekh na viongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), wako hospitali kwa uchunguzi na matibabu ikiwa ni siku moja baada ya kuachiwa huru.

  Wakili wao, Juma Abdallah amethibitisha kwamba masheikh 18 kati ya 36 wakiongozwa na Sheikh Fadid Ahmed, tayari wamefikishwa katika Hospitali ya Al-Rahma iliyoko Zanzibar kwa ajili ya uchunguzi wa afya zao na matibabu.

  Wengi wanaonekana kuwa na afya dhaifu kutokana na kukaa ndani kwa muda mrefu.

  Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), Sylvester Mwakitalu alitangaza kuwafutia mashtaka Mashekh hao wote 36 wa jumuiya hiyo, waliokaa gerezani kwa zaidi ya miaka 7.

  Hospitali ya Al-Rahma iliyoko Zanzibar wanakotibiwa baadhi ya masheikh
  Image caption: Hospitali ya Al-Rahma iliyoko Zanzibar wanakotibiwa baadhi ya masheikh

  BBC inaweza kuthibitisha kwamba mpaka sasa Mashekh 16 wameshatoka jela huku wengine 18 waliobaki walitarajiwa kutoka leo.

  Uamuzi huo wa kuwaachia huru masheikh hao umekuja siku chache baada ya Mahakama kuu kuwafutia mashitaka 14 kati ya 25 waliokuwa yakiwakabili, huku upelelezi wa kesi yao uliochukua zaidi ya miaka 7 huku wakiwa jela, ukilalamiukiwa na viongozi wa dini, baadhi ya wanasiasa hasa wa upinzani na wanaharakati wa haki za binadamu, waliodai hatua hiyo ni kama kuwadhulumu haki zao.

  Soma zaidi: