Uhuru Kenyatta

 1. Fahamu kwanini Naibu wa Rais wa Kenya anasema atamtegemea Mungu

  Siasa za ni nani atakayemrithi Rais Uhuru Kenyatta atakapoondoka madarakani zinaendelea kupamba moto nchini Kenya.

  Katika tukio la hivi punde Naibu wa Rais William Ruto ameonekana kusalimu amri baada ya kusema atamwachia Mwenyezi Mungu kumsaidia katika azma yake ya kuwania kiti cha urais wa nchi hiyo katika uchaguzi wa mwaka 2022, vyombo vya habari vimeripoti.

  Kwa Mujibu wa Gazeti la The Star, Rais Uhuru Kenyatta amesema atamuunga mkono mmoja wa viongozi wa muungano wa upinzani wa Nasa kugombea nafasi hiyo.

  Gazeti hilo linasema Rais alitoa kauli hiyo alipokutana na viongozi kutoka eneo la mashariki mwa Kenya katika Ikulu ya Nairobi.

  Katika hatua ambayo inaonekana kujibu kauli ya Rais Kenyatta,Bw. Ruto aliandika mtandao wa Twitter siku ya Jumanne kuelezea hisia zake akiambatanisha gazeti hilo.

  View more on twitter

  Dkt Ruto na wandani wake wamekosoa vikali kauli ya Rais Kenyatta wakihoji hatima ya Wakenya waliompigia kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

  Maelezo zaidi:

 2. Rais wa Kenya atangaza kazi kwa watengenezaji bunduki haramu

  Zaidi ya silaha haramu 5,000 zilizojisalimishwa wakati wa msamaha zilichomwa moto mwaka jana
  Image caption: Zaidi ya silaha haramu 5,000 zilizojisalimishwa wakati wa msamaha zilichomwa moto mwaka jana

  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa watengezaji bunduki haramu kujiunga na kiwanda kipya cha utengenezaji silaha nchini.

  Amesema salaha nyingi haramu zinazokamatwa na mamlaka za usalama zinatengezwa nchini.

  Rais amewaahidi watengenezaji silaha "uthabiti" wa kazi "kukuza uchumi na kusaidia kudumisha usalama wan chi yako”.

  Alisema wale wanaotaka kazi kuwasiliana na vyombo vya usalama kutoa huduma zao.

  Mnamo mwezi Aprili Kenya ilizindua kiwanda cha silaha mbacho kilijengwa kwa gharama ya dola milioni 36.

 3. Jaji Mkuu mwingine wa zamani Kenya amkosoa Rais Kenyatta

  David Maraga
  Image caption: Jaji Mkuu wa zamani wa Kenya David Maraga

  Hatua ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuwakataa majaji sita waliopendekezwa na Tume ya Hudama za Mahakama,JSC, imeendelea kuzua hisia mseto.

  Kiongozi wa hivi punde kutoa kauli yake kuhusiana na suala hilo ni Jaji Mkuu mshaafu David Maraga.

  Katika mahojiano na Kituo cha Televisheni cha KTN, Bwana Maraga alisema: ''Hali kama hii ikiendelea nchini itaongozwa bila katiba''

  Maraga amemtaka rais Kenyatta kuwateua majaji sita aliowaacha nje.

  ''Muda umewadia kwa bunge kumuondoa madarakani (Uhuru) akikiuka katiba'' aliongeza kusema.

  Majaji hao sita ni miongoni mwa majaji 41 ambao walikuwa wamependekezwa kwa ajili ya uteuzi na Tume ya Huduma za mahakama nchini humo (JSC) miaka miwili iliyopita. Mmoja wa majaji hao alifariki.

  Rais Kenyatta amekataa mapendekezo ya JSC licha ya maagizo mawili ya mahakama yaliyomtaka kufanya hivyo.

  Martha Koome: Mfahamu Jaji mkuu wa kwanza mwanamke Kenya

 4. 'Lazima tushirikiane na Kenya kwenye vita dhidi ya corona'

  Rais Samia

  Rais Samia Suluhu Hassan ameliambia Bunge la Kenya kuwa Tanzania itashirikiana na nchi jirani ikiwemo Kenya katika mapambano dhidi ya mlipuko wa corona.

  Rais Samia amewaambia wabunge na maseneta wa Kenya kuwa tayari Tanzania imeshaanza kuchukua hatua tahadhari juu ya corona ikiwemo kusitisha safari za moja kwa moja na nchi zenye kasi ya maambukizo ya corona.

  Akihutubia mkutano maalumu ulioandaliwa kwa ajili yake, amesisitiza kuwa Tanzania si kisiwa katika mapambano dhidi ya corona, na wakati ikisubiriwa mapendekezo kutoka kamati maalumu aliyoiunda, kitu ambacho ana hakika nacho ni lazima kushirikiano na majirani.

  "Lazima tushirikiane na majirani katika vita dhidi ya corona, lazima tushirikiane na kenya katika hili," amesema Rais Samia.

 5. Rais Samia alihutubia Bunge la Kenya

  Rais Samia Bungeni

  Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amehutubia kikao cha pamoja cha Bunge la taifa na Bunge la Seneti nchini Kenya.

  Rais Samia amekuwa nchini Kenya kwa ziara ya siku mbili ya kikazi.

  Ziara yake ni muendelezo wa jitihada za nchi hizo mbili kuboresha na kuendeleza uhusiano wa muda mrefu.

  Bunge la Kenya

  Soma zaidi:

 6. Kenyatta: Mahindi yaliyokwama mpakani yaruhusiwa kuingia nchini

  Rais Kenyatta

  Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amemuagiza waziri wake biashara kuondoa msongamano wa bidhaa katika mpaka ya Kenya na Tanzania.

  Bw. Kenyatta ametoa muda wa wiki mbili mahindi yote yaliyokwama mpakani kuruhusiwa kuingia nchini.

  ''Hiyo mahindi imelala hapo mpakani,Waziri mimi nakupatia wiki mbili…yote ifunguliwe na hiyo maneno iishe'' alisema.

  Kenyata ametoa tamko hilo leo mbele ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakati wa kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya linaloendelea jijini Nairobi.

  Mlolongo mrefu wa malori ya kubeba mizigo
  Image caption: Mlolongo mrefu wa malori ya kubeba mizigo

  Mapema mwezi Machi Kenya ilipiga marufuku ununuzi wa mahindi kutoka mataifa jirani ya Tanzania na Uganda.

  Uamuzi huo ulifikiwa baada ya uchunguzi kubaini kwamba mahindi kutoka mataifa hayo mawili sio salama kwa matumizi ya chakula cha binadamu.

 7. Rais Kenyatta na Samia wafanya mazungumzo ya faragha

  Rais Samia na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta

  Rais Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Uhuru Kenyatta wa Kenya wapo katika mazungumzo ya faragha katika Ikulu ya Rais, jijini Nairobi.

  Mama Samia amewasili asubuhi ya leo jijini Nairobi na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kabla ya kuelekea Ikulu ambapo alipokelewa na Bwana Kenyatta.

  Mazungumzo hayo ya ndani yanatazamiwa kuhususisha masuala mbalimbali kipaumbele kikiwa ni kukuza ushirikiano wa kibiashara na mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili jirani.

  Baada ya mazungumzo hayo, marais hao wawili wanatarajiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari na kueleza baadhi ya mambo waliyokubaliana.

  Rais Samia yupo Kenya kwa ziara ya siku mbili na hapo kesho mchana anatarajiwa kuhutubia Bunge la Kenya.

  Soma zaidi: