Elimu

 1. Mwanataaluma asimamishwa kazi Tanzania kwa tuhuma za rushwa ya ngono

  University of Dodoma

  Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) nchini Tanzania kimetoa taarifa kwa umma kujibu tuhuma dhidi ya mwanataaluma wa chuo hicho.

  Taarifa hiyo inasema "chuo kilipokea kwa masikitiko makubwa taarifa za tuhuma dhidi ya mtumishi wake ndugu Petro Bazil Mswahili ambaye ni Mwanataaluma juu ya kujihusisha na rushwa ya ngono kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma".

  Chuo hicho kimesema, mwalimu huyo amesimamishwa majukumu yake yote kuanzia Oktoba 25 mwaka huu hadi uchunguzi utakapokamilika.

  Tayari , Chuo kimeanzisha mchakato wa hatua za kinidhamu na maadili kulingana na sheria na kanuni za utumishi wa umma.

  Aidha, Chuo kinapenda kuutaarifu Umma kuwa kitendo hiki hakivumiliki wala kukubalika na kwamba wakati wote Chuo kitaendelea kusimamia nidhamu na maadili kwa watumishi wake wote.

  Pia, Chuo kitaendelea kuchukua hatua kali kwa mtumishi yeyote atakayebainika kujihusisha na makosa ya kinidhamu. Chuo kimesikitishwa sana kwa usumbufu uliojitokeza.

 2. Wanafunzi walivamia bunge DRC wakitaka walimu wao waongezewe mshahara

  m

  Mamia ya wanafunzi wamelivamia bunge nchini DRC wakitaka walimu wao waongezewe mshahara.

  Wanafunzi hao walikuwa wanapeperusha matawi na kuimba "tunataka kusoma" na "ikiwa hatutasoma, tutatumia dawa za kulevya".

  Maandamano ya aina hiyohiyo yalitokea katika mji wa Beni kaskazini mwa Kivu ,kwa mujibu wa radio inayomilikiwa na Umoja Mataifa- Radio Okapi.

  Walimu wamekuwa katika mgomo tangu Oktoba 4, mwanzoni mwa masomo mwaka huu wakitaka waongezewe mshahara na kupunguza umri wa kustaafu pamoja na masuala mengine.

  Serikali imewashutumu viongozi wa dini ambao wanasimamia shule nyingi za msingi , kwa kudai kuwa wanahusika na mgomo huo ingawa viongozi hao wamekanusha madai dhidi yao.

  Makamu wa rais wa Jamuhuri ya demokrasia ya Kongo Jean-Marc Kabunda, amewataka wanafunzi kurudi nyumbani maana haya sio mapambano yao.

  "Nyinyi sio watu wa mtaani, mnapaswa kuwa shuleni na kama hampo shule mnapaswa kuwa nyumbani," alisema.

 3. Video content

  Video caption: Africa Eye: Watoto wa Nigeria wanaotekwa nyara

  Kumeshuhudiwa jumla ya matukio tisa makubwa ya utekaji katika ajimbo matano

 4. Video content

  Video caption: 'Nilimpeleka mwanangu shule za Binafsi kupitia kuuza uji mitaani'

  Ni hadithi ya kusisimua ya Bi Basila Swai mkazi wa Jiji la Kibiashara la Dar Es Salaam ambaye hakutaka ugumu wa Maisha aliyoyapitia uwe kikwazo cha mwanae mpendwa kwenda shule na h