Biashara

 1. Tanzania yaridhia mkataba wa eneo huru barani Afrika

  Eagan Salla

  BBC Swahili, Dar es Salaam

  Viwanda

  Tanzania imeridhia mkataba eneo huru la biashara kwa mataifa 54 barani Afrika lengo likiwa ni kupanua wigo wa kibiashara na kuongeza nafasi za ajira kwa vijana.

  Akiongea na waandishi wa habari waziri ofisi ya waziri mkuu uwekezaji Jeofrey Mwambe akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam amesema serikali ina nia ya kuimarisha uwekezaji ili kuwa na uchumi imara.

  Bwana Mwambe amesema taifa hilo limejizatiti kuimarisha uwekezaji ikiwa ni pamoja na kufanyia marekebisho sera ya uwekezaji ya mwaka 1996 na sheria ya uwekezaji ya mwaka 1997 ili kutengeneza mazingira rafiki jwa wawekezaji wote wa nje na wandani.

  Siku za nyuma kumekuwa na kusigana kwa serikali ya Tanzania na baadhi ya wawekezaji akiwemo bilionea Aliko Dangote mgogoro ambao waziri Mwambe anasema tayari wameshapatia ufumbuzi changamoto nane kati zilizokuwa zinazorotesha uwekaji wake nchini Tanzania.

  Baada ya kuingia madarakani Rais Samia Suluhu hasana amefanya ziara kadhaa kwenye maitaifa jirani akinuia kuboresha mahusiano mema na kukuza ushirikiano wa kibiashara, siku za hivi karibuni alizunguka maeneo mbalimbali ya taifa hilo kuandaa makala ya “the royal tour” akilenga kuvitangaza vivutio vya utalii na kuonesha fursa za uwekezaji zilizopo kote nchini.

  Waziri Mwambe amesisitiza juu ya watendaji wote wa serikali kuwajibika ipasavyo kuwahudumia wawekezaji na kuondoa urasimu usio wa lazima ili kuharakisha uwekezaji kwani kwa kufanya hivyo Tanzania itatengeneza ajira zaidi kwa vijana na kujiimarisha kiuchumi.

  Fahamu njia zinazoweza kukwamua hali ya uchumi na biashara Tanzania

  Tanzania:Uchumi wa Tanzania umestahimili vipi athari za corona?

 2. Video content

  Video caption: Onesmo Mbasha: Tazama jinsi biashara ya kuuza uume wa ng'ombo inavyomtajirisha Mtanzania h

  Onesmo Mbasha ambaye zamani alikuwa mfanyabiashara wa mavazi sasa anajipatia mamilioni ya fedha kwa kuuza uume wa ng'ombe kwa Wachina ambao wao wanadai wanautumia kutengeneza nyuzi

 3. Video content

  Video caption: Je unaweza kuishi katika nyumba zinazoandamwa na mapepo?

  Japan ni taifa ambalo watu wengi wanaamini mapepo

 4. young woman rhinoplasty stock photo

  Sawa na vijana wa rika yake Ruxin mwenye umri wa miaka 23 anapenda kuangalia mara kwa mara mitandao ya kijamii inayotoa matangazo ya moja kwa moja kila siku, lakini huangalia kitu maalum- taarifa za hivi karibuni kabisa za upasuaji wa kubadilisha au kurekebisha maumbile ya mwili.

  Soma Zaidi
  next
 5. Rais Samia awafukuza kazi maafisa wawili kwa kuwaonea wafanyabiashara

  Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewafukuza kazi Mkuu wa wilaya pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa na Sheilla Lukuba, kufuatia tukio la hivi karibuni ambapo wafanyabiashara wadogo waliondolewa kwa nguvu katika eneo hilo.

  Rais Samia ametangaza uamuzi huo mkoani Mwanza wakati wa mkutano wake na Vijana wa Tanzania.

  Rais alielezea kusikitishwa kwake na kitendo cha kuondolewa kwa nguvu kwa Wafanyabiashara hao, na kuongeza ingekuwa ni lazima Wafanyabiashara hao kuondolewa ingetumika njia nyingine na si nguvu na kuharibu bidhaa zao.

  ''Wafanyabiashara hao walitengewa eneo la mbali kwa ajili ya kufanya biashara zao na walipoona hakuna biashara waliamua kurudi maeneo ya mjini na ndipo walipoanza kuondolewa kwa nguvu'', alisema

  Amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu kusimamia jambo hilo.

  Wiki iliyopita Rais Samia alimfuta kazi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila aliyetaka wananchi wabebe mabango kumkaribisha.

 6. Habari za hivi pundeMfanyabiashara maarufu wa Kenya Chris Kirubi afariki dunia

  Chris Kirubi

  Mtaalamu mashuhuri wa viwanda na mmoja wa wafanyabiashara tajiri zaidi Afrika, Dkt Chris Kirubi amefariki dunia, familia yake imethibitisha.

  Dkt Chris Kirubi ambaye pia ni Mwenyekiti wa makampuni kadhaa ikiwemo ya habari ya Capital Group Limited, alikuwa akiugua saratani tangu mwaka 2016.

  Kirubi aliorodheshwa na jarida la Forbes kuwa Mkenya wa pili kwa utajiri mwaka 2011 katika orodha iliyojumuisha familia ya kiongozi mwanzilishi wa nchi hiyo, Marehemu Rais Jomo Kenyatta.

  Alifanikiwa pia kushika nafasi ya 40 ya tajiri zaidi barani Afrika baada ya katika nafasi ya 31, mali yake ikiwa na thamani ya dola milioni 300.

  Bw. Kirubi atakumbukwa kwa kuwahimiza vijana kujiamini wanaweza bila kujali walikotoka akiongeza kwamba yeye pia alinzia chini na kufikia upeo wa maisha yake, baada ya kufiliwa na wazazi wake akiwa na umri mdogo.

  “Haijalishi ulikotoka. Hata kama unaishi kwenye mabanda. Hatma ya maisha yako iko mikononi mwako,” alisema.

  Kirubi pia amekuwa akitumia mtandao wa kijamii wa Twitter kuwahamasisha vijana kujiepusha na watu ambao huenda wakawa kikwazo katika ndoto ya ufanisi maishani mwao.

 7. Video content

  Video caption: Jinsi uteute wa konokono unavyoweza kulainisha ngozi na kuzuia usizeeke

  Jinsi wataalamu wa urembo wanavyolikimbilia soko la ute wa konokono ili kutibu na kulainisha ngozi.