Dawa

 1. Morocco yahalalisha bangi ya dawa

  Bangi

  Bunge nchini Morocco limeidhinisha sheria inayohalalisha ukuzaji wa bangi kwa ajili ya matumizi ya tiba na viwandani.

  Lengo ni kuingia katika soko la kimataifa linalokua la kimataifa, kukuza kilimo na kutoa ajirahasa katika maeneo ya vijijini ambayo hayana maendeleo.

  Morocco ni moja nchi zinazokuza bangi kwa kiwango kikubwa kwa matumizi haramu. Hii itasalia kuwa haramu chini ya sheria mpya.

  Madhara ya Bangi

  • Unaweza kusababisha kuchanganyikiwa na wasiwasi usio wa kawaida
  • Ikivutwa na tumbaku, inaweza kuongeza hatari ya ugonjwa kama vile saratani ya mapafu
  • Matumizi ya mara kwa mara yamehusishwa na hatari ya kupatwa na magonjwa ya kiakili
  • Upungufu wa kudumu wa kiwango cha mtu kufikiria na kufahamu mambo, baada ya kutumia kwa muda mrefu

  Maelezo zaidi:

 2. Video content

  Video caption: Dawa za kutengeneza mwili wenye 'Umbo namba nane' zilivyohatarisha maisha ya wanawake

  Dawa za kutengeneza mwili wenye 'Umbo namba nane' zilivyohatarisha maisha ya wanawake

 3. Rais Kenyatta awafukuza wakurugenzi wote wa bodi ya usambazaji wa dawa

  kenya

  Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewafukuza kazi wakurugenzi wote wa bodi ya wakala wa usambazaji wa dawa.

  Hatua hii imekuja baada ya KEMSA kukabiliwa na kashfa kadhaa miaka ya hivi karibuni – ikiwemo ya vifaa vya kujikinga na Covid-19.

  Huku usambazaji wa dawa ukiainishwa kuwa miongoni mwa sababu zilizosababisha.

  Kashfa ya hivi karibuni ilihusisha dozi elfu ishirini na nne ya dawa za kupunguza makali ya Ukimwi ambazo tayari zimeondolewa kwa umma.

  Kenya imesitisha matumizi ya Nevirapine mwaka 2019 baada ya wagonjwa kuanza kuathirika na dawa hizo.

  Wakala hao ni sehemu ya sababu ya kwanini zaidi ya dozi 200,000 za dawa ya anti-retroviral zimekwama katika ghala iliyopo Mombasa, miezi minne baada ya US-AID kutoa msaada.

  Mwaka jana, KEMSA ilishutumiwa kutumia vibaya mamilioni ya dola kununua vifaa kinga vya Covid-19.

  Hata hivyo wakala hao wanatarajiwa kurudisha imani kwa umma.

  Na Bodi mpya inatarajiwa kuanza kazi wiki tatu zijazo.

 4. Tanzania kuchunguza kampuni 'inayonunua mikojo ya wanawake wajawazito'

  Mkojo

  Mamlaka ya dawa na vifaa Tiba (TMDA) Tanzania inachunguza kampuni moja ambayo imedaiwa kukusanya mikojo ya wanawake wajawazito ili kutengeneza tiba ya mwanadamu, kulingana na gazeti la The Citizen nchini humo.

  Mamlaka ya (TMDA) imenukuliwa ikisema haitambui na haijawahi kusajili kampuni ya Polai (Tz) – ambayo inasemekana kuhusika na sakata hiyo.

  Gazeti la The Citizen limeripoti kwamba uchunguzi wake unaonesha ukusanyaji wa mkojo uliokuwa ukifanywa kisiri.

  Mkojo

  Gazeti hilo limemnukuu mfanyakazi wa kampuni hiyo aliyekiri kwamba imekuwa ikikusanya mikojo ya wanawake wajawazito kwa utengenezaji dawa zenye kuhusishwa na ugumba.

  Hakuna utafiti wowote wa kisayansi unaonesha kwamba mkojo unafaida za kitiba.

  Mamlaka ya TMDA imesema itachukua hatua stahiki baada ya kumaliza uchunguzi wake.

 5. Video content

  Video caption: Virusi vya Corona: Kutana na Msafiri Njema aliyebuni mfumo kujifukiza jijini Dar es Salaam

  Wakati dunia ikiendelea kupambana na virusi vya Corona, Mtanzania Msafiri Mjema amebuni mfumo rahisi wa kujifukiza alioupa jina la Aspera Covid 19 Nyungu,

 6. Video content

  Video caption: Amazon yafungua duka la mtandaoni

  Kampuni kubwa ya Mauzo,Amazon imezindua duka la dawa kupitia mtandao ambalo litawaruhusu wateja wake kununua dawa.

 7. Mkono wa mtoto uliokatwa waunganishwa tena

  Benevolence Iticha
  Image caption: Benevolence Iticha akionesha mkono wake uliounganishwa tena

  Madaktari nchini Kenya katika hospitali kuu ya Taifa ya Kenyatta wamefanya upasuaji wa kipekee kwa mara ya tano na kufanikiwa kurejesha mkono uliokuwa umevunjika mahali pake, upasuaji huo wa hivi karibuni ukiwa ni kijana wa miaka saba ambaye mkono wake ulikatwa kwa bahati mbaya wiki tatu zilizopita.

  Benevolence Itachi mkono wake ulikatwa Oktoba 4, 2020, na mkataji wa makapi na kukimbizwa mara moja katika hospitali ya Nazareth iliyoagiza apelekwe hospitali ya taifa ya Kenyatta.

  Mkuu wa upasuaji Dkt. Benjamin Wabwire aliwaambia wanahabari siku ya Jumatano kwamba mchakato huo ulichukua saa 10 na kujumuisha timu ya wataalamu wa kurekebisha maumbile.

  Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta
  Image caption: Hospitali ya taifa ya Kenyatta ikizungumza na wanahabari

  “Mkono wake ulihifadhiwa katika eneo baridi na walifanikiwa kufika hospitali kwa wakati, Benevolence akiwa mwenye umri wa chini zaidi kukiwa na matumaini kwamba ubongo wake utaendelea kuitikia mabadiliko hayo na ataweza kuendelea kufanya kazi zake kama kawaida wakati anapoendelea kupata nafuu,” alisema.

  Daktari D. Wabwire alisema kuwa changamoto kubwa kwa ajali kama hizo ni muda kwasababu mafanikio ya upasuaji yanategemea wakati alipokatwa mkono na muda mwathirika anawasili hospitali.

  “Changamoto kubwa imekuwa muda kwa sababu wanahitajika kufika ndani ya muda ili tuweze kuunganisha tena the msukumo wa damu katika ehemu iliyokatwa,” amesema Dkt. Wabwire.