Uhifadhi (Maumbile na maliasili)

 1. Simba ahasiwa baada ya kuzalisha watoto wengi

  Simba

  Simba mmoja katika hifadhi ya wanyama nchini Uholanzi amehasiwa baada ya kuzaa watoto watano mwaka jana.

  Simba huyo mwenye umri wa miaka 11, anayeitwa Thor, aliwapachika mimba simba wawili. Wa kwanza alizaa mapacha, wakati wa pili alikuwa na watoto watatu.

  "Kwa nini tunafanya hivyo? Kwa sababu yeye ni ‘mzaaji’ aliyethibitishwa," daktari mkuu wa Zoo ya Royal Burgers huko Arnhem alisema.

  Hazina ya utunzi wa wanyama wa pori duniani imesema idadi ya samba walio porini imepungua kwa asilimia 20-30 katika miaka 20 iliyopita Lakini daktari wa wanyama Henk Luten, ambaye alifanya upasuaji huo Alhamisi, alisema hifadhi hiyo ya wanyama sasa ilikuwa na DNA ya kutosha kutoka kwa Thor.

  "Tuna watoto wengi wake na hatutaki kuzidisha DNA yake," aliliambia shirika la habari la Reuters.

  Ingawa sio jambo ambalo halijawahi kusikika , kufanyia simba vasektomi ni jambo nadra sana kutokea "Ni mara ya kwanza katika miaka 35 kuwa daktari wa mifugo hapa kumfanyia simba operesheni hii'' Bw Luten alisema.

  Aliamua kutumia vasektomi badala ya kuhasiwa kwa simba huyo kwa sababu utaratibu wa mwisho ungemfanya apoteze kidevu chake.

  Ukosefu wake wa testosterone baada ya kuhasiwa pia ungemfanya Thor apoteze nafasi yake katika uongozi wa kundi la kijamii na Simba katika Hifadhi hiyo Simba wametajwa kama waliopo hatarini ya kuangamizwa na WWF, ambayo inamaanisha wanakabiliwa na hatari kubwa ya kutoweka porini.

 2. Donald Trump amemuunga mkono rais wa Misri kuhusu bawa la Nile

  Kwa wakosoaji wake hatua ya Rais wa Marekani Donald Trump, kuongeza mvutano kati ya washirika wawili wa Marekani wa muda mrefu, Misri na Ethiopia, kuhusu bwawa kubwa la mto Nile ni ishara ya kufeli kwa diplomasia ya utawala wake barani Afrika.

  Soma Zaidi
  next
 3. Mabaki ya samaki maarufu wa Zambia 'yatoweka'

  Mafishi

  Mabaki ya 'Mafishi' – samaki maarufu wa Zambia ambaye kifo chake kimeombolezwa tangu Jumatatu – yametoweka mahali iliyokuwa imehifadhiwa.

  Samaki huyo aliishi kwenye kidimbwi cha Chuo Kikuu cha Copperbelt (CBU) kwa zaidi ya mwongo mmoja na wanafunzi walimchukulia kama chanzo cha bahati.

  Aliombolezwa na viongozi wakuu serikalini akiwemo rais Edgar Lungu na baadhi ya mawaziri wake.

  Naibu Chansela wa CBU Naison Ngoma, amethibitisha kutoweka kwa mabaki ya mafishi na kuongeza kuwa uchunguzi umeanzishwa kubaini kilichotokea, kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Zambia Daily Mail.

  “Nalifahamishwa kwamba samaki huyo alianza kutoa harufu mbaya kwenye jokovu Iakini nilipoulizia yuko wapi niliambiwa ametoweka’’alinukuliwa kusema.

  Prof Ngoma anasema huenda samaki huyo ameliwa au kutupwa.

  Ameongezea kuwa hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wale waliohusika na kutoweka kwa samaki huyo.

 4. Kambi ya watalii Kenya inayovuruga uhamaji wa nyumbu kufungwa

  Nyumbu

  Kambi ya watalii iliyojengwa karibu na Mto Mara nchini Kenya na ambayo ilizuia nyumbu wanaohama njia ya kupita itabolewa Alhamisi, kulingana na Seneta wa eneo hilo Ledama Ole Kina.

  Seneta huyo aliambia BBC kuwa inasikitisha kambi hiyo ilivuruga uhamiaji huo wa kila mwaka kwa muda mfupi lakini nyumbu hao waliendelea mbele na safari yao.

  "Kambi hiyo ilijengwa kinyemela kando ya mto na imekuwa hupo kwa zaidi ya siku 10, na ilijengwa katika njia ambayo haijawahi kupitiwa na nyumbu hao lakini mara hii kutokana na mvua inayonyesha kupitia hapo'' alisema bwana Ole Kina.

  Siku ya Jumatano Waziri wa Utalii wa Kenya Najib Balala, aliweka kwenye mtandao wa Twitter video inayoonesha jinsi mamia ya nyunbu hao ambao huwa kivutio kikubwa cha watalii wakijaribu kuvuka mto Mara, lakini wakarudishwa nyuma na watu walipokaribia kambi hiyo.

  View more on twitter

  Bw. Balala aliandika katika Twitter kwamba amezungumza na Gavana wa eneo hilo kuomba kambi hiyo ya watalii ‘’kuondolewa’’ kando ya mto huo ili kutoa njia ya wanyama hao kupita.

  Hatua hiyo imezua gumzo kali mitandaoni huku watu wakitumia mtandao wa kijamii wa Twitter kuelezea ghadhabu zao.

  Mmoja wao aliita ‘’chukizo’’ na mwengine kusema ni ‘’uharibifu mkubwa wa turathi yetu ".

  Uhamaji mkubwa wa nyumbu ni moja wapo ya Maajabu Saba mpya duniani.

 5. Video content

  Video caption: Mhifadhi wanyama afariki baada ya kushambuliwa na simba

  Mhifadhi wanyama maarufu nchini afrika kusini ameuwawa baada ya kushambuliwa na simba wawili weupe aliok uwa akiwatembeza.

 6. Video content

  Video caption: je, unatumai kuwa bahari zitasafika?

  Utafiti mpya wa kisayansi unasema kuwa licha ya bahari kufahamika kama jaa la taka kwa miongo kadhaa,juhudi za kusafisha zimeanza kuzaa matunda kote duniani.

 7. Na Peter Mwai

  BBC Reality Check

  Tree sapling next to muddy hands

  Serikali ya Ethiopia iliweka lengo la kupanda miche ya miti bilioni nne katika kipindi cha miezi mitatu pekee mwaka huu. Je, walifanikiwa?

  Soma Zaidi
  next