Shirika la Msalaba Mwekundu

 1. Uganda kumpatia ardhi mwanamuziki mashuhuri Marekani, Akon

  Isack Mumena

  BBC Swahili Kampala

  Museveni

  Waziri wa ardhi nchini Uganda Dkt.Chris Barayamunsi amewaambia wandishi wa habari pamoja na msanii huyo kuwa serikali inapatia aridhi ya ekari ya mraba mmoja katika eneo lolote ambalo mwanamuziki huyo atalitaka nchini humo.

  Mwanamuziki mashuhuri na mzaliwa Senegal, Akon aliwasili nchini Uganda mwishoni mwa juma akiambatana na mkewe Rozina Negusei, ambapo wanaenda kuwekeza Dolla milioni $12 nchini Uganda katika tasnia mitindo.

  Msanii huyo alikutana na Rais Museveni nyumbani kwake Rwakitura baada ya Museveni kumutumia Elikoputa ya jeshi la UPDF mwishoni mwa juma.

  Kwenye mkutano na wandishi habari hapo jana, Akon ameahidi kuwekeza nchini Uganda katika sekita ya utalii, nishati na miundo mbinu chini ya kampuni yake ya Akon Lighting Afrika.

  Pia ameahidi kutangaza jina la Uganda kimataifa, amesema jumuiya za kimataifa zinazungumza mabaya tu kwa Uganda yaliyofanywa katika utawala wa aliyekuwa rais wa zamani wa Uganda Idd Amin.

  Msanii huyo amechaguwa Uganda kuwa makao makuu ya mradi wake wa kuboresha miji barani Afrika yaani Acon City Projects mataifa mengine katika mradi huo ni Senegal anakozaliwa,Ghana na Ethiopia.

 2. Wanamgambo 'wawafurusha wenyeji' maeneo ya virusi Msumbiji

  Wanamgambo wamewafurusha maelfu ya watu kutoka majumbani mwao
  Image caption: Wanamgambo wamewafurusha maelfu ya watu kutoka majumbani mwao

  Makabiliano kati ya vikosi vya serikali ya Msumbiji na wanamgambo wa Kiislam kaskazini mwa mkoa wa Cabo Delgado yamewafanya wakazi kukimbilia maeneo yaliyo na viwango vya juu vya maambukizi ya corona kwa mujibu wa Shirika la kimataifa la Mslaba Mwekundu(IRCS).

  Baadhi ya wakimbizi hao wako Pemba ambako IRCS lilisaidia kujenga kituo cha matibabu ya virusi vya corona, linasema shirika hilo.

  Hali hiyo inawaweka katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi, anasemamkuu anayesimamia shughuli za IRCS mjini Pemba Raoul Bittel.

  Wanamgambo hao wamekuwa wakifanya mashambulio katika maeneo ya vijijini katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

  Kundi hilo linaloitwa al-Shabab au vijana na wenyeji– linaendesha ajenda za kijihadi lakini limekuwa likitumia changamoto miongo kadhaa zinazokabili jamii kama vile ukosefu wa kazi, udanganyifu katika uchaguzi, ufisadi na ghasia kujiimarisha.