Nguvu za Nyuklia

 1. Rais mpya wa Iran Ebrahim Raisi kuapishwa

  Ebrahim Raisi (right) is close to Iran's Supreme Leader Ayatollah Khamenei

  Rais mpya wa Iran Ebrahim Raisi,anatarajiwa kuapishwa rasmi kuingia madarakani baada ya kushinda uchaguzi mwezi Juni.

  Bw. Raisi, mhubiri mwenye misimamo mikali anamrithi Hassan Rouhani, alionekana na nchi za magharibu kuwa na misimamo ya kadri.

  Anaingia madarakani wakati ambapo changamoto zinazoikabili Iran zinaendelea kuongezeka kutokana na vikwazo vya kimataifa vilivyolemaza uchumi wake.

  Mvutano pia ulioongezeka kati ya nchi hiyo na mataifa ya kigeni ambayo yanailaumu Iran kwa shambulio baya la ndege isiyokuwa na rubani dhidi ya meli ya mafuta karibu na Oman wiki iliyopita, ambayo Iran imekanusha.

  Watu wawili - walinda usalama wa Uingereza na Kiromania - waliuawa wakati meli ya MV Mercer, inayomilikiwa na Israel iliposhambuliwa. Uingereza, Amerika na Israel zinailaumu Iran kwa kutekeleza shambulio hilo.

  Mvutano kati ya Iran na Marekani umeongezeka tangu 2018, wakati Rais wa wakati huo Donald Trump alipoondoa nchi hiyo katika mkataba wa wa kimataifa juu ya mpango wa nyuklia wa Iran na kurudisha vikwazo.