Biashara (Uuzaji na Ununuzi)

 1. Rais Samia ataka Tanzania kujiandaa kwa matumizi wa sarafu ya kidijitali

  President Samia told the Bank of Tanzania on Sunday to be vigilant on digital currencies

  Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa nchi hiyo kujiandaa kutumia ya sarafu za mauzo ya mtandaoni, maarufu Bitcoin.

  Samia aliiambia Benki Kuu ya Tanzania,siku ya Jumapili kuwa macho wakati ambapo kumekuwa na ongezeko la matumizi ya sarafu hiyo kote duniani.

  "Najua nchi nyingi duniani hazijaanza kutumia sarafu za mauzo ya mtandaoni. Hata hivyo, natoa wito kwa Benki ya Kuu ya Tanzania kuaanza kufuatilia yanayojiri na kujiandaa.

  "Hatutaki kupatikana ghafla au kufahamu baadae kwamba raia wako mbele yetu na wameaanza kutumia sarafu za kidijitali," alisema.

  El Salvador wiki iliyopita ilikuwa nchi ya kwanza duniani kuorodhesha rasmi sarafu ya kidijitali, Bitcoin, kuwa sarafu halali.

 2. Kenyatta: Mahindi yaliyokwama mpakani yaruhusiwa kuingia nchini

  Rais Kenyatta

  Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amemuagiza waziri wake biashara kuondoa msongamano wa bidhaa katika mpaka ya Kenya na Tanzania.

  Bw. Kenyatta ametoa muda wa wiki mbili mahindi yote yaliyokwama mpakani kuruhusiwa kuingia nchini.

  ''Hiyo mahindi imelala hapo mpakani,Waziri mimi nakupatia wiki mbili…yote ifunguliwe na hiyo maneno iishe'' alisema.

  Kenyata ametoa tamko hilo leo mbele ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wakati wa kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya linaloendelea jijini Nairobi.

  Mlolongo mrefu wa malori ya kubeba mizigo
  Image caption: Mlolongo mrefu wa malori ya kubeba mizigo

  Mapema mwezi Machi Kenya ilipiga marufuku ununuzi wa mahindi kutoka mataifa jirani ya Tanzania na Uganda.

  Uamuzi huo ulifikiwa baada ya uchunguzi kubaini kwamba mahindi kutoka mataifa hayo mawili sio salama kwa matumizi ya chakula cha binadamu.

 3. Video content

  Video caption: Tanzania yatoa ufafanuzi kuhusu mahindi kupigwa marufuku Kenya

  Tanzania Profea Kitila Mkumbo amesema majadiliano baina ya pande mbili yanaendelea

 4. Magufuli awataka wakulima wa taifa hilo kulisha dunia baada ya corona

  Rais Magufuli wa Tanzania.

  Rais wa Tanzania John Magufuli, amesihi wakulima nchini humo kuongeza kiwango cha uzalishaji wa chakula akibashiri uhaba wa chakula duniani baadaye mwaka huu kwasababu ya janga la virusi vya corona.

  Aliwataka wakulima kutumia vizuri fursa ya kupungua kwa uzalishaji kwa nchi ambazo huwa ni wazalishaji wakubwa wa chakula kwasababu ya masharti ya afya yaliyowekwa kote duniani.

  "Mwaka huu kuna uwezekano wa kutokea kwa baa kubwa la jaa duniani kwasababu watu wengi wanazingatia hatua za kutotoka nje kujikinga dhidi ya corona, lakini hilo halistahili kutukatisha tamaa kwasababu hata sheria hizo zikiwekwa bado watahitaji kula, tutakuza mazao na kuyauza," amezungumza na wananchi kaskazini magharibi mwa mji wa Bukoba.

  Rais wa Tanzania amekuwa akikosolewa kwa kutozingatia sana ukubwa wa madhara ya janga la corona, na kusema mara kadhaa kwamba mgogoro wa afya umekuzwa na kukejeli wanaovaa barakoa.

  Mnamo mwezi Juni alitangaza kuwa nchi hiyo "haina virusi vya corona" kwasababu ya maombi ya wananchi.

  Shirika la Afya Dunia (WHO) limeonesha wasiwasi wake juu ya mkakati wa serikali ya nchi hiyo katika kukabiliana na Covid-19.