Uvuvi na Samaki

 1. Boti iliyo na tani kadhaa za mafuta yakwama Mauritius

  Wafanyakazi wa chombo hicho wameokolewa
  Image caption: Wafanyakazi wa chombo hicho wameokolewa

  Boti ya uvuvi iliyo na bendera ya China imekwama katika miamba ya matumbawe nchini Mauritius, karibu kilomita 10 kutoka mji mkuu wa, Port Louis.

  Chombo hicho, LURONGYUANYU 588, kilikwama Pointe aux Sables maili chache kutoka ufukweni.

  Ilikuwa imebeba tani 130 za mafuta ya dizeli na tani tano za mafuta mengine lakini haikuwa na samaki, kulingana na Waziri wa Uvuvi, Sudheer Maudhoo.

  Boti hiyo ilikuwa imepangiwa kuhamisha mafuta kutoka kwa meli na kuchukua vifungu katika Port Louis.

  “kwa sasa inaelea juu ya maji na hakuna mafuta yaliyomwagika kufikia sasa,” waziri alisema.

  “Mipango ya dharura imefanywa endapo mafuta yataanza kumwagika kutoka kwa chombo hicho katika bandari ya Port Louis."

  Wafanyakazi 16 wa boti hiyo waliokolewa Jumapili jioni. Walikuwa raia 14 wa China baharia mmoja raia wa Indonesia na mwingine wa Ufilipino.

  Walinzi wa kitaifa wa pwani ya Mauritius wamesema walipokea ombi la msaada kutoka kwa boti hiyo ya uvuvi.

  Bahari yenye dhoruba ilifanya operesheni ya uokoaji kuwa ngumu hadi helikopta ya polisi ikaitwa.

 2. Mabaki ya samaki maarufu wa Zambia 'yatoweka'

  Mafishi

  Mabaki ya 'Mafishi' – samaki maarufu wa Zambia ambaye kifo chake kimeombolezwa tangu Jumatatu – yametoweka mahali iliyokuwa imehifadhiwa.

  Samaki huyo aliishi kwenye kidimbwi cha Chuo Kikuu cha Copperbelt (CBU) kwa zaidi ya mwongo mmoja na wanafunzi walimchukulia kama chanzo cha bahati.

  Aliombolezwa na viongozi wakuu serikalini akiwemo rais Edgar Lungu na baadhi ya mawaziri wake.

  Naibu Chansela wa CBU Naison Ngoma, amethibitisha kutoweka kwa mabaki ya mafishi na kuongeza kuwa uchunguzi umeanzishwa kubaini kilichotokea, kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Zambia Daily Mail.

  “Nalifahamishwa kwamba samaki huyo alianza kutoa harufu mbaya kwenye jokovu Iakini nilipoulizia yuko wapi niliambiwa ametoweka’’alinukuliwa kusema.

  Prof Ngoma anasema huenda samaki huyo ameliwa au kutupwa.

  Ameongezea kuwa hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wale waliohusika na kutoweka kwa samaki huyo.

 3. Rais wa Zambia aongoza nchi kuomboleza kifo cha samaki

  Rais Edga Lungu wa Zambia

  Zambia inaomboleza kifo cha samaki wake mkubwa katika chuo kikuu cha umma cha Copperbelt (CBU).

  Samaki huyo aliyejulikana kama Mafishi – ameombolezwa na rais Edgar Lungu na kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema.

  Neno Mafishi limekuwa likisambaa kwa kasi katika mtandao wa Twitter nchini Zambia kufuatia kifo cha samaki huyo Jumatatu usiku.

  Samaki huyo alikuwa akiishi katika kidimbwi cha chuo kikuu na baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakimtembelea kabla ya kufanya mtihani ili kuomba wapite.

  Wanafunzi wengine wanasema aliwasaidia kujiondolea msongo wa mawazo .

  Rais Lungu alitumia nukuu ya Mahatma Gandhi kumuomboleza samaki huyo kwa kuandika:"ukuu wa taifa na maendeleo ya maadili yake yanaweza kuhukumiwa kutokana na jinsi anavyowatendea wanyama wake."

  View more on facebook

  Bwana Hichilema aliandika: "Tunaungana na jamii ya wanafunzi wa sasa na wazamani wa chuo kikuu cha CBU, kufuatia kifo chasamaki wao Mafishi."

  Samaki huyo alikuwa sehemu ya mpango wa turathi ya viumbe wa majini na anasemekana ameishi ndani ya kidimbwi cha chuo hicho kwa karibu miaka saba, kwa mujibu wa kituo cha kibinafsi cha televisheni, Diamond.

  Tazama wanafunzi walivyomuomboleza samaki huyo usiku wa Jumatatu:

  View more on twitter
 4. Jinsi dagaa wanavyotumika katika uvuvi

  Miradi mbalimbali ya kitengo cha mambo kale chuo kikuu cha Dar es salaam katika kuhakikisha jamii inayoishi maeneo ya kihistoria inaweze kujikwamua kiuchumi.

  Soma Zaidi
  next