Guinea

 1. Kiongozi wa kijeshi wa Guinea kuapishwa kuwa rais

  Kiongozi wa kijeshi nchini Guinea Kanali Mamady Doumbouya

  Kiongozi wa kijeshi nchini Guinea Kanali Mamady Doumbouya anatarajiwa kuapishwa leo kama rais wa mpito.

  Sherehe ya kuapishwa kwake itafanyika katika ikulu ya rais na itahudhuriwa na wale walioalikwa pekee.

  Kanali Doumbouya aliongoza mapinduzi yaliyomuondoa madarakani Rais Alpha Condé mapema mwezi uliopita.

  Anatarajiwa kuunda serikali katika wiki chache zijazo.

  Kiongozi huyo wa kijeshi aliye na miaka 41, atakuwa kiongozi wa pili wa Afrika mwenye umri mdogo kuongonza nchi, mdogo zaidi akiwa ni wa Mali Kanali Assimi Goïta, 38 ambaye aliongoza mapinduzi ya kumng’oa madarakani Rais Keïta.

  Baada ya mapinduzi ya Guinea Kanali Doumbouya alisema askari wake wamechukua uongozi na walitaka kumaliza ufisadi, ukiukwaji wa haki za binadamu na usimamizi mbaya uliokithiri nchini humo.

  Rais Condé alichaguliwa katika uchaguzi uliokumbwa na utata kuongoza kwa muhula wa tatu licha ya maandamano ya ghasia mwaka jana.

  Mapinduzi Guinea:Mfahamu Kanali Mamady Doumbouya, kiongozi wa mapinduzi nchini Guinea

  Je mapinduzi ya kijeshi yanaongezeka Afrika?

 2. Jeshi nchini Guinea lazuia wanachama wake kushiriki uchaguzi mkuu ujao

  Wanajeshi walichukua madaraka nchini Guinea mnamo 5 Septemba
  Image caption: Wanajeshi walichukua madaraka nchini Guinea mnamo 5 Septemba

  Uongozi wa kijeshi nchini Guinea umewazuia wanachama wake kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao ambao hiyo itaashiria kurudi kwa utawala wa raia.

  Hayo yanajiri wakati jeshi lilitangaza siku ya Jumatatu hati ya mpito ambayo ilimthibitisha kiongozi wa jeshi Kanali Mamady Doumbouya kama rais kufuatia mapinduzi ya mapema mwezi huu.

  Hati hiyo pia inaangazia serikali inayoongozwa na waziri mkuu wa raia na baraza la kitaifa la mpito ambalo litatumika kama bunge kwa muda.

  Baraza hilo litakuwa na wanachama 81 kutoka kwa jamii na itajumuisha viongozi wa biashara ,vyama vya kisiasa, mashirika ya kidini, wanadiplomasia na mashirika ya kitaalamu. Pia wanazuiwa kushiriki uchaguzi wa ngazi ya mikoa na kitaifa.

  Karibu asilimia 30 ya wanachama wa baraza hilo lazima wawe wanawake, na itajumuisha rais na makamu wake wawili .

  Baraza litaamua juu ya urefu wa kipindi ambacho kitatawala kabla ya uchaguzi kufanywa ili kuanzisha serikali ya kidemokrasia.

  Mapinduzi Guinea:Mfahamu Kanali Mamady Doumbouya, kiongozi wa mapinduzi nchini Guinea

 3. Wanajeshi nchini Guinea wamzuia kwa muda waziri wa zamani

  Wanajeshi walichukua madaraka nchini Guinea mnamo 5 Septemba
  Image caption: Wanajeshi walichukua madaraka nchini Guinea mnamo 5 Septemba

  Utawala mpya wa kijeshi nchini Guineaumemkamata waziri wa zamani siku ya Jumapili na kupekua nyumba yake kabla ya kumuachia saa kadhaa baadye.

  Wanaume waliokuwa wamevalia sara walivamia nyumba ya Tibou Kamara katika mji mkuu wa Conakry wakati wa asubuhi, kumkamata na kumpeleka mahali pasipojulikana. Aliachiliwa huru mwendo wa mchana.

  Vitu kadhaa ikiwemo simu zilichukuliwakutoka kwake.

  Kukamatwa kwake kunaashiria kulithibitishwa na Kamati ya kitaifa ya maridhiano na (CNRD) Pamoja na timu yake.

  Viongozi wa mapinduzi wanamtuhumu kwa kukiuka ahadi ya kutokua na upande wowote katika usimamizi wa jeshi.

  Bw. Kamara alikuwa waziri wa viwanda na mshauri war ais wa zamani Alpha Condé, ambaye alifurushwa madarakani mapema mwezi huu.

  Maelezo zaidi:

  Mapinduzi Guinea:Mfahamu Kanali Mamady Doumbouya, kiongozi wa mapinduzi nchini Guinea

  Je mapinduzi ya kijeshi yanaongezeka Afrika?

 4. t

  Kanali Doumbouya, ambaye anasemekana alipata mafunzo ya kijeshi nchini Ufaransa, anaonekana kuwa katika uongozi wa kikosi cha jeshi kilichochukua madaraka nchini Guinea kwa jina la National Committee for Rally and Development (CNRD).

  Soma Zaidi
  next
 5. Watu 50 wauawa katika maandamano Guinea

  Vikosi vya uslama vyalaumiwa kwa kutekeleza mauaji ya kiholela Guinea
  Image caption: Vikosi vya uslama vyalaumiwa kwa kutekeleza mauaji Guinea

  Shirika la kutetea haki la Amnesty International limesema karibu watu 50 wameuawa kwa kupigwa risasi katika maandamano ya kupinga serikali nchini Guinea mwaka jana.

  Ripoti mpya ya shirika hilo limelaumu vikosi vya usalama kwa kutekeleza mauaji ya kiholela.

  Baadhi ya waandamanaji walipigwa risasi wakiandamana dhidi ya hatua ya Rais Alpha Condé kutaka kusalia madarakani kwa muhula wa tatu.

  Ripoti hiyo pia imeangazia jinsi watu 200 walivyojeruhiwa na wengine 70 kuzuiliwa kinyume cha sheria.

  Uchaguzi wa urais utafanyika nchi humo baadaye mwezi Oktoba.