India

 1. Watu 11 wauawa na radi wakijipiga picha ‘selfies’ India

  radi

  Radi imepiga na kuua takribani watu 11 na wengine kujeruhiwa huko Jaipur kaskazini mwa India siku ya Jumapili.

  Watu hao walikuwa wakijipiga picha (selfie ) kwenye mvua wakiwa juu ya jengo eneo ambalo ni maarufu katika kivutio cha utalii.

  Watu 27 walikuepo katika jengo hilona wakati kuta za ngome wakati tuko hilo likitokea – na baadhi waliripotiwa kuruka mpaka chini.

  Radi huua watu wapatao 2,000 nchini India kwa wastani kila mwaka.

  Afisa mkuu wa polisi aliviambia vyombo vya habari kuwa watu wengi waliouawa katika jengo hilo walikuwa vijana.

  Jumapili peke yake, wameshuhudia zaidi ya vifo tisa vikiripotiwa katika jimbo la Rajasthan ambako Jaipur ipo , kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani.

  Kiongozi wa jimbo hilo , Ashok Gehlot,alitangaza kutoadola 6700 sawa na 500,000 rupees kama fidia kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.

  Msimu wa mvua kubwa nchini India, hunyesha Juni mpaka Septemba.

  Mamlaka ya hali ya hewa nchini India (IMD) imesema vifo vya radi vimeongezeka mara mbili nchini humo tangu miaka ya 1960 – sababu inayotajwa ni mabadiliko ya tabia nchi.

  Takwimu zinasema matukio ya radi yanaongezeka kwa 30%-40% tangu mwanzoni na katikati ya mwaka -1990.

 2. Digital Covid certificate

  Cheti kipya cha usafiri kimeanza kutumika ndani ya mataifa ya EU kwa wale waliochanjwa, waliopimwa na kubainishwa hawana ugonjwa wa Covid-19, au wale waliopona hivi karibuni kutokana na ugonjwa huo. Lakini je itachangia ubaguzi?

  Soma Zaidi
  next
 3. Mtoto aokolewa mtoni akielea ndani ya boksi India

  Mtoto huyo mwenye umri wa siku 21 amepelekwa hospitalini
  Image caption: Mtoto huyo mwenye umri wa siku 21 amepelekwa hospitalini

  Nahodha wa boti moja katika jimbo la India lililopo eneo la kaskazini la jimbo la Uttar Pradesh amepokea pongezi chungu nzima baada ya kumuokoa mtoto wa kike aliyepatikana akielea ndani ya boksi dogo katika mto Ganges.Soma zaidi.

 4. Kiongozi wa 'familia kubwa zaidi duniani' afariki nchini India

  Ziona Chana

  Mwanamume wa miaka 76- anayeamiiwa kuwa kiongozi wa familia kubwa zaidi duniani amefariki katika jimbo la Mizoram, nchini India.

  Ziona Chana, mkuu wa dhehebu la kidini ambalo linaunga mkono ndoa ya wake wengi, alifariki Jumapili, na kuwaacha wake 38, watoto 89 na wajukuu 36.

  Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Waziri Mkuu Kiongozi wa jimbo la Mizoram, Zoramthanga,ambaye alitoa salamu zake za rambi rambi katika mtandao wa Twitter "kwa masikitiko makubwa ".

  View more on twitter

  Chana aliripotiwa kuugua ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu

  Madaktari waliiambia shirika la habari la PTI kwamba hali ya Chana ilikuwa mbaya zaidi nyumbani kwake katika kijiji cha, Baktawng Tlangnuam. Alilazwa hospitali Jumapili jioni ambako alithibitishwa kufariki alipofikishwa.

  Ni vigumu kubainisha ikiwa kweli Chana alikuwa kiongozi wa familia kubwa zaidi duniani kwa kuwa kuna wengine ambao wamedai taji hilo.

  Pia ni vigumu kukadiria ukubwa wa familia ya Chana. Ripoti moja ilidai alikuwa na wake 39, watoto 94, wajukuu 22 na kitukuu mmoja, ambao kwa jumla ni watu 181.

  Wakati ripoti kadhaa za habari nchini humo zimemtaja kuwa anashikilia "rekodi ya ulimwengu" kwa familia kubwa kama hiyo, haijulikani ni rekodi gani ya ulimwengu.

  Imeripotiwa pia kuwa familia hiyo imeangaziwa mara mbili kwenye kipindi maarufu cha Ripley's Amini au la.

 5. India yaripoti visa karibu 9,000 vya ugonjwa usiokuwa wa kawaida

  India imeshuhudia maelfu ya maabukizi ya ''Black Fungi''
  Image caption: India imeshuhudia maelfu ya maabukizi ya ''Black Fungi''

  India imeripoti zaidi ya visa 8,800 vya ugonjwa hatari wa "kuvu nyeusi" huku nchi hiyo ikikodolea macho janga la magonjwa.

  Ugonjwa huo usiokuwa wa kawaidi, unajulikana kama mucormycosis, huua hadi asilimia 50 ya wagonjwa, huku wengine wakiponea kifo baada ya kutolewa jicho moja.

  Lakini katika miezi ya hivi karibuni, India imeshuhudia maelfu ya maabukizi ya ugonjwa unayowaathiri waliougua corona na wanaopona.

  Madktari wanasema kuna uwezekano ugonjwa huo unatokana na dawa aina ya steroid inayotumiwa kutibu corona. Wanaougua maradhi ya kisukari wamo hatarini zaidi.

  Madaktari wameiambia BBC kwamba ugonjwa huo unamshambulia mtu kati ya siku 12 hadi 18 baada ya kupona corona.

  Maelezo zaidi:

  Mucormycosis 'kuvu nyeusi’ inayowalemaza wagonjwa wa Covid India

 6. Ujumbe wa India katika mkutano wa G7 London wapatikana na Corona

  India's foreign minister, right, met with the US delegation and the UK home secretary on Tuesday
  Image caption: Waziri wa mambo ya nje India,kulia alikutana ujumbe wa Marekani na Waziri wa Mambo ya ndani wa Uingereza Jumanne

  Ujumbe wa India unaohudhuria mkutano wa G7 jijini London wamepatikana na virusi ya Corona.

  Waziri wa Mambo ya nje wa India Subramanyan Jaishankar Katika mtandao wa twitter amethibitisha kwamba Wajumbe hao sasa wamejitenga na watahudhuria mkutano huo kupitia mtandao.

  Afisa wa serikali ya Uingereza alisema washiriki wawili walipimwa na kupatikana na Corona baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kila siku katika mkutano huo.

  Mkutano huo wa mataifa ya G-7 unaingia siku yake ya mwisho huku mawaziri wa Mambo ya nje wa mataifa hayo wakijadili usambazaji wa chanjo ya corona ulimwenguni.

  Shirika la Afya Duniani WHO lilikuwa limehimiza mataifa yalioendelea kusaidia nchi masikini kupata chanjo hizo.