Wanyama

 1. Kenya inashika nafasi ya nne kwa idadi ya tembo ulimwenguni

  Ni Zimbabwe, Botswana na Tanzania pekee zilizo na tembo zaidi
  Image caption: Ni Zimbabwe, Botswana na Tanzania pekee zilizo na tembo zaidi

  Kenya ni ya nne duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya tembo, kulingana na matokeo ya awali ya senya ya wanyamapori iliyofanywa hivi karibuni.

  Nchi hiyo ina jumla ya tembo 36,280 aina ya - ongezeko la zaidi ya tembo karibu 2,700 kutoka walipohesabiwa mwaka 2017.

  Ni Zimbabwe, Botswana na Tanzania zina tembo wengi zaidi.

  Kwa miaka kadhaa wanyamapori wa Kenya wamepungua kwa kiwango kikubwa kutokana na uwindaji haramu na muingiliano wa watu na wanyama hali ambayo imechangia kupotea kwa makazi ya wanyama hao na njia wanazotumia wakati wa kuhama.

  Lakini Shirika la Huduma kwa Wanyamapori nchini Kenya (KWS) linasema sensa, iliyofanywa kati ya mwezi Mei na Julai, ilionesha kupungua kwa idadi ya tembo, vifaru na spishi zingine za wanyama wanaokabiliwa na tishio la kuangamia.

  Nchi hiyo ina vifaru 1,739, miongoni mwao vifaru weupe wa kaskazini duniani, vifaru weusi 897 na vifaru 840 weupe wa kusini.

  Idadi ya vifaru weusi wanaokabiliwa na tisho la kuangamia imeongezeka kwa 200 tangu walipohesabiwa miaka minne iliyopita.

 2. Video content

  Video caption: Kenya inafanya hesabu kubwa zaidi ya wanyama kuwahi kutokea

  Nchi hiyo ya Afrika Mashariki ni nyumbani kwa spishi za wanyama wanaokabiliwa na tishio la kuangamia.

 3. Chatu ashangaza wafanyakazi kwa kujitokeza kwenye rafu za viungo

  Nyoka ajitokeza kwenye rafu
  Image caption: Nyoka ajitokeza kwenye rafu

  Duka la kuuza vyakula liligeuka kuwa hali ya mshike mshike Australia wakati mmiliki wa duka hilo alipoona chatu anayetoka kwenye rafu ya duka.

  Helaina Alati, 25, alikuwa katika duka lake huko Sydney siku ya Jumatatu wakati nyoka huyo asiye na sumu mwenye urefu wa mita 3 alipojitokeza.

  Duka hilo kubwa lipo pembezoni mwa mji wa viunga vya kaskazini magharibi.

  Lakini kuona nyoka kwenye rafu yenye viungo sicho kile Bi Alati alichokitarajia.

  Kwa bahati nzuri kwa pande zote mbili, Bi Alati ni mwokoaji wa wanyama pori na anaufahamu uzuri wa nyoka.

  "Niligeuza kichwa changu tu na tayari alikuwa karibu sentimita 20 kutoka usoni mwangu, akiniangalia tu moja kwa moja, " aliiambia BBC.

  Alifanya uamuzi mara mbili mbili lakini alibaki mtulivu.

  Hakuna mtu mwingine aliyekuwa karibu.

  Mara moja akagundua ni chatu wa almasi. Bi Alati alijua kwamba nyoka huyo hana sumu hasa baada ya kutoa ulimi wake na kuusimamisha.

  "Alikuwa akiniangalia moja kwa moja wakati wote, ni kama alikuwa akisema: "Unaweza kunipeleka nje tafadhali?", amesema.

  Baada ya kupiga picha ya nyoka, Bi Alati alitahadharisha wafanyikazi na akasema anaweza kuwasaidia kumtoa.

  Alichukua begi la nyoka kutoka nyumbani kwake, akarudi dukani, "akampiga mkia na akaanguka ndani yake."

  Kisha alimuacha katika msitu ulio mbali na nyumba hizo,

 4. Video content

  Video caption: Simba-bahari wavamia mji wa pwani ya Chile

  Je, ushawahi kufikiria utafanya nini ukikutana na mnyama mkali?