Afya

 1. Uganda yatoa agizo kwa wafanyakazi wote wa umma kupata chanjo

  chanjo

  Wakala wa serikali ya Uganda wanaosambaza chanjo ya Uviko -19 katika vituo vya afya amewaambia wafanyakazi wote na wageni kuonesha uthibitisho wa kuwa wamepata chanjo zote za corona.

  Mtu yeyote ambaye hajapata chanjo zote za corona lazima awasilishe cheti cha kuonesha kuwa hana maambukizi ya corona ,vipimo ambavyo amevifanya ndani ya saa 72 la sivyo hataruhusiwa kuingia ndani.

  Katika taarifa, maduka ya dawa yanayomilikiwa na serikali yanapaswa kuonesha mfano.

  Wale ambao wameathirika na agizo hilo ni wakurugenzi wa hospitali za umma, wauza madawa, wasambazaji wa dawa pamoja na wafadhili na wanasiasa.

  Uganda mpaka sasa imepokea dozi milioni 5.6 za chanjo za Covid-19 - na nyingine zilikuwa zimechangiwa lakini ni watu milioni 2.3 ndio wamepata chanjo na watu 580,000 ndio wamemaliza dozi kamili ya chanjo.

  Waziri wa afya Jane Ruth Aceng, siku ya Jumatano alilaumu mchakato wa utoaji chanjo kwenda taratibu.

  Taifa hilo limepanga kutoa kipaumbele kwa kutoa chanjo kwa watu milioni 4.8 la kundi la watu ambao ni pamoja na watumishi wa afya na walimu ,mpaka ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.

  Kufunguliwa tena kwa uchumi wa nchi hiyo kunategemea chanjo.

 2. Markus Mpangala

  Mchambuzi, Tanzania

  Chanjo ya Corona

  Uzinduzi wa Mpango wa Serikali ya Tanzania wa kuinua Uchumi kwa kutumia mkopo wa fedha wa shilingi Trilioni 1.3 uliotolewa na Shirika la Fedha Duniani na kukabiliana na Ugonjwa wa Virusi vya Korona umeibua mjadala mkali miongoni mwa raia nchini humo

  Soma Zaidi
  next
 3. m

  Uzee ni uhalisia na hauepukiki , huwa hatma ya kila mtu. Hali hii huwa ndio huwa inakaribia hatua ya mwisho ya maisha ya binadamu, lakini mwanasayansi wa maumbile David Sinclair anakanusha mtazamo huo.

  Soma Zaidi
  next
 4. Vijana wamezama katika maeneo ambayo hawawezi kujinasua

  Si wachache: karibu vijana 4,000 wako katika hatari ya kutumiwa kila mwaka kusafirisha dawa za kulevya katika maeneo ya vijijini nchini Uingereza, kwa mujibu wa data iliyotolewa na taasisi isiyo ya kiserikali Safer London.

  Soma Zaidi
  next
 5. Video content

  Video caption: Tuzo ya Nobel: Joto la jua au kukumbatiwa ni tiba ya maumivu

  Sasa Wanasayansi ambao waligundua jinsi miili yetu inahisi joto la jua au kukumbatiwa kwa mpendwa wameshinda Tuzo ya Nobel.

 6. iStock

  Ilikuwa mwaka jana wakati kijana Zakaria (sio jina ake halisi) mwenye umri wa miaka 29 alikuwa amelala kitandani mwake usiku majira ya saa kumi usiku. Mara alianza kuhisi maumivu ya kifua. Mwili wake mzima ulianza kutokwa jasho. Hapakuwa na mtu mwingine nyumbani wa kumpeleka hospitalini wakati ule.

  Soma Zaidi
  next