Kenya

 1. Mpenzi wake Agnes Tirop akamatwa akitoroka

  Agnes Tirop
  Image caption: Agnes Tirop

  Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mume wa mwanariadha anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio ndefu Agnes Tirop ambaye alidungwa kisu hadi kufa nyumbani kwake.

  Emmanuel Rotich , ambaye alikamatwa katika mji wa pwani ya Kenya Mombasa , atakabiliwa na mashtaka uchunguzi utakapokamilika , afisa alisema.

  Bi Tirop mwenye umri wa miaka 25 alipatikana amefariki siku ya Jumatano katika mji wa magharibi wa Iten , kituo cha mazoezi cha wanariadha.

  Alikuwa amemaliza wa nne katika mashindano ya mwaka huu ya Olimpiki mjini Tokyo katika fainali ya mbio za mita 5000.

  Mwaka 2019, alishinda medali ya shaba katika mbio za mita 10,000 katika mashindano ya ubingwa ya dunia.

  Mume wake kwasasa anazuiliwa baada ya kukamatwa alipokuwa akitoroka, kwa mujibu wa George Kinoti , mkurugenzi wa idara ya jinai , akizungumza na kitengo cha habari cha AFP.

  Salamu za rambirambi zimetolewa na raia wengi wa Kenya pamoja na wanariadha wenzake.

  View more on twitter
  View more on twitter
 2. Masten Wanjala: Mtuhumiwa wa mauaji aliyetoroka kizuizini auawa Kenya

  Bw Wanjala alikiri kutumia dawa za kulevya na kuua zaidi ya watoto 10
  Image caption: Bw Wanjala alikiri kutumia dawa za kulevya na kuua zaidi ya watoto 10

  Masten Wanjala mtuhumiwa aliyekiri kuwaua zaidi ya watoto kumi na baadaye kutoroka katika kituo cha polisi alipokua anazuiliwa ameuawa na wanakijiji wa Bungoma magharibi mwa Kenya.

  Naibu kamishena wa kaunti ya Bungoma Cornelius Nyaribai amethibitisha kifo chake katika ujumbe wa Twittter.

  Polisi wanasema Masten Wanjala alifuatwa na wanakijiji hadi nyumbani katika mji wa Bungoma na kupigwa hadi kufa.

  Mamlaka ilikuwa imeanzisha msako mkali kumtafuta mtu huyo ambaye alikiri kuwaua zaidi ya wavulana kumi katika kipindi cha miaka mitano.

  Masten Wanjala alitoweka kutoka kwa seli za polisi katika mji mkuu, Nairobi saa chache kabla ya kuitikia mashtaka ya mauaji ya wavulana 14.

  Maafisa watatu wa polisi wa Kenya waliokuwa kazini siku walifishwa mahakamani siku ya Alhamisi na kufunguliwa mashtaka ya kumsaidia mtuhumiwa huyo.

  Bwana Wanjala alikamatwa mnamo Julai na alikiri kutumia dawa za kulevya na kuwaua wavulana wadogo, na pia kunywa damu zao katika visa vingine.

 3. Morphine, Cocaine iliyofichwa katika vifungu vya nguo zanaswa JKIA,Kenya

  th

  Morphine na cocaine iliyofichwa kwenye vifungo vya kitenge vilinaswa Alhamisi katika uwanja wa ndege ya Jomo Kenyatta,JKIA nchini Kenya .

  Mkurugenzi wa DCI George Kinoti amesema kasha la dawa hizo za kulevya zilizofichwa katika vifurushi viwili zilinaswa kufuatia habari walizopokea awali.

  "Moja ya shehena ambazo zilikuwa zilipelekwa Australia kutoka Kenya zilitajwa kuwa pete za jadi za Kiafrika," alisema.

  Kinoti alisema mtu wa kawaida angechukulia jozi 168 za vipuli kuwa vipuli kama ilivyoripotiwa .

  "... lakini maafisa wa polisi waliokuwa makini waliona kuna zaidi ndani ya kifurushi hicho. Baada ya uchunguzi wa kina, waligundua podari ya manjano iliyofichwa kwa ujanja ndani ya mapambo," Kinoti alisema.

  View more on twitter

  Kinoti aliendelea kusema kuwa shehena ya pili ilikuwa imetajwa kuwa nguo 12 za vitenge na ilikuwa ikipelekwa Hong Kong.

  Wapelelezi wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya walifungua shehena na wakapata nguo 12 vifungo 199 zaidi vilivyotumiwa kuficha dawa hizo.

 4. Mahakama ya Kenya yaamuru kwamba usajili wa watu kwa njia ya kielektroniki ulikiuka sheria

  th

  Mahakama kuu nchini Kenya imetangaza kwamba mpango wa kutoa vitambulisho vipya vilivyotolewa baada ya usajili wa kielektronikikwa jina Huduma Namba ni kinyume cha sheria .

  Jaji alisema mpango huo ulikwenda kinyume na sheria ya ulinzi wa data ya 2019.

  Serikali pia ililaumiwa kwa kutotathmini jinsi ulinzi wa data ungeathiriwa kabla ya kutekelezwa kwa mpango huo.

  Wizara ya mambo ya ndani imeamrishwa kufanya tathmini hiyo kulingana na sheria.

  Mpango wa Huduma Namba ulizinduliwa ili kuleta pamoja maelezo yote kumhusu kila raia katika kadi moja ili waweze kupata huduma rahisi za serikali.

  Habari muhimu za kibinafsi , kama maelezo ya mawasiliano, alama za vidole na taaluma ya mtu, zilikusanywa mnamo 2019.

  Mamilioni ya kadi za Huduma Namba zilikuwa zimechapishwa na zingine tayari zimechukuliwa na Wakenya.

  Msemaji wa serikali Cyrus Oguna Jumatano aliwasihi wale ambao hawajazichukua kadi zao kufanya hivyo na kufafanua kwamba kadi hizo hazitatumika katika uchaguzi mkuu ujao, vyombo vya habari vya nchi hiyo viliripoti.

 5. Juisi za Apple zaondolewa sokoni katika mataifa saba ya Afrika

  apple

  Juisi ya Apple (tufaha) inayotengenezwa na kampuni ya Afrika Kusini ya Ceres imeondolewa sokoni katika mataifa saba ya Afrika kwa sababu ya kuwa na kiwango cha juu cha sumu ambayo inaweza kusababishia mtu kutapika na kupata kichefuchefu.

  Juisi hizo zina aina ya sumu inayotolewa na baadhi ya kuvu{fungi} katika tufaha na bidhaa zake.

  Uchunguzi wa maabara unaonesha kuwa juisi za Ceres zina kiwango kikubwa cha sumu zaidi ya kiwango kinachoruhusiwa kisheria 50 microgrammes kwa lita moja.

  Juisi hizi zinauzwa Kenya, DRC, Zambia, Zimbabwe, Uganda, Seychelles na Mauritius.

  Juisi hii ina soko kuu katika nchi za Mashariki na Kusini (Comesa) na wateja wametakiwa kurudisha juisi zilizonunuliwa tangu tarehe 14 na 30 Juni 2021

 6. Polisi watatu wa Kenya mashakani baada ya mshukiwa wa mauaji ya watoto 14 kutoweka kizuizini

  Bw Wanjala alikiri kutumia dawa za kulevya na kuua zaidi ya watoto 10
  Image caption: Bw Wanjala alikiri kutumia dawa za kulevya na kuua zaidi ya watoto 10

  Maafisa watatu wa polisi wa Kenya wanatarajiwa kufishwa mahakamani leo kukabiliwa na mashtaka ya kumsaidia mtuhumiwa ambaye alikiri kuua watoto zaidi ya kumi nchini humo kutoroka.

  Masten Wanjala alitoweka kutoka kwa seli za polisi katika mji mkuu, Nairobi saa chache kabla ya kuitikia shtaka la mauaji ya wavulana 14.

  Mamlaka imeanzisha msako wa mtu huyo ambaye ametajwa kuwa hatari sana.

  Bwana Wanjala alikamatwa mnamo Julai na alikiri kutumia dawa za kulevya na kuwaua wavulana wadogo, na pia kunywa damu zao katika visa vingine.

 7. Rais Kenyatta kuwa rais wa kwanza wa Afrika kukutana na rais wa Marekani Joe Biden

  KENYA

  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta atakutana na rais wa Marekani Joe Biden wakati akimaliza ziara yake ya siku mbili nchini Marekani.

  Rais Kenyatta atakuwa rais wa kwanza kutoka Afrika kukutana na rais Biden tangu kiongozi huyo aapishwe mwaka huu.

  Msemaji wa Ikulu ya Kenya amesema viongozi hao wawili watajadili mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya amani , usalama na mabadiliko ya tabia nchi.

  Jumanne, Rais Kenyatta aliwaongoza viongozi wa biashara kusaini mikataba kadhaa ya uwekezaji wa biashara ndogo na wastani pamoja na miradi ya usafirishaji na nishati safi.

  Marekani inaiona Kenya kuwa mshirika sahihi katika kupambana dhidi ya ugaidi katika eneo la Mashariki mwa Afrika.

 8. 'Kenya haitakubali kutoa hata inchi moja ya ardhi yake kwa Somalia'

  kenya

  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameonya kuwa uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa wa kuipatia Somalia eneo kubwa la bahari linalogombaniwa kutoka pwani ya nchi yao itafanya uhusiano kati ya nchi hizo mbili kudorora.

  Kenyatta alipinga uamuzi huo wa eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta na gesi akisema watageuza faida za kisiasa na kiuchumi, na kutishia usalama katika Pembe dhaifu la Afrika.

  Amesisitiza wito wake wa kuwepo kwa suluhu ya mazungumzo katika mzozo huo.

  Awali rais wa Somalia Mohammed Abdullahi Mohammed maarufu farmajo aliitaka Kenya kuheshimu sheria ya kimataifa baada ya mahakama hiyo ya Umoja wa Kimataifa kukabidhi umiliki wa eneo kubwa linalodaiwa kuwa na mafuta na gesi katika bahari hindi kwa Somali.

  Katika hotuba iliokwenda moja kwa moja katika runinga baada ya uamuzi huo, Mohamed Abdullahi Mohamed, alisema kwamba Nairobi inapaswa kuona uamuzi huo kama fursaya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

  Mnamo 2009, nchi hizo mbili zilikubaliana katika hati ya makubaliano, ikiungwa mkono na UN, kumaliza mzozo wa mipaka kupitia mazungumzo.

  ramani

  Lakini miaka mitano baadaye, Somalia ilisema mazungumzo yalishindwa na badala yake ikaenda kwa ICJ.

  Mwaka 2014, Somalia iliamua kutafuta ufumbuzi wa mzozo huo katika mahakama ya kimataifa ya (International Court of Justice) iliyoko Hague.

  Katika ombi lake, Somalia ilisema mazungumzo ya kidiplomasia yameshindikana na sasa mahakama "iamue uratibu sahihi wa kijiografia wa mpaka mmoja wa baharini katika Bahari ya Hindi".

  Lakini hayo si yote. Somalia iliitaka mahakama ya kimataifa ICJ kutangaza kuwa “Kenya… imekiuka wajibu kimataifa wa kuheshimu haki za nchi na mahakama".

  Mwaka mmoja baadae , Kenya iliweka upingamizi mahakamani juu ya kesi hiyo.