Ethiopia

 1. IMF yashindwa kutoa makadirio ya pato la ndani la Ethiopia

  M

  Shirika la Fedha Duniani(IMF) limesema kuwa haliwezi kukisia kukua kwa kiwango cha Pato ndani la Ethiopia kwa kipindi cha mwaka 2022-2026 kufuatia kile wanachosema kuwa ni "kiwango cha juu cha kutokuwa na uhakika".

  Hali inakuja kufuatia mzozo uliochukua miezi kumi na moja katika eneo la kaskazini la Tigray.

  IMF imetoa makadirio ya uchumi ya dunia kwa kukadiria kukua kwa pato la ndani kwa nchi kuwa 2% kwa mwaka 2021, ambayo iko chini kwa 6% ya mwaka 2020.

  Kwa kulinganisha, na nchi jirani ya Eritrea- ambayo pia inahusika katika mzozo huo - itaona ukuaji wa 4.8% kwa 2022-2026.

  Kenya- ambayo ina uchumi mkubwa Afrika Mashariki- kwa upande mwingine, utaongezeka kwa 6% katika kipindi hicho hicho.

  Katika muongo mmoja uliopita, Ethiopia ilikuwa miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi zaidi, kwa kuongezeka hata mara mbili ya takwimu ya kiwango kilichopita.

  Hata hivyo uchumi wake umeathirika kutokana na ukame, mvutano ya kikabila wakati huohuo wataalam pia wameonya juu ya kulipwa kwa deni lake la kigeni ambalo lilifadhili miradi mikubwa ya miundombinu.

  Nchi zingine ambazo IMF haikutoa makadirio ni Afghanistan, Libya na Syria- na nchi zote zilizokumbwa na mizozo.

  Ripoti ya IMF ilisema uchumi wa duniani unakadiriwa kukua asilimia 5.9 mnamo 2021 na asilimia 4.9 mnamo 2022, asilimia 0.1 chini kwa 2021 kuliko makadirio ya Julai.

  Mlipuko wa janga la corona pia umeathiri uchumi haswa wa nchi zinazoendelea.

 2. Jeshi la Ethiopia lafanya mashambulio Tigray, wasema waasi

  Vita vya Tigray vimesababisha uharibifu mkubwa na kuhama watu karibu milioni mbili
  Image caption: Vita vya Tigray vimesababisha uharibifu mkubwa na kuwaathiri watu karibu milioni mbili

  Jeshi la Ethiopia limefanya mashambulio ya kuratibiwa kwenye maeneo yote ya vita dhidi ya vikosi vya jimbo la kaskazini mwa eneo hilo la Tigray.

  Wamesema serikali ilitumia silaha zakufyatua makombora, vifaru, jeti na droni katuika jaribio la "kulivamia tena " jimbo.

  Chanzo cha ngazi ya juu cha waasi kimesema kuwa vikosi vya Tigray vilikuwa vimeimarisha ulinzi katika maeneo yao.

  Serikali ya Ethiopia haijathibitisha kufanya mapigano yoyote, na kuzimwa kwa mawasiliano nchini humo kunafanya uthibitishaji huru wa taarifa mapigano kutowezekana.

  Afisa wa ngazi ya juu wa wa wapiganaji wa Tigray People's Liberation Front (TPLF), Getachew Reda, amesema kuwa mashambulio ya serikali yaliyoanzishwa wiki iliyopita sasa "yamefikia kiwango cha juu".

  Alipoulizwa iwapo mapigano ya ardhini yameanzishwa, msemaji wa Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed Billene Seyoum amesema kuwa serikali ina wajibu wa kuwalinda raia wake kote nchini dhidi ya vitendo vya ugaidi lakini hatutoa maelezo zaidi.

  Mzozo wa miezi 11 umesababisha mzozo wa kibinadamu, huku Umoja wa Mataifa ukionya kuhusu watu 400,000 waliishi katika hali ya njaa katika jimbo la Tigray mwezi Julai.

  Mamia ya watu wameuawa katika mzozo, na wengine milioni mbili wamelazimika kuzikimbia nyumba zao.

  Ni vigumu kuhalalisha mashambulio

  Serikali ya Ethiopia haijathibitisha taarifa za mashambulio makali dhidi ya waasi wa Tigray, lakini uhamasishaji wa vikosi vya nchi hiyo na wanamgambo washirika wake ambao umekuwa ukifanywa kwa miezi michache iliyopita bila shaka unadhihirisha kwamba operesheni kubwa ilikuwa inaandaliwa.

  Huku uchaguzi ukiwa umemalizika na msimu wa mvua ukielekea ukingoni, Waziri Mkuu Abiy anaonekana kuangazia juu ya suluhu ya kijeshi kwa mzozo wa muda mrefu.

  Vita tayari vimesababisha athari mbaya kwa nchi: Maelfu ya watu wameuawa, mamilioni kusambaratika na maelfu wanakabiliwa na njaa.

  Lakini pande zote mbili zimetuma ishara mseto kuhusu utashi wao wa kukubali suluhu ya amani.

  Jeshi la Ethiopia lilichukua udhibiti wa maeneo mengi ya Tigray katika mwezi wa Novemba 2020, baada yavikosi vya TPLF kuchukua ngome ya jeshi.

  Katika mwezi Juni 2021, waasi waliiteka tena Tigray katika shambulio la kushitukiza, na halafu wakaingia katika baadhi ya maeneo ya majimbo jirani kama Amhara.

  Ethiopia imewatangaza waasi wa TPLF kama shirika la ugaidi, lakini TPLF wanasisitiza kuwa ni serikali halali katika Tigray.

  Itakuwa kazi ngumu hatahivyo kwa Bw Abiy kuhalalisha mashambulio mengine makubwa wakati serikali yake ikikabiliwa na shinikizo kubwa la kimataifa la kumtaka aanzishe mazungumzo na waasi.

 3. UN yashangazwa na Ethiopia kwa kuwafukuza maafisa wake wakuu

  Mamilioni ya watu wamehama makazi yao kutokana na mapigano hayo
  Image caption: Mamilioni ya watu wamehama makazi yao kutokana na mapigano hayo

  Umoja wa Mataifa (UN) imeelezea kushtushwa kwake na hatua ya Ethiopia kuwafukuza nchini humo maafisa wake wakuu.

  Hii ni baada ya Ethiopia kuwapatia maafisa saba wakuu wa Umoja huo muda wa saa 72 kuondoka nchini humo "kwa kujihusisha na masuala yake ya ndani", kupitia ujumbe wa Tweeter kutoka kwa wizara ya mambo ya nje.

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema UN inashirikiana na serikali "kwa matarajio kwamba "wafanyikazi walioathiriwa na hatua hiyo wanaweza "kuendelea na kazi yao muhimu".

  Maafisa hao ni pamoja na wakuu wa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa Unicef, Adele Khodr, na kaimu mkuu wa ofisi ya masuala ya binadamu Grant Leaity,UNOCHA.

  Umoja wa Mataifa hivi karibuni ulieelezea wasiwasi wake kufuatia ya hatua ya kuwekwa kwa vizuizi vya misaada kufika eneo la Tigray linalokumbwa na mzozo.

  Inakadiria kuwa zaidi ya watu milioni tano kaskazini wanahitaji msaada wa kibinadamu.

 4. Sudan: Wanajeshi wa Ethiopia 'walirudishwa nyuma' baada ya kujaribu kuingia al-Fashaga

  Wakuu wa jeshi la Sudan wameapa kushikilia eneo hilo linalozozaniwa (picha ya maktaba)
  Image caption: Wakuu wa jeshi la Sudan wameapa kushikilia eneo hilo linalozozaniwa (picha ya maktaba)

  Sudan inasema imezima jaribio la majeshi ya Ethiopia "kuingia" katika himaya yake.

  Mkuu wa majeshi ya Sudan, Jeneral Abdel Fattah al-Burhan, amesema hii inaonesha jinsi majeshi inavyolinda nchi hiyo kufuatia jaribio la mapinduzi lililotibuka wiki iliyopita.

  Katika taarifa yake, Sudan ilisema tukio hilo lilifanyikakatika wilaya ya Umm Barakit.

  Jeshi la Ethiopia halijajibu ombi la BBC la kutoa maoni.

  Lakini kituo cha Habari cha al- Jazeera kinanukuu serikali ya Ethiopia ikisema:"Tunakanusha harakati za vikosi vyetu kwenye mpaka wa Sudan au kuingia kwao katika eneo lolote."

  Umm Barakit liko katika eneo la mpakani la al-Fashaga linalozozaniwa, ambako hali ya taharuki imeonezeka.

  Ramani

  Kwa miongo kadhaa, raia wa Ethiopia wamekuwa wakifanya shughuli za kilimo katika ardhi hiyo yenye rotuba inayodaiwa na Sudan.

  Uhusiano kati ya Sudan na Ethiopia umezorota zaidi tangu Ethiopia ilipoanza kujaza maji katika bwawa iliyojenga katika Mto Nile na vita kuzuka katika eneo lake la Tigray.

  Katika miezi ya hivi karibuni, mapigano yameripotiwa mara kadhaa katika eneo la al-Fashaga.

  Kwanini Ethiopia, Sudani wanapambania al-Fashaga?

  Bwawa la mto Nile:Maji ya mto huu yanatishia kuleta vita kati ya Misri,Ethiopia na Sudan

 5. Waasi wa Ethiopia watuhumiwa kuharibu vituo vya afya

  Mzozo kaskazini mwa Ethiopia ulianza miezi 10 iliyopita
  Image caption: Mzozo kaskazini mwa Ethiopia ulianza miezi 10 iliyopita

  Serikali ya Ethiopia inasema waasi wameharibu maelfu ya vituo vya afya latika eneo la kaskazini mwa nchi.

  Zaidi ya watu milioni 1.9 katika majimbo ya Amhara na Afar nchini Ethiopia hawwezi kupata huduma za afya baada ya waasi watiifu kwa Tigray People’s Liberation Front (TPLF)kuripotiwa kupora vituo vya afya.

  Waasi hawajatoa tamko lolote kuhusuana na tuhuma hizo za hivi punde dhidi yao.

  Waziri wa Afya Lia Tadesse amewaambia wanahabaru siku ya Jumanne kwamba waasi waliharibu hopsitali 20 na vituo vya afya, 277 na zahanati 1,162 katika eneo la Amhara.

  Aliongeza kuwa hospitali mojaa, zahanati 10 na vituo 38 vya afya zimeharibiwa katika eneo la Afar.

  Mnamo Agosti 30, Waziri wa Elimu Getahun Mekuria alisema waasi wameharibu zaidi ya shule 7,000 kaskazini mwa Ethiopia, zikiwemo 445 katika jimbo la Afar nza zaidi ya 140 katika jimbo la Amhara.

  Mapigano kati ya waasi wa Tigray na vikosi vya muungano vya Ethiopia yalizuka katika jimbo la Tigray Novemba 2020, lakini mapigano hayo sasa yamesambaaa hadi maeneo jirani ya Amhara na Afar.

  Maelezo zaidi:

  Uchumi wa Ethiopia waathiriwa na mzozo wa Tigray

  Mgogoro wa Tigray-Ethiopia: Baa la njaa lililosababishwa na binadamu

  Ushahidi unaoonesha jinsi jeshi la Ethiopia lilivyofanya mauaji Tigray

 6. Harar street scene

  Mji wa Harar uliopo Ethiopia unaotambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO, umekuwepo kwa Zaidi ya miaka 1,000 mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza, anaeleza upekee wa urithi uliopo hapo.

  Soma Zaidi
  next
 7. Waasi wa Tigray wasema watu 150 wamekufa kutokana njaa

  mm

  Kikundi cha waasi cha eneo la Tigray, Ethiopia kimesema kuwa watu 150 wamekufa kutokana na njaa na kukosekana kwa misaada ya kibinadamu kunafanya hali kuwa mbaya zaidi.

  Serikali ya Ethiopia haijajibu lolote kuhusu madai hayo. Lakini awali ilikanusha madai ya Umoja wa Mataifa kuhusu kuweka zuio la misaada kuingia.

  Mkuu wa kilimo wa TPLF, Atinkut Mezgebo alisema watu na wanyama wanakufa kutokana na kukosa chakula na dawa na "janga linaweza kuwa kubwa zaidi ya tujuavyo".

  Aliiambia BBC Tigrinya kuwa watu wanakufa kutokana na njaa huku wanawake na watoto wakiwa ndio waathirika wakubwa zaidi wa uhaba wa chakula.

  Si rahisi kuhakiki madai haya kwa kuwa bado mawasiliano ya simu yamekatwa na intaneti haifanyi kazi Tigray.

  Lakini wakala wametoa angalizo juu ya athari za janga la kibinadamu.

  Taarifa iliyotolewa na jeshi la Tigrayan siku ya Jumatatu, imesema kuwa kuna baadhi ya vifo vinavyotokea katika kambi na watu kuhama makazi kutokana na mgogoro unaoendelea.

  Hali bado si nzuri Tigray.

  Kwa mujibu wa UN, malori 100 ya chakula yanapaswa kuingia katika eneo hilo kila siku ili kukidhi misaada ya kibinadamu.

  Lakini malori chini ya 500 yamewasili katika eneo hilo tangu Julai.

  Idadi ya watu wanaohitaji msaada wa dharura imeongezeka kwa milioni tano na watu 400,000 wanakabiliana na njaa.

 8. Wapiganaji wa Tigray watuhumiwa kuwalenga raia

  Wakazi wa Tigray

  Wapiganaji katika eneo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia, kupora vituo vya afya na vituo vingine vya kibinadamu katika eneo jirani la Amhara, shirika la habari la AP linaripoti.

  Mzozo wa miezi 10 kaskazini, ulioanza juu ya uongozi wa Tigray, sasa umeongezeka.

  Kumekuwa na ripoti kadhaa za ukatili uliodaiwa kkutekelezwa na wanajeshi wa muungano na washirika wao katika eneo laTigray na AP wanaripoti kwamba kuna madai kwamba mashambulio ya Amhara ni kulipiza kisasi.

  Shirika hilo la habari pia linasema vifaa vya matibabu katika hospitali ya mji wa Nefas Mewucha was vilivunjwa na bidhaa za tiba kuporwa.

  "Ni uwongo kwamba hawalengi raia na miundombinu," msimamizi wa hospitali Birhanu Birhanu amenukuliwa akisema.

  Wapiganaji wa Tigray wamekanusha madai kwamba raia wanalengwa.

  Katika ujumbe wa Facebook siku ya Alhamisi ubalozi wa Marekani mjini Addis Ababa ulisema kuwa"visa vitatu vya uporaji wa misaada ya kibinadamu vimethibitishwa katika mabohari ya kijamii kaskazini mwa Amhara".

  Ap pia anamnukuu mtu ambaye aliona nyumba ya watawa ya Karne ya Checheho ikishambuliwa kwa makombora.

  Soma zaidi: