Pakistan

 1. Afghanistan: Timu ya soka ya chipukizi wa kike yatorokea Pakistan

  tl

  Wachezaji wa kike kutoka timu ya vijana ya soka ya taifa ya Afghanistan wamevuka mpaka kuingia Pakistan.

  Wasichana hao walikuwa wametumia mwezi uliopita wakiwa wamejificha kwa hofu ya kukandamizwa kwa haki za wanawake na kundi la Taliban lililoingia madarakani.

  Timu ya soka ya taifa ya watu wazima iliondoka Kabul mwezi uliopita lakini timu ya vijana inasemekana waliachwa wakiwa hawajui la kufanya kwasababu ya hawakuwa na pasipoti na nyaraka zingine muhimu.

  Wachezaji 32 na familia zao walipata visa baada ya ushawishi wa chama cha serikali cha "Football for Peace".

  Maafisa walisema kundi hilo, jumla ya watu 115, watasafiri kutoka Peshawar kwenda mji wa mashariki wa Lahore, ambapo watapewa makazi katika makao makuu ya Shirikisho la Soka la Pakistani.

  Gazeti la Independent hivi karibuni liliweka wazi kwamba wachezaji hao walikuwa wamemwandikia Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan kuomba ruhusa ya kuingia nchini humo kwa haraka.

  Barua hiyo ilidai kwamba wasichana hao walikuwa katika "hatari ya tishio kubwa" kutoka kwa Taliban.

  Baada ya kuanguka utawala wa serikali ya Afghanistan, wachezaji wa Kabul walionywa na nahodha wa zamani wa timu ya taifa, Khalida Popal, kufuta picha zao zote wakicheza zilizopo kwenye mitandao ya kijamii na kuchoma vifaa vyao vyote ikiwemo sare ili kuepuka ukandamizaji unaoweza kutokea kutoka kwa serikali mpya.

  Timu ya soka ya wanawake yakimbilia Pakistan
  Image caption: Timu ya soka ya wanawake yakimbilia Pakistan

  Wiki iliyopita naibu wa tume ya kitamaduni ya Taliban, Ahmadullah Wasiq, alitonyesha shaka juu ya mustakabali wa michezo ya wanawake nchini humo wakati alisema haionekani kuwa "inafaa wala yenye ulazima," akijibu swali juu ya hatima ya timu ya wanawake ya kriketi.

  "Katika mchezo wa kriketi, wanaweza kukabiliwa na hali ambayo uso na mwili wao hautafunikwa. Uislamu hauruhusu wanawake kuonekana kwa namna hiyo", Wasiq alisema.

  "Ni enzi ya vyombo vya habari, na kutakuwa na picha na video, halafu watu watatazama. Uislamu na Imarati ya Kiislamu [Afghanistan] hairuhusu wanawake kucheza kriketi au kucheza aina ya michezo inayowaonesha wazi miili yao kwa watu."

  Wanawake walizuiwa kushiriki katika michezo wakati wa mwisho Taliban kuwa madarakani kutoka mwaka 1996-2001.

  Afghanistan: Viongozi wa Taliban wazozana Ikulu, vyanzo vimeeleza

  'Taliban wa Marekani': John Walker Lindh, mwanajihadi wa Marekani aliyekutana na Bin Laden kabla ya 9/11

 2. Wafanyakazi wakamatwa kwa kukataa kuwapa polisi burger za bure

  Wafanyikazi hawakuruhusiwa kufunga jikoni walipokuwa wakizuiliwa, mgahawa huo umesema
  Image caption: Wafanyikazi hawakuruhusiwa kufunga jikoni walipokuwa wakizuiliwa, mgahawa huo umesema

  Wafanyikazi wote 19 katika mkahawa mmoja nchini Pakistan walizuiliwa baada ya kukataa kuwapa baga (burger) za bure kundi la maafisa wa polisi wiki iliyopita.

  Wafanyikazi wa Johnny & Jugnu mjini Lahore walikamatwa Jumamosi usiku na kuzuiliwa usiku kucha.

  Maafisa tisa wa polisi waliohusika katika tukio hilo sasa wamesimamishwa kazi.

  Afisa mwandamizi wa polisi wa mkoa Inam Ghani alitangaza kusimamishwa kwao katika mtandao wa Twitter, akisema: "Hakuna mtu anayeruhusiwa kuchukua sheria mikononi mwake. Udhalimu hautavumiliwa. Wote wataadhibiwa."

  Katika taarifa iliyochapishwa kwenye Facebook, Johnny & Jugnu ilisema maafisa hao wa polisi walikuwa wamekwenda kwenye mgahawa huo siku mbili kabla ya tukio hilo na kuomba burger za bure.

 3. Watu 36 wafariki katika ajali ya treni Pakistan

  At least 30 people have died in the crash, and several more are in a critical condition
  Image caption: Watu kadhaa pia wameripotiwa kuwa katika hali mahututi

  Treni mbili za abiria zimegongana kusini mwa Pakistan, na kuua watu takriban 36 na wengine kadhaa kujeruhiwa.

  Maafisa walisema kuwa gari moshi moja lililokuwa likisafiri kwenda mkoa wa Sindh lilikuwa limepoteza mkondo na kuanguka katika njia ya reli. Treni ya pili iliyokuwa na abiria kisha iligongana nayo na kupinduka.

  Timu za uokoaji ziliwapeleka majeruhi katika hospitali za karibu na inadhaniwa kuwa watu kadhaa wako katika hali mbaya.

  Pakistan imeshuhudia msururu wa ajali mbaya za treni katika miaka iliyopita.

  Kati ya 2013 na 2019, watu 150 walikufa katika ajali kama hizo, kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini humo.

  Afisa mwandamizi katika wilaya ya Ghokti, Usman Abdullah, aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba ni vigumu kujua ni watu wangapi bado wamenaswa katika treni hizo.