Uchafuzi Baharini

 1. Video content

  Video caption: Picha za droni zafichua maisha kama ya binadamu ya nyangumi hatari zaidi

  Utafiti mpya ulioongozwa na Chuo Kikuu cha Exeter na Kituo cha Utafiti wa Nyangumi unaonyesha nyangumi wauaji wanaweza kushirikiana kati yao kulingana na umri na jinsia,

 2. Video content

  Video caption: Mbona maelfu ya wahamiaji wa Ethiopia hufanya safari hatari na ndefu kwenda Saudi Arabia?

  Baadhi ya wahamiaji hawa wanaelezea jinsi wanavyokabiliwa na wizi, utapeli na njaa katika joto la zaidi ya nyuzi joto 50.

 3. Video content

  Video caption: Kwanini Kenya inasisitiza kuhusu uhifadhi wa mazingira ya Kasa wa baharini?

  Ukijulikana kwa umaarufu wake wa michanga myeupe na hoteli za kifahari, mji wa Malindi uliopo katika pwani ya Kenya na kaskazini mwa mji wa kitalii wa Mombasa upo katikati ya juh

 4. Boti iliyo na tani kadhaa za mafuta yakwama Mauritius

  Wafanyakazi wa chombo hicho wameokolewa
  Image caption: Wafanyakazi wa chombo hicho wameokolewa

  Boti ya uvuvi iliyo na bendera ya China imekwama katika miamba ya matumbawe nchini Mauritius, karibu kilomita 10 kutoka mji mkuu wa, Port Louis.

  Chombo hicho, LURONGYUANYU 588, kilikwama Pointe aux Sables maili chache kutoka ufukweni.

  Ilikuwa imebeba tani 130 za mafuta ya dizeli na tani tano za mafuta mengine lakini haikuwa na samaki, kulingana na Waziri wa Uvuvi, Sudheer Maudhoo.

  Boti hiyo ilikuwa imepangiwa kuhamisha mafuta kutoka kwa meli na kuchukua vifungu katika Port Louis.

  “kwa sasa inaelea juu ya maji na hakuna mafuta yaliyomwagika kufikia sasa,” waziri alisema.

  “Mipango ya dharura imefanywa endapo mafuta yataanza kumwagika kutoka kwa chombo hicho katika bandari ya Port Louis."

  Wafanyakazi 16 wa boti hiyo waliokolewa Jumapili jioni. Walikuwa raia 14 wa China baharia mmoja raia wa Indonesia na mwingine wa Ufilipino.

  Walinzi wa kitaifa wa pwani ya Mauritius wamesema walipokea ombi la msaada kutoka kwa boti hiyo ya uvuvi.

  Bahari yenye dhoruba ilifanya operesheni ya uokoaji kuwa ngumu hadi helikopta ya polisi ikaitwa.

 5. Video content

  Video caption: je, unatumai kuwa bahari zitasafika?

  Utafiti mpya wa kisayansi unasema kuwa licha ya bahari kufahamika kama jaa la taka kwa miongo kadhaa,juhudi za kusafisha zimeanza kuzaa matunda kote duniani.

 6. Faith Sudi

  BBC Swahili

  Kivukio cha Likoni

  Gumzo limezuka kuhusu jitihada zinazoendelea mpaka sasa Kenya kuopoa miili ya watu wawili waliozama baharini siku tisa zilizopita. Baadhi ya wenyeji wa pwani wanadai kwamba janga kama hili linapotokea, tambiko maalum huhitaji kufanywa.

  Soma Zaidi
  next