Utamaduni

 1. Video content

  Video caption: Sudan Kusini: Mambo matano usiyoyajua kuhusu Sudan Kusini

  Ni miaka 10 tangu Sudan Kusini ilipokuwa taifa changa duniani

 2. Kukandwa kwa kutumia kisu kulianzia China zaidi ya miaka 2000 iliyopita

  Kukanda kwa namna hiyo ni nadra kuona leo nchini China na Japan, imeibuka tena nchini Taiwan katika miaka ya hivi karibuni kwani watu wameitafuta kutibu mifadhaiko ya maisha ya kisasa.

  Soma Zaidi
  next
 3. Video content

  Video caption: Maziko Kagera: Kwanini mtu akifa huzikwa karibu na nyumba yake

  Huko kaskazini magharibi mwa Tanzania mtu akifa basi huzikwa karibu na nyumba yake,

 4. Malkia wa Zulu azikwa Afrika Kusini

  Malkia alizikwa kulingana na utamaduni ya ufalme wa Swati
  Image caption: Malkia alizikwa kulingana na utamaduni ya ufalme wa Swati

  Malkia Mantfombi Dlamini Zulu wa jamii wa Zulu nchini Afrika Kusini amezikwa.

  Mazishi yake yalifanyika katika kasri lake la Kwakhangelamankengane mjini Nongoma nyakati za alfajiri. Ukumbusho wake ulifanyika usiku kucha.

  Alizikwa kulingana na utamaduni wa ufalme wa Swati. Mwili wa malkia ulifungwa kwa ngozi ya ng’ombe ambayo ulipewa ujumbe uliotumwa na kaka yake, Mfalme Mswati III wa Eswatini.

  Mazishi yalihudhuriwa na jamaa zake kutoka pande zote mbili za ufalme.

  Shughuli ya kumuaga rasmi itakayofadhiliwa na serikali itafanyikabaadaye leo.

  Baada ya Malkia Mantfombi kuzikwa, kilichosalia ni kumtafuta atakayeongoza ufalme wa Zulu.

 5. Malkia wa Zulu kuzikwa katika sherehe ya faragha

  Zulu people in traditional attire mourned the queen
  Image caption: Watu wa Zulu wakiwa wamevalia nguo za kitamaduni kumuomboleza Malkia

  Malkia wa Zulu, Mantfombi Dlamini Zulu, anatarajiwa kuzikwa katika sherehe ya faragha mkoani KwaZulu-Natal nchini Afrika Kusini.

  Alifariki ghafla mjini Johannesburg wiki iliyopita, karibu mwezi mmoja baada ya kifo cha mume wake, Mfalme Goodwill Zwelithini.

  Familia haijatangaza hadharani chanzo cha kifo chake.

  Licha ya sherehe kubwa, wasichana wa Kizulu waliofuata na mwili wa Malkia Mantfombi kurudi ikulu yake Jumatano jioni.

  Uamuzi wa atakayeongoza ufalme wa Zulu unatarajiwa kutolewa baada ya mazishi.

  Maelezo zaidi:

  Ufalme wa Zulu: Jinsi waasi wa ufalme na wanawafalme wanavyopigania uongozi

 6. Mzozo wa mrithi wa mfalme wa Wazulu waelekea mahakamani

  Hatua hiyo ya kisheria inakuja siku kadhaa baada ya kifo cha Malkia Shiyiwe Mantfombi Dlamini
  Image caption: Hatua hiyo ya kisheria inakuja siku kadhaa baada ya kifo cha Malkia Shiyiwe Mantfombi Dlamini

  Mzozo kuhusu ni nani atakayemrithi marehemu Mfalme wa Wazulu, Goodwill Zwelithini, sasa unaelekea mahakamani, vyombo vya habari vinaripoti.

  Mke wa kwanza, Malkia Sibongile Dlamini, anapinga kutekelezwa kwa wosia wa mfalme uliomtaja mfalme ajaye - huku kukiwa na madai kwamba wosia wake wa mwisho huenda ulighushiwa.

  Hatua hiyo ya kisheria inakuja siku kdhaa baada ya kifo cha Malkia Shiyiwe Mantfombi Dlamini Zulu.

  Alikuwa ameteuliwa kushikilia wadhifa huo kwa muda tarehe 24 mwezi Machi baada ya Mfalme Zwethilini kufariki kutokana na matatizo yanayohusiana na ugonjwa wa kisukari akiwa na umri wa miaka 72.

  Lakini katika kesi ya kupinga uteuzi wa Malkia Mantfombi kama mrithi wa Mfalme, Malkia Sibongile alitaka mahakama kutambua ndoa yake na na marehemu mfalme huyo kuwa halali. Pia anataka kupewa asilimia 50 ya usimamizi wa nyumba zake.

  Siku ya Jumapili, Waziri Mkuu wa Zulu Mwanamfalme Mangosuthu Buthelezi alielezea hatua hiyo ya kisheria kama "aibu", alipokuwa akizungumza na Shirikala utangazaji la Afrika Kusini SABC.

  "Baadhi ya wanafamilia wa kifalme wameshangazwa sana na kile alichofanya kwasababu bado anaomboleza. Wao, kama wajane wa Mfalme, na hatua ya kukimbilia mahakamani kwa njia waliofanya ni fedheha kwa familia ya ufalme." aliambia SABC.

  Maelezo zaidi:

 7. Mbunifu wa fulana ya Jay Z yenye nembo ya msikiti wa Lamu aomba radhi

  RIYADHA MOSQUE LAMU

  Mbunifu wa Marekani aliyetumia picha ya msikiti wa kihistoria uliopo pwani ya Kenya, Lamu katika fulana aliyoivaa nyota wa Marekani Jay-Z aomba radhi.

  Viongozi wa msikiti wa Riyadha walioghadhabishwa na kupinga kwa fulana yenye msikiti wa Lamu kuvaliwa na msanii kwa kuhofia kuvaliwa katika sehemu za starehe wameridhia maombi ya msamaha wa mbunifu huyo.

  "Tumekubali msamaha wake kwa kuwa alifanya kwa nia njema," maofisa wa msikiti wamesema.

  Mbunifu Zeddie Loky aliripotiwa kutengeneza fulana hiyo ili kuutangaza mji wa Lamu.

  View more on twitter

  BBC iliwasiliana naye na akasema;.

  Lamu imetajwa na Shirika la Umoja wa Mataifa UNESCO-kuwa eneo la urithi wa dunia na msikiti huo uliojengwa karne ya 19 ni miongoni mwa vivutio vikubwa.

  Ni msikiti ulioanza tangu mwaka 1837, ni miongoni mwa taasisi za zamani zaidi za ufundishaji za Kiislamu katika Afrika Mashariki.

  Waumini walipata ghadhabu walipoona picha ya mwanamuziki wa Marekani akiwa amevaa fulana yenye picha ya msikiti wa Lamu katika makundi ya WhatsApp , alisema katibu mkuu wa msikiti huo bwana Abubakar Badawy.

 8. Video content

  Video caption: Umuhimu wa fimbo kwa Kabila la Iraqw Tanzania

  Je wajua kuwa kabila la wa Iraqw ama Cushitic wa nchini Tanzania fimbo ni muhimu kuliko nyumba kwa wanaume.