Google

 1. Mradi wa majaribio ya mtandao wa 4G unaotumia puto kusitishwa

  Vibofu vya kampuni ya Loon vinaelea umbali wa kilomita 20 kutoka usawa wa bahari

  Kenya itasitisha mradi wa majaribio wa teknolojia ya intaneti inayowezeshwa kwa kutumia maputo yenye rubani ambayo yalikuwa yanalenga upatikanaji wa intaneti katika maeneo ya vijijini.

  Hii ni baada ya kampuni mama ya mawasiliano ya Google kufuta ushirikiano wake na kampuni ya Loon iliyokuwa inasimamia mradi huo wa kujenga maputo hayo kuwezesha upatikanaji wa intaneti.

  Huduma hiyo ya mtandao ya maputo yenye rubani ilikuwa na jukukumu la kutoa huduma ya mtandao wa 4G ili watu waweze kuwa na huduma ya mawasiliano kwa njia ya sauti na video, kuingia kwenye tovuti, barua pepe, ujumbe mfupi na kuwezesha utumiaji wa video kwa njia ya moja kwa moja.

  Lakini mpango huo ulishindwa kufaulu kwasababu haukuweza hata kupata pesa za chini kabisa kuugharamia ili kuuwezesha, kulingana na tamko lililowekwa kwenye blogu moja.

  Kampuni ya Loon ilikuwa imesaini makubaliano makubwa nakampuni ya mawasiliano ya Kenya ya Telcom kuwezesha upatikanaji wa mtandao wa 4G katika maeneo ya vijijini nchini humo.

  Telkom imesema mradi huo ambao ulikuwa unafanyiwa majaribio utamalizika Machi 1 kufuatia tangazo la kwamba utendakazi wa kampuni ya Loon unasitishwa.

  "Miezi kadhaa ijayo, timu ya kampuni ya Loon itashirikianakwa karibu na kampuni ya Telkom kuhakikisha huduma hiyo iliyokuwa kwenye majaribio inakamilika vizuri,"taarifa imesema hivyo.

 2. Covid-19 yaongoza orodha ya taarifa zilizotafutwa zaidi kwenye Google 2020

  Google

  Katika mwaka ambao umegubikwa na athari za janga la corona, sio jambo la kushangaza kwamba ugonjwa huo ulitafutwa sana katika mtandao wa Google nchini Kenya, Afrika Kusini na Nigeria, kwa mujibu wa uchunguzi wa kampuni hiyo, kutokana na jinsi maswali yalivyoulizwa kuhusu ugonjwa huo.

  Afrika Kusini ambayo iliathiriwa zaidi na janga la corona barani Afrika, watu walitafuta taarifa kuhusu amri ya kutotoka nje na habari kuhusu sigara na pombe ambazo zilipigwa marufuku kuuzwa.

  Nchini Kenya, baadhi ya mambo yaliyotafutwa katika mtandao kuhusu janga la corona ni pamoja na: jinsi ya kutengeneza vyeyuzina namna ya kuimarisha kinga ya mwili.

  Taarifa za kupotosha kuhusu mtandao wa 5G kusambaza virusi vya corona zilikuwa miongoni mwa masuala yaliitafutwa na watu nchini Afrika Kusini .

  Pia watu walipendelea taarifa kuhusu uchaguzi wa Marekani na katika nchi hizo tatu zaidi wakitaka kupata maelezo zaidi kumhusu rais Joe Biden na makamu wa rais mtarajiwa Kamala Harris.

  Wanigeria, sawa na watumiaji wengine wa mtandao wa Google nchini Kenya na Afrika Kusini, walitafuta taarifa kuhusu watu mashuhuri nchini humo.

  Taarifa kuhusu Ligi ya Primia zilikuwa maarufu sana nchini Kenya.

  Nchini Nigeria, wembo wa Fem, ulioimbwa na nyota wa miondoko ya kiafrika Davido ulitafutwa zaidi.

 3. Video content

  Video caption: Atamba kwa mtindo wake wa kipekee wa fasheni

  Kutokana Covid- 19, nembo mbalimbali za fasheni zilisitisha maonyesho yao. Lakini si mbunifu wa mitindo Anifa Mvuemba ambaye amebuni njia ya maonyesho ya ya fasheni ya kipekee...

 4. Video content

  Video caption: Cesaria Evora: Muimbaji kutoka Cape Verde aliyepata sifa kimataifa kwa kipaji chake

  Alipata umaarufu kwa kuwa muimbaji anayetembea miguu chuma, na ni shujaa ndani na nje ya Cape Verde kwa nyimbo zake zinazoihusu nchi yake.