Ndondi

 1. Video content

  Video caption: Wafahamu wanandondi 3 kutoka Afrika wanaovuma Ulaya licha ya kupitia changamoto

  Mcameroon Francis Ngannou ambaye alinusurika kama mhamiaji, alipovuka bahari ya Mediterranian kwa mtumbwi na kuishi katika mitaa ya jiji la Paris hadi kuwa namba mbili katika mapam

 2. Bondia afariki baada ya kupigwa KO katika shindano la ndondi

  b

  Maswali yanaulizwa kuhusu taratibu za usalama katika ndondi ya Zimbabwe kufuatia kifo cha Taurai Zimunya baada ya kupigwa katika pambano mjini Harare.

  Zimunya, 24, wa uzito wa Super bantam, alifariki siku ya Jumatatu, baada ya kuzimia wakati wa pambano lisilo la ubingwa siku ya Jumamosi.

  Ni mara ya kwanza kwa bondia kufariki nchini Zimbabwe kutokana na majeraha aliyoyapata ulingoni.

  Lawrence Zimbudzana, katibu mkuu wa Bodi ya Kitaifa ya Kudhibiti Ndondi na Mieleka ya Zimbabwe (ZNBWCB), anasema kuwa mipango ya uchunguzi bado haijashughulikiwa.

  "Kwa sasa tutaangazia mazishi, na kisha tuketi na kuangalia masuala," Zimbudzana aliambia BBC Sport Africa katika mazishi ya Zimunya Jumatano.

  Taarifa iliyotolewa na ZNBWCB ilisema kuwa "taratibu zote muhimu za matibabu zilifuatwa na msaada wa dharura wa matibabu ulitolewa mahali hapo kabla ya kupelekwa hospitali".

  Zimunya alipigwa makonde kadhaa kichwani kabla ya kubanduliwa nje katika raundi ya tatu ya pambano la raundi sita.

  Aliyekuwa mkufunzi wake Tatenda Gada alihuzunika, akihisi nyota huyo alikuwa na uwezo mkubwa.

  "Tumeopokonywa mojawapo ya matarajio yetu mazuri," Gada alisema. "Nilifanya kazi na Taurai kwa zaidi ya miaka minne - nilimtazama akistawi na alikuwa mmoja wa nyota wajao katika fani hii."

  Baba yake Zimunya, Samson, alikuwa bondia mahiri asiye wa kulipwa na alitarajia mtoto wake angebeba jina la ukoo na kuwa bingwa.

  Ndondi ilikuwa imerejea tu Zimbabwe baada ya vizuizi vya kupambana na janga la corona kulegezwa.

 3. Habari za hivi pundeBondia Manny Pacquiao astaafu katika ndondi

  Manny Pacquiao ni bondia pekee kuwahi kushinda mataji ya uzani tofauti duniani

  Bondia wa Ufilipino Manny Pacquiao ametangaza kustaafu mchezo huo ili kuangazia kazi yake ya siasa.

  Bondia huyo anayeshikilia mataji ya uzani tofauti ni seneta nchini humo na tayari ametangaza nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2022.

  Katika pigano lake la mwisho bondia huyu mwenye umri wa miaka 42-alishindwa na bondia wa Cuba Yordenis Ugas mjini Las Vegas mwezi uliopita.

  "Nilisikia kengele ya mwisho tu. Mchezo ulikua umeisha," alisema Pacquiao.

  Katika video iliyowekwa katika mitandao ya kijamii, Pacquiao alielezea kustaafu kwake kama "uamuzi mgumu" katika Maisha yake, akiongeza kuwa ndondi ilimpatia "nafasi ya kupigana na umaskini" na "ujasiri wa kubadilisha maisha zaidi".

  Pia aliwashukuru mashabiki wake, marafiki na wale wote waliomuunga mkono katika mchezo huo,hususan Mkufunzi wake wa muda mrefu Freddie Roach, ambaye alimtaja kama "familia yangu, kaka na rafiki".

  "Sitasahau kile nilichofanya na kufanikisha maishani mwangu," alisema.

  Pacquiao anatambulika kama bondia bora wa kulipwa duniani, akishinda mataji 12 katika mikanda minane tofauti na ni bondia wa pekee kushikilia ubingwa wa dunia kwa miongo minne.

  Soma:

  Manny Pacquiao: Kutoka Ulingo wa masumbwi mpaka siasa: Je atauweza ulingo wa Ikulu?

  Manny Pacquiao: Nyota wa ndondi anayewania urais Ufilipino

  Rodrigo Duterte: Rais wa Ufilipino aliyekiri kuua watu kwa mikono yake

 4. Félix Verdejo: Bondia ashtakiwa kwa kumuua mpenzi wake mjamzito

  Bw. Verdejo (kulia) alipigana katika Olimpiki ya mwaka 2012
  Image caption: Bw. Verdejo (kulia) alipigana katika Olimpiki ya mwaka 2012

  Bondia wa Puerto Rico aliyepigana katika michezo ya Olimpiki ya London mwaka 2012 ameshtakiwa kwa kumteka na kumuua mpenzi wake aliyekuwa mjamzito.

  Félix Verdejo anatuhumiwa kwa kumshambulia na kumuua Keishla Rodríguez kisha kuutupa mwili wake chini ya daraja karibu na San Juan,mji mkuu wa eneo hilo la kisiwani lilipo chini ya himaya ya Marekani.

  Alijisalimisha kwa polisi siku ya Jumapili baada ya kukataa kushirikiana na wachunguzi, polisi imesema.

  Kifo hicho kiibua maandamano kupinga mauji dhidi ya wanawake huko Puerto Rico.

  Mwezi Januari, kisiwa hicho kilitangaza hali ya hatari kufuatia dhulma dhidi ya wanawake. Puerto Rico huripoti angala kisa kimoja cha mauji ya mwanamke kila wiki, kwa mujibu wa kundi la kutetea haki nchini, huku visa vingine 60 vy auhalifu wa aina hiyo vikiripotiwa mwaka jana.

  Bondia huyo mwenye umri wa miaka 27- anakabiliwa na mashtaka ya utekaji, wizi wa gari ulisababisha kifo na kuua kwa kukusudia mtoto ambaye hajazaliwa.

 5. Video content

  Video caption: Monalisa Sibanda ni mwanandondi wa kulipwa wa kwanza mwanamke nchini Zimbabwe.

  Monalisa Sibanda ni mwanandondi wa kulipwa wa kwanza mwanamke nchini Zimbabweambaye akitafuta kulipiza kisasi kutokana na kifo cha mama yake, lakini sasa ameamua kusamehe