Riadha

 1. Mary Keitany: Mkenya anayeshikilia rekodi ya dunia ya Marathon astaafu

  Mary Keitany set a world record for a women-only race at the 2017 London Marathon

  Mwanariadha wa Kenya wa mbio za marathon upande wa wanawake Mary Keitany ametangaza kustaafu akiwa na miaka 39 baada ya kuumia mgongo.

  Bado anashikilia rekodi ya dunia ya marathon ya wanawake pekee aliyokimbia kwa muda wa saa mbili na dakika 17 na sekunde moja, amabyo aliweka katika ushindi wake wa tatu wa London Marathon 2017.

  Pia alishinda New York Marathon mara nne.

  "Sasa ni wakati wa kusema kwaheri - ikiwa tu kama mkimbiaji wa mtaalamu- kwenye mchezo ninaupenda sana, "alisema.

  "Baada ya ufanisi wangu wa mwaka 2019, wakati nilipoandikisha matokeo mazuri ikiwa ni pamoja na kuwa nafasi ya pili mjini New York, Nilikuwa na matumaini kuwa bado ninaweza kuwa na mshindani mkubwa kimataifa kwa miaka kadhaa zaidi ingawa nina miaka zaidi 30, "Keitany aliongeza katika taarifa yake.

  "Walakini, nina huzuni kusema, jeraha la mgongo ambalo nilipata mwishoni mwa 2019 lilichangia uamuzi kuhusu kustaafu kwangu.

  "Sikuweza kupata matibabu niliyotaka Ulaya kwa sababu ya vizuizi vya usafiri vinavyohusiana na janga la corona mwaka jana na kila wakati nilifpoikiri nimepata nafuu na kuanza mazoezi kwa bidii, nakabiliwa na shida hiyo tena.

  Mafanikio ya kwanza ya Keitany ulimwenguni yalikuja mnamo 2007 wakati aliposhinda nishani ya fedha ya kibinafsi na tuzo ya dhahabu ya tumi kwenye Mashindano ya Nusu ya Marathon ya Dunia.

  Kwa nini Mkenya Mary Keitany aliwatumia wanaume kufanya mazoezi ya mbion za London Marathon

 2. By Celestine Karoney

  BBC Sport Africa, Nairobi

  Kenya's Ferdinand Omurwa Omanyala breaking the African 100m record

  Mwanariadha wa Kenya Ferdinand Omanyala, anayeshikilia rekodi ya mbio za mita 100, anasisistiza kuwa hana wasiwasi juu ya maswali yaliyoibulika kutokana na marufuku ya madawa ya kusisimua misuli aliyowekewa mwaka 2017.

  Soma Zaidi
  next
 3. Mwanariadha wa Namibia Beatrice Masilingi akiwa katika mashindano ya olimpiki mjini Tokyo

  Beatrice mwenye umri wa miaka 18 anasema kwamba anafurahia kushiriki katika mbio za mita 200 upande wa akina dada katika mashindano ya Olimpiki ya 2020 yanayofanyika mjini Tokyo ambapo mbio za kufuzu kwa fainali zitaanza siku ya Jumatatu.

  Soma Zaidi
  next
 4. Kenya yawazuia wanariadha wake kushiriki Kimanjaro Marathon

  Wanariadha wa Kenya wamekuwa wakitawala mbio hizo katika makala yaliopita.
  Image caption: Wanariadha wa Kenya wamekuwa wakitawala mbio hizo katika makala yaliopita.

  Kenya imekataa kuwaidhinisha wanariadha wake kushiriki mbio za masafa marefu za Kilimanjaro Marathon nchini Tanzania kwa kuhofia janga la corona.

  Mashindano hayo yanayotambuliwa na Shirikisho la Riadha Duniani IAAF- yataandaliwa Jumapili hii chini ya mlima Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika.

  Wanariadha wa Kenya wamekuwa wakitawala mbio hizo katika makala yaliopita.

  Katika taarifa, Shirikisho la Riadha la Kenya limetoa wito kwa "wanariadha wote kutosafiri Tanzania kushiriki mashindano hayo".

  Tanzania haijakuwa ikitoa data ya hali ya corona nchini humo tangu kati kati ya mwaka jana.

  Mapema wiki hii Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitoa wito kwa Tanzania kuanza kutoa data ya watu walioambukizwa virusi vya corona.

  Maelezo zaidi: