Brazil

 1. Uwanja maarufu wa Maracana Brazil kupewa jina la Pele

  Uwanja wa Maracana

  Uwanja maarufu wa Maracana nchini Brazil unatarajiwa kubadilishwa jina kwa heshima ya mchezaji nguli wa soka, Pele.

  Hii ni baada ya wabunge wa Jimbo la Rio de Janeiro, kupiga kura ya uwanja huo kubadilishwa jina kuwa Uwanja wa Edson Arantes do Nascimento - Rei Pele.

  Edson Arantes do Nascimento ni jina halisi la mchezaji huyo aliye na umri wa miaka 80, na jina Rei linamaanisha mfalme kwa Kireno.

  Gavana wa Jimbo la Rio de Janeiro lazima aidhinishe hatua hiyo kabla ya jina la uwanja huo kubadilishwa rasmi.

  Pele, ambaye aliongoza Brazil kushinda Kombe la Dunia mara tatu, alifunga bao lake la 1,000 katika uwanja huo mwaka 1969 wakati wa mchuano kati ya timu yake ya Santos na Vasco da Gama.

  Uwanja wa Maracana uliandaa fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1950 na 2014, na hali kadhalika sherehe ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki mwaka 2016.

  Zaidi ya mashabiki 200,000 waliripotiwa kufiks katika uwanja huo kutazama fainali ya mwaka 1950, ambapo Uruguay ilishinda Brazil, japo uwanja huo sasa una uweza kuwahimili watu 78,838.

  Uwanja huo ulipewa jina Mario Filho, mwandishi wa hambari aliyeshinikiza ujenzi wake miaka ya 1940, lakini unajulikana kama Maracana jina la eneo ulipojengwa.

 2. A pregnant young woman with her hands over her belly

  Hatua ya kumtoa mimba mtoto wa miaka 10 wiki hii, imezua mjadala mkali nchini Brazil, ambapo suala la uavyaji mimba linakumbwa na mgawanyiko mkubwa. Lakini Melania Amorim, daktari ambaye amekuwa akiwasaidia waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia kwa miaka 30, ameiambia BBC kuwa visa kama hivyo vinaendelea kuongezeka na kuelezea kwanini kutoa mimba ndio nji asalama kwa wasichana hao kuliko kujifungua

  Soma Zaidi
  next
 3. Fernanda making positive signals from a hospital bed

  Fernanda Martinez aliye na umri wa miaka 22- anakabiliwa na hali inayofahamika kwa kimombo kama Ehlers-Danlos syndromes (EDS), ambayo husababisha, kuzaana kwa seli zisizokuwa za kawaida mwilini- ambazo huathiri mfumo wa utumbo.

  Soma Zaidi
  next
 4. Ilustração de uma mulher com bebê no colo

  Baadhi ya wanawake wamekuwa wakiua watoto wao baada ya kutumia njia mbadala ili kumtoa mtoto tumboni kabla ya siku za kuzaliwa kuwadia na kujaribu kuficha ukweli. Fahamu hali ilivyo nchini Brazil na kile wanawake hao wanachopitia.

  Soma Zaidi
  next