Australia

 1. Korea Kaskazini:Aukus inaweza kuchochea 'nchi kukimbilia kujihami na zana za kinyuklia

  Kim Jong-un
  Image caption: Picha ya Kim Jong-un kutoka maktaba

  "Korea Kaskazini imekosoa mkataba mpya wa usalama kati ya Marekani, Uingereza na Australia, ikisema unaweza kusababisha "nchi kukimbilia kujihami na zana za kinyuklia."

  Afisa wa wizara ya mambo ya nje alisema makubaliano ya Aukus "yatasumbua usawa wa kimkakati katika eneo la Asia-Pasifik."

  Mkataba huo utajumuisha Marekani na Uingereza zikiipa Australia teknolojia ya kujenga nyambizi zinazotumia nyuklia.

  Inatazamwa sana kama juhudi ya kukabiliana na ushawishi wa China katika Bahari ya China Kusini inayozozaniwa.

  Mkataba wa Aukus ulitangazwa wiki iliyopita na pia utajumuisha makombora ya meli, akili ya bandia na teknolojia zingine.

  "Hivi ni vitendo visivyofaa na vya hatari ambavyo vitasumbua usawa wa kimkakati katika eneo la Asia-Pasifiki na kusababisha kila nchi kukimbilia kuwa na silaha za nyuklia," amesema afisa wa wizara ya mambo ya nje ya DPRK akirejelea makubaliano ya usalama.

  Wiki iliyopita, Korea Kaskazini ilifanya majaribio mawili makubwa ya silaha - lile la kombora la masafa marefu na kombora la balistiki.

  China pia imekosoa makubaliano hayo na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Beijing Zhao Lijian amesema muungano huo unahatarisha "kuharibu kabisa amani ya eneo ... na kuimarisha juhudi za kujihami kwa silaha za nyuklia.

  Pyongyang ilisema ni "kawaida kabisa kwa nchi jirani [kama] China kulaani vitendo hivi kama kutowajibika kwa kuharibu amani na utulivu wa eneo hilo."

  Matarajio ya mkataba huo ni kuona Marekani ikishirikisha wengine teknolojia yake ya nyambizi kwa mara ya kwanza katika miaka 60, hapo awali ikiwa ilishirikisha Uingereza mara moja tu.

  Ni nchi gani zilizo na nyambizi?

  Nchi zilizo na nyambizi
  Image caption: Nchi zilizo na nyambizi

  Inamaanisha Australia itaweza kujenga nyambizi zenye nguvu za nyuklia ambazo ni haraka mno na ngumu kuzigundua kuliko meli za kawaida.

  Zinaweza kukaa ndani ya maji kwa miezi kadhaa na kudungua makombora ya umbali mrefu - ingawa Australia inasema haina nia ya kuweka silaha za nyuklia ndani yake.

  China haikutajwa moja kwa moja wakati wa tangazo la mpangilio wa usalama.

  Hata hivyo, viongozi wa nchi hizo tatu walitaja mara kwa mara masuala ya usalama wa kikanda ambayo "yameongezeka sana".

  Korea Kaskazini pia ilirejelea taarifa ya hapo awali iliyotolewa na Ufaransa, ambayo ilitaja makubaliano hayo kuwa "usaliti," na kusema kwamba mkataba huo umesababisha "mgogoro mkubwa" kati ya washirika.

  Ufaransa imekuwa ikikosoa mkataba wa Aukus kwasababu ilifikisha ukomo wa makubaliano yenye thamani ya $ 37bn (£ 27bn) yaliyosainiwa na Australia mnamo mwaka 2016 kwa Ufaransa kujenga nyambizi 12 za kawaida.

  Ufaransa inasema iliarifiwa juu ya makubaliano hayo saa chache kabla ya tangazo rasmi kwa umma kutolewa.

 2. Chatu ashangaza wafanyakazi kwa kujitokeza kwenye rafu za viungo

  Nyoka ajitokeza kwenye rafu
  Image caption: Nyoka ajitokeza kwenye rafu

  Duka la kuuza vyakula liligeuka kuwa hali ya mshike mshike Australia wakati mmiliki wa duka hilo alipoona chatu anayetoka kwenye rafu ya duka.

  Helaina Alati, 25, alikuwa katika duka lake huko Sydney siku ya Jumatatu wakati nyoka huyo asiye na sumu mwenye urefu wa mita 3 alipojitokeza.

  Duka hilo kubwa lipo pembezoni mwa mji wa viunga vya kaskazini magharibi.

  Lakini kuona nyoka kwenye rafu yenye viungo sicho kile Bi Alati alichokitarajia.

  Kwa bahati nzuri kwa pande zote mbili, Bi Alati ni mwokoaji wa wanyama pori na anaufahamu uzuri wa nyoka.

  "Niligeuza kichwa changu tu na tayari alikuwa karibu sentimita 20 kutoka usoni mwangu, akiniangalia tu moja kwa moja, " aliiambia BBC.

  Alifanya uamuzi mara mbili mbili lakini alibaki mtulivu.

  Hakuna mtu mwingine aliyekuwa karibu.

  Mara moja akagundua ni chatu wa almasi. Bi Alati alijua kwamba nyoka huyo hana sumu hasa baada ya kutoa ulimi wake na kuusimamisha.

  "Alikuwa akiniangalia moja kwa moja wakati wote, ni kama alikuwa akisema: "Unaweza kunipeleka nje tafadhali?", amesema.

  Baada ya kupiga picha ya nyoka, Bi Alati alitahadharisha wafanyikazi na akasema anaweza kuwasaidia kumtoa.

  Alichukua begi la nyoka kutoka nyumbani kwake, akarudi dukani, "akampiga mkia na akaanguka ndani yake."

  Kisha alimuacha katika msitu ulio mbali na nyumba hizo,

 3. Video content

  Video caption: Bibi wa miaka 106 hataki kuitwa mzee,na anajua kudensi!

  Baada ya miongo kadhaa ya kuishi nje ya nchi, Bi Kramer alirudi nyumbani Sydney akiwa na miaka 99.

 4. Tazama: Bibi wa miaka 106 ambaye hataki kuitwa mzee

  Video content

  Video caption: Bibi wa miaka 106 hataki kuitwa mzee,na anajua kudensi!

  Bi. Eileen Kramer mwenye umri wa miaka 106, anaonekana kuendelea na kazi zaidi licha ya umri aliokuwa nao. Baada ya miongo kadhaa ya kuishi nje ya nchi, Bi Kramer alirudi nyumbani Sydney akiwa na miaka 99. Tangu wakati huo, alishirikiana na wasanii kutengeneza video kadhaa kuonesha kipaji chake na mapenzi yake ya kucheza muziki.

 5. Video content

  Video caption: Wimbi la Panya kwenye mashamba lilivyosababisha hasara kwa wakulima

  Wimbi la Panya kwenye mashamba lilivyosababisha hasara kwa wakulima