Japan

 1. Olimpiki Tokyo: Mwanariadha Mjerumani mwenye asili ya Tanzania ashinda dhahabu

  Mwanariadha Mihambo

  Raia wa Ujerumani mwenye asili ya Tanzania Malaika Mihambo, amelishindia taifa lake medali ya dhahabu katika mashindano ya michezo ya Olimpiki ya long Jump.

  Mwanaridha huyo aliruka urefu wa mita saba ili kuchukua ushindi.

  Awali Mihambo alikabiliwa na changamoto kadhaa kabla ya mashindano hayo lakini hatimaye alifanikiwa kuonesha umahiri wake.

  Katika fainali ya mchezo huo iliofanyika hii leo Jumanne, bi Malaika hakuonesha ishara zozote za kuibuka mshindi.

  Urefu wa mita saba alioruka katika jaribio la sita ulimwezesha kuipatia Ujerumani nishani yake ya kwanza ya dhahabu katika mchezo huo tangu Heike Drechsler aliposhinda mwaka 2000.

  Nishani ya fedha ilimwendea mshindi mara nne wa mashindano ya dunia na Olimpiki yaliofanyika mjini London Brittney Reese wa Marekani baada ya kuruka mita 6.97 huku Ese Brume wa Nigeria akijinyakulia medali ya shaba na kuiongezea Afrika idadi ya medali katika michezo hiyo.

 2. Kikosi cha Algeria kinachoshiriki mashindano ya Olimpiki

  Mchezaji wa Judo kutoka Algeria fethi Nourine amepigwa marufuku na atarudishwa kwao kutoka katika michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 baada ya kujiondoa katika mashindano hayo kuzuia kukutana na mpinzani wake kutoka Israel.

  Soma Zaidi
  next
 3. Mwanariadha wa Uganda afurushwa Japan

  Olimpiki

  Mnyanyuaji uzani wa Uganda aliyetoweka katika kambi ya Olimpiki magharibi mwa Japan Ijumaa iliyopita amerejea nyumbani saa chache kabla ya kuanza rasmi kwa michezo ya Olimpiki.

  Julius Ssekitoleko alirejeshwa nyumbani leo asubuhi na kuchukuliwa na polisi muda mfupi baada ya kutua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Entebbe.

  Mama yake mzazi, mke wake mjamzito na maafisa wengine wa serikali waliokuwa wamesafiri kumlaki hawakufanikiwa kumuona.

  Katika taarifa, Wazara ya Mambo ya Nje ilisema, "Serikali ya Uganda imejitolea kuendelea kumhudumia mwanariadha huyo ili kumsaidia atulie na kuendeleza kazi yake lakini pia kumsaidia kuelewa jinsi vitendo kama hivi vibaya havimuathiri yeye tu kama mwanariadha lakini pia wanariadha wengine katika sekta ya Michezo na taifa kwa ujumla. "

  Wakati alipotoweka katika chumba chake cha hoteli huko Izumisako mjini Osaka, Julius alikuwa hajatimiza viwango vya Olimpiki vilivyowekwa kimataifa alipofika Japan.

  Alitakiwa kurejea nyumbani Uganda katikati ya wiki hii.

  Aliacha kijikaratasi chenye ujumbe pamoja na mizigo yake akisema anataka kubaki Japan na kufanya kazi.

  Polisi wa Japan walimpata Julius katika mji wa Yokkaichi, maili 105 kutoka kambi wa wachezaji wa Olimpiki.

 4. Kwa jamaa walioachwa nyuma na wapendwa wao - hofu ya kuwatafuta jouhatsu wao - inaweza kuwaathiri vibaya.

  Kila mwaka baadhi ya watu huamua 'kutoweka' na kuanza upya maisha, ajira, nyumba na familia. Nchini Japan, kuna makapuni ambazo zinawasaidia wale wanotaka kutoweka na kupotea kabisa.

  Soma Zaidi
  next