Uislamu

 1. Msemaji wa Taliban mwenye mazungumzo ya kutisha aliyeamua kuonesha uso wake

  Msemaji wa Taliban
  Image caption: Msemaji wa Taliban

  Kwa miaka mingi amefanya kazi nyuma ya pazia, sauti tu kupitia simu ndio ilikuwa inasikika.

  Lakini siku ya Jumanne, hilo lilibadilika wakati msemaji wa Taliban Zabihullah Majahid alipojitokeza kwenye mkutano wa kwanza na waandishi wa habari wa Taliban.

  "Yalda Hakim wa BBC anasema "alishtuka", kuona sura ya mwanamume ambaye alikuwa akiongea naye kwa zaidi ya muongo mmoja, akijibu swali la kwanza kutoka kwa mwandishi wa habari wa kike.

  Hakim anaongeza kuwa hilo lililikuwa tofauti na ujumbe mwingine aliokuwa akipokea kutoka kwake.

  "Baadhi ya ujumbe ulikuwa ni wenye msimamo mkali Kiisilamu. Wale ambao munafikiri: Mtu huyu ni mwenye kiu ya damu kwa Wamarekani, yeye ni mwenye kiu ya damu kwa mtu yeyote katika serikali ya Afghanistan. "

  "Halafu leo ​​amekaa hapo na kusema hakutakuwa na kisasi," Hakim anasema.

  "Kwa miaka mingi ametuma ujumbe wa umwagaji damu na sasa ghafla, anataka amani? Ni vugumu sana kuunganisha hilo".

 2. Mzozo waibuka Burundi juu ya 'Adhana'- wito wa Sala

  Waziri aliwaomba mashekhe kupunguza sauti ya Adhana wakati wa alfajiri
  Image caption: Waziri aliwaomba mashekhe kupunguza sauti ya Adhana wakati wa alfajiri

  Viongozi wa Kiislamu nchi Muslim Burundi wamejitenga na kauli iliyotolewa na mmoja wao kumkosoa waziri wa mambo ya ndani aliyetoa wito kwa mashekhe kupunguza sauti ya adhana ya asubuhi ili isiwe kero kwa umma.

  Katika kikao cha pamoja na viongozi wa kidini, Waziri wa Mambo ya ndani wa Burundi Gervais Ndirakobuca aliwaomba viongozi kidini wasipige kelele wakati wa maombi ya usiku na kwa wenzao wa Kiislamu kupunguza sauti ya Adhana (wito wa sala) wakati wa alfajiri.

  Jumanne asubuhi Ndikumana Rashid, alisikika akimkaripia waziri na kumtaka afutilie mbali matamshi aliyotoa na kuomba msamaha.

  Bw. Rashid alisema kauli ya waziri ni shambulio la moja kwa moja dhidi ya dini ya Kiislamu.

  Wawakilishi wa Waislamu hata hivyo wamesema Bw. Rashid atawajibikia kauli yake kwa kumtukana waziri.

  Mkuu wa Baraza la Waislamu nchini Burundi Zuberi Mohamed, amesema hakuna mzozo kati ya Waislamu na serikali akiongeza kuwa wito wa sala jimbo la kawaida.

 3. Video content

  Video caption: Mbona kuna mgongano kuhusu sikukuu ya Eid?

  Kufuatia hali ya sintofahamu ya kutofautiana kuanza na kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani nimetaka kufahamu kutoka kwa Mussa Yusuphu Kundecha.