Morocco

 1. Kesi ya ubakaji wa Khadija Morocco: Watu wafungwa miaka 20

  Msichana huyo alisema watekaji wake walimchora tattoo kwa nguvu na kumteketeza kwa sigara
  Image caption: Msichana huyo alisema watekaji wake walimchora tattoo kwa nguvu na kumteketeza kwa sigara

  Mahakama nchini Morocco imewahukumu kifungo cha miaka 20 jela wanaume 11 waliopatikana na hatia ya kumbaka na kumteka msichana wa miaka 17 mwaka 2018,kulingana na wakili wa mashtaka.

  Msichana huyo - anayeitwa Khadija - alikuwa ameonesha hadharani majeraha ya kuchomwa na michoro ya tattoo ambayo anasema wahusika walimtendea.

  Katika mahojiano ya mwaka 2018 alisema "hatawahi kuwasamehe" washambuliaji wake.

  Kesi hiyo ilisababisha hasira ya kitaifa na kusababisha kampeni ya #JusticePourKhadija.Khadija's lawyer told the AFP news agency that he would appeal.

  Ibrahim Hachane alisema kuwa hukumu zilizotolewa huko Beni Mallal "hazikuwa ngumu" kwa sababu washukiwa wanaopatikana na hatia ya ulanguzi wa watu wanaweza kufikia jela miaka 30.

  Bwana Hachane aliambia AFP washambuliaji hao pia waliamriwa kulipa faini ya dola 16,000 sawa na (Pauni 12,000).

  Wanaharakati wa kutetea haki wanaonya kuwa mashambulio dhidi ya wanawake yameongezeka nchini Morocco, huku utafiti ukionesha kuwa zaidi ya nusu ya wanawake wamekabiliwa na unyanyasaji.

  Mwaka 2018 serikali ilipitisha sheria inayoharamisha unyanyasaji dhidi ya wanawake ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku ndoa za lazima, unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya umma, na adhabu kali kwa aina fulani za vurugu.

  Lakini ilikosolewa na shirikal la Human Rights Watch kwa kutofanya uhalifu ubakaji katika ndoa na kukosa ufafanuzi sahihi wa vurugu za nyumbani.

  Khadija alisimulia jinsi alivyoteseka mikonono mwa washambuliaji wake, akiongeza kuwa walichomtende "kilimuathiri"vibaya.

  "Nilijaribu kutoroka mara kadhaa, lakini walinishika na kunipiga," aliiambia runinga ya Chouf TVnchini Morocco katika mahojiano yam waka 2018.

  "Walinitesa, hawakunipatia chakula wala maji, na hawakuniruhusu kuoga."

  Ijapokuwa Wamorocco wengi walistajabishwa na kitendo hicho, jamaa za washukiwa walimtuhumu Khadija kwa udanganyifu wakidai alikuwa akiishi ‘maisha mabaya’’

  Sheria mpya kuwasaidia wanawake Morocco dhidi ya udhalilishaji na unyanyasaji wa kingono

  Ubakaji wa ndoa: 'Mume wangu alikuwa malaika-kisha akanibaka'

  Fahamu mataifa ambayo wabakaji wanaweza kuepuka mkono wa sheria kwa kufunga ndoa na waathiriwa

 2. Morocco yahalalisha bangi ya dawa

  Bangi

  Bunge nchini Morocco limeidhinisha sheria inayohalalisha ukuzaji wa bangi kwa ajili ya matumizi ya tiba na viwandani.

  Lengo ni kuingia katika soko la kimataifa linalokua la kimataifa, kukuza kilimo na kutoa ajirahasa katika maeneo ya vijijini ambayo hayana maendeleo.

  Morocco ni moja nchi zinazokuza bangi kwa kiwango kikubwa kwa matumizi haramu. Hii itasalia kuwa haramu chini ya sheria mpya.

  Madhara ya Bangi

  • Unaweza kusababisha kuchanganyikiwa na wasiwasi usio wa kawaida
  • Ikivutwa na tumbaku, inaweza kuongeza hatari ya ugonjwa kama vile saratani ya mapafu
  • Matumizi ya mara kwa mara yamehusishwa na hatari ya kupatwa na magonjwa ya kiakili
  • Upungufu wa kudumu wa kiwango cha mtu kufikiria na kufahamu mambo, baada ya kutumia kwa muda mrefu

  Maelezo zaidi:

 3. Mwanamke ajifungua watoto tisa Mali

  Watoto

  Mwanamke mmoja nchini Mali amejifungua watoto tisa katika hali ambayo sio ya kawaida.

  Halima Cisse, 25, alijifungua watoto wa kike watano na wavulana wanne katika hospitali ya Morocco siku ya Jumanne ambako alikuwa amelazwa, Waziri wa Mali Fanta Siby alisema katika taarifa. Alijifungua kupitia njia ya upasuaji.

  Bi Cisse amekuwa akitarajia kijifungua watoto saba kulingana na uchunguzi wa skani ya tumbo aliyofanyiwa nchini Mali na Morocco lakini skani hiyo haikugundua amebeba watoto wengine wawili.

  Siku ya Jumanne, Dkt Siby alisema watoto hao na mama yao “wanaendelea vyema”. Wanatarajiwa kurejea nyumbani wiki chache zijazo.

  Aliwapongeza madaktari waliomhudumia Mali na Morocco, “ambao ujuzi wao ni chanzo cha matokeo mema ya ujauzito huu".

  Mimba ya Bi Cisse imeshangaza taifa hilo la Afrika Magharibi na imewavutia baadhi ya wakuu wa nchi hiyo – huku baadhi yao wakisafiri had Morocco alipohitaji utunzi wa kitaalamu, shirika la habari la Reuters liliripoti.

  Msemaji wa wizara ya afya ya Morocco, Rachid Koudhari, ameliambia shirika la habari ya AFP kwamba hakujua uzazi wa aina hiyo hutokea nchini humo.

 4. Bilionea wa Afrika aliyeteuliwa kuwa rais wa Caf ni nani?

  Patrice Motsepe

  Ijumaa, Patrice Motsepe atakuwa rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) wakati ambapo raia huyo wa Afrika Kusini atakuwa bila mpinzani kwenye uchaguzi utakaofanyika Morocco.

  Soma zaidi

 5. Tawala hasimu za Libya zakutana Morocco kwa mazungumzo

  Nasser Bourita
  Image caption: Waziri wa mambo ya nje wa Morocco, Nasser Bourita, akiongoza mkutano huo

  Wajumbe wa tawala mbili hasimu nchini Libya wamekutana kwa mazungumzo nchini Morocco wiki mbili baada ya pande hiz mbili kusitisha mapigano.

  Wajumbe watano kutoka kila upande ikiwa ni pamoja na ule wa serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa iliyo na makao yake Tripoli na bunge hasimu lililo na makao yake katika mji wa mashariki wa Tobruk.

  Akifungua rasmi mkutano huo katika mji wa Bouznika Waziri wa mambo ya nje wa Morocco Nasser Bourita, amesema Morocco haina ajenda yoyote bali inataka uwapatia nafasi viongozi wa Libya kadili masuala yanayowagawanya.

  Morocco ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka2015 ambao ulichangia kubuniwa kwa serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa mjini Tripoli.

 6. El Moutawakel alipita mstari wa kumaliza mbio haraka mbele ya wenzake kiasi kwamba alidhani alikua amekosea kuanza mbio

  Kama wewe ni mwanamke wa Morocco na ndio umetimiza umri wa miaka 36, huenda ulikua karibu kupewa jina Nawal. Hii ni kwasababu ushindi wa Nawal El Moutawakel tarehe 8 Agosti 1984 katika michezo ya Olyimpiki mjini Los Angeles ulikuwa na maana kubwa sana kwa Mfalme wa Morocco Hassan II kiasi kwamba alitangaza kuwa watoto wote wa kike waliozaliwa siku hiyo waitwe jina lake. Hii ni hadithi yake...

  Soma Zaidi
  next