Maslahi ya Wanyama

 1. Video content

  Video caption: Fahamu jinsi ndege kwa jina tai walivyo katika hatari ya kuangamia Afrika

  Kati ya tai 11 wanaopatikana barani Afrika , saba wapo katika hatari ya kuangamia . Nchini Kenya spishi moja – ya tai wenye ndevu – imesalia na tai watano kulingana na wahifadhi w

 2. Mbwa wa Joe Biden wafukuzwa White House

  German shepherds Major (top) and Champ were the first pets to live in the White House in four years

  Mbwa wanaomilikiwa na Rais wa Marekani Joe Biden na mke wake Jill Biden wameondolewa Ikulu ya White House baada ya mmoja wao, kwa jina Major, kuripotiwa kumuuma ajenti wa usalama.

  Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Marekani, mbwa hao aina ya 'German shepherd' wamepelekwa nyumbani kwa Biden huko Wilmington, Delaware.

  Hii ni kutokana na ukali wa Major dhidi ya wafanyakazi wa White House.

  Bw. Biden na familia yake walimuasili Major mwaka 2018. Alikuwa mbwa wa kwanza kutoka makao ya wanyama kuishi katika Ikulu ya Marekani.

  Mbwa wao, Champ, ana miaka 13.

 3. Biashara ya nguruwe yapigwa marufuku Shinyanga,Tanzania

  Homa ya nguruwe yabainika Tanzania
  Image caption: Homa ya nguruwe yabainika,Shinyanga, Tanzania

  Mkuu wa Wilaya ya kahama Annamringi Macha amepiga marufuku biashara ya nyama ya nguruwe na usafirishaji wa nguruwe wenyewe baada ya wanyama hao kubainika kwa homa ya nguruwe, Gazeti la serikali ya Tanzania, Habari leo limeandika.

  Akizungumza na waandishi wa habari, mkuu huyo wa wilaya alisema amechukua uamuzi huo ili kukinga wananchi na watumiaji wa nyama hiyo dhidi ya ugonjwa huo.

  ‘’Maeneo yanayofanya biashara ya nyama ya nguruwe, vichinjio, wapishi na sehemu za starehe haziruhusiwi kufanya biashara hiyo kwa sasa mpaka itakapotangazwa tena,’’ Macha alisema.

  Bwana Macha alisema dalili za mlipuko wa ugonjwa huo zilianza Desemba mwaka jana na sasa ni kama unasambaa.

  Bwana Macha pia alipiga marufuku usafirishaji wa wanyama hao kutoka sehemu moja hadi nyingine bila kibali cha daktari na atakayekiuka agizo hilo atachukuliwa hatua za kisheria.

  Daktari wa Mifugo Halmashauri ya Mji wa Kahama, Dkt. Damian Kilyenyi amethibitisha kuwa zaidi ya nguruwe 500 wamekufa kwasababu ya ugonjwa huo.

  Homa ya nguruwe ni nini?

  • Ni ugonjwa wa kupumua unaosababishwa na virusi ya influenza aina A, vinavyofahamika kama H1N1
  • Chanzo chake ni kwenye nguruwe, lakini sasa huambukiza binadamu na huenezwa kwa kupiga chafya au kukohoa.
  • Dalili za ugonjwa huo zinakaribiana na za homa ya msimu - homa kali, kukohoa, maumivu kooni, maumivu mwilini na mzizimo.
  • Wanaoathirika zaidi huwa wajawazito, watoto wa chini ya miaka mitano, wazee wa zaidi ya miaka 65 na wale wenye matatizo mengine ya kiafya.
  • Virusi hiyo vilitambuliwa mara ya kwanza nchini mexico mwaka 2009 na vikaenea upesi maeneo mengine duniani.
 4. Video content

  Video caption: Tazama jinsi mjusi huyu alivyonusurika kifo kutoka kwa nyoka wenye njaa

  Mjusi mkubwa anayeishi baharini nusra awe chakula cha nyoka walio na njaa kisiwani Galapagos huko Fernandina.

 5. Video content

  Video caption: Tazama vita vya sokwe vilivyodumu miaka 4 Tanzania

  Tafiti mbalimbali zilizofanywa juu ya Wanyama aina ya Sokwe, matokeo yake mengi ikiwemo tabia za nyani hufananishwa na binadamu. Kama ilivyo kwa binadamu Sokwe pia huwa na migogo