G7

 1. Viongozi wa G7 waahidi chanjo bilioni moja za corona kwa mataifa masikini

  Borris Johnson

  Viongozi wa mataifa saba yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi na kiviwanda duniani wameahidi kutoa dozi bilioni moja za chanjo ya Covid- 19 kwa mataifa maskini kama "hatua kubwa kuelekea upatikanaji wa chanjo kwa watu wote duniani", amesema Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson.

  Wakati wa kumalizika kwa kongamano la G7 mjini Cornwall, Bw. Johnson alisema mataifa yanapinga "mbinu za kitaifa".

  Lakini akaongeza kuwa chanjo ya ulimwengu itaonyesha faida za maadili ya kidemokrasia ya G7.

  Pia kulitolewa ahadi ya kuwaondolea mchango wa kushughulikia mabdailiko ya tabia nchi

  Baada ya mkutano wa kwanza wa viongozi wa ulimwengu ndani ya miaka miwili , Bw. Johnsona alisema "Ulimwengu ulikuwa unatutegemea sisi kukataa baadhi ya njia za ubinafsi, za kitaifa ambazo ziliharibu mwitikio wa kwanza wa ulimwengu kwa janga hiyo na kutumia juhudi zote za kidiplomasia, kiuchumi na kisayansi kutokomeza Covid -19".

  Alisema viongozi wa G7 waliahidi kusambaza chanjo hizo kwa nchi masikini moja kwa moja au kupitia mpango wa Shirika la Afya Ulimwenguni la Covax - zikiwemo dozi milioni 100 kutoka Uingereza.

  Maelezo zaidi:

  G7 yaitaka China, kuchunguzwa dhidi ya uasili wa Corona

 2. Ujumbe wa India katika mkutano wa G7 London wapatikana na Corona

  India's foreign minister, right, met with the US delegation and the UK home secretary on Tuesday
  Image caption: Waziri wa mambo ya nje India,kulia alikutana ujumbe wa Marekani na Waziri wa Mambo ya ndani wa Uingereza Jumanne

  Ujumbe wa India unaohudhuria mkutano wa G7 jijini London wamepatikana na virusi ya Corona.

  Waziri wa Mambo ya nje wa India Subramanyan Jaishankar Katika mtandao wa twitter amethibitisha kwamba Wajumbe hao sasa wamejitenga na watahudhuria mkutano huo kupitia mtandao.

  Afisa wa serikali ya Uingereza alisema washiriki wawili walipimwa na kupatikana na Corona baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kila siku katika mkutano huo.

  Mkutano huo wa mataifa ya G-7 unaingia siku yake ya mwisho huku mawaziri wa Mambo ya nje wa mataifa hayo wakijadili usambazaji wa chanjo ya corona ulimwenguni.

  Shirika la Afya Duniani WHO lilikuwa limehimiza mataifa yalioendelea kusaidia nchi masikini kupata chanjo hizo.