China

 1. China: Sera ya watoto watatu yapitishwa rasmi kuwa sheria

  China
  Image caption: China yageuza rasmi sheria ya kupata watoto

  China imefanya marekebisho rasmi kwa sheria zake ili kuwaruhusu wanandoa kuwa na watoto hadi watatu, ili kuongeza kiwango cha kuzaliana.

  Kanuni hiyo ilikuwa moja kati ya kadhaa zilizopitishwa Ijumaa kwenye mkutano wa wabunge wa bunge la kitaifa National People Congress (NPC).

  Maelezo juu ya sheria yenye utata ya kupambana na vikwazo dhidi ya Hong Kong, ambayo wafanyabiashara wengi walihofia ingewaweka katika wakati mgumu, pia ilitarajiwa.

  Lakini vyombo vya habari vya Hong Kong viliripoti Ijumaa kuwa uamuzi huo umecheleweshwa.

  China ilitangaza mnamo mwezi Mei kuwa itawaruhusu wanandoa kuwa na watoto hadi watatu, katika mabadiliko makubwa ya sera.

  Uamuzi huo sasa umepitishwa rasmi kuwa sheria, pamoja na maazimio kadhaa ambayo yalilenga kuongeza kiwango cha kuzaliana na "kupunguza mzigo" wa kulea mtoto, limesema shirika la habari la Xinhua.

  Hii ni pamoja na kufuta "ada ya uendelezaji jamii" - adhabu ya kifedha kwa wanandoa hulipwa kwa kuwa na watoto zaidi ya idadi iliyoidhinishwa, kuhimiza serikali za mitaa kutoa likizo ya wazazi, kuongeza haki za ajira za wanawake na kuboresha miundombinu ya utunzaji wa watoto.

  Takwimu za hivi karibuni za sensa zilionesha kupungua kwa kasi ya kiwango cha kuzaliana.

  Soma zaidi:

  Jinsi sera mpya ya watoto 3 inavyozidi kuwaumiza Wachina

  China yakomesha sera ya watu kuwa na watoto wawili pekee

 2. ad

  Kama mataifa mengi, Amerika haina uhusiano wowote wa kidiplomasia na Taiwan lakini inahitajika na sheria ya 1979 kukipatia kisiwa hicho kinachojitawala njia ya kujilinda na ndio mshirika wake muhimu zaidi wa kimataifa.

  Soma Zaidi
  next
 3. Wuhan kupima watu wote Corona

  vipimo vya corona China

  Mamlaka katika jiji la Wuhan nchini China, zitaanza kuwapima watu wote baada ya maambukizi kuongezeka katika eneo hilo.

  Wuhan imerekodi visa saba, ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja

  Jiji hilo lenye wakazi milioni 11 walikua katika wakati hatarishi zaidi baada ya virusi vya corona kubainika kwa mara ya kwanza mwaka 2019.

  China kwa sasa inashuhudia visa vingi vya maambukizi ya corona katika kipindi cha miezi kadhaa kukibainika visa 300 katika kipindi cha siku 10.

  Majimbo 15 chini humo yamekumbwa na virusi hivyo na kufanya serikali kuendesha zoezi la kupima watu chi mzima na kuweka masharti ya kutotoka nje.

  Mamlaka nchini humo zimehusisha kuenea kwa maaambukizi ya virusi vya vya Delta na msimu unaoendelea wa utalii wa ndani.