Burundi

 1. Rais wa Burundi ashutumiwa kwa kumkosoa mwandishi wa habari

  Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye,
  Image caption: Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye,

  Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, ameshutumiwa kwa kumshambulia kwa maneno mwandishi wa habari aliyeangazia hali ya ugonjwa wa corona nchini humo.

  Rais alikuwa amesema Esdras Ndikumana, ambaye ni mwanahabari wa kituo cha Ufaransa RFI, alikuwa akichafua taswira ya Burundi kutokana na habari yake.

  Hata hivyo, Waandishi Wasio na Mipaka (RSF) walisema kuwa "matamshi hayo yana uzito mkubwa na hatari" ni "ukumbusho wa kusikitisha wa uhuru wa vyombo vya habari jinsi ulivyo dhaifu nchini Burundi."

  Shirika la habari la RFI lilielezea "tuhuma za rais kama "zisizo na msingi na za kipuuzi."

  Mkuu wa RSF Afrika Arnaud Froger alimsihi rais " kutotengeneza uadui pasipo na haja" na kuongeza kwamba anachostahili kufanya ni "kupambana na janga hilo badala ya kukabiliana na waandishi wa habari".

  Siku za nyuma, kumekuwa na wasiwasi juu ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Burundi.

 2. Dinah Gahamanyi

  BBC Swahili

  Haiba ya utulivu ya Bi Margret Kenyatta imempatia mvuto miongoni mwa Wakenya wa tabaka mbali mbali

  Kwa muonekano, ni mwanamke mpole, mtaratibu na bila shaka kwa wanaomtazama wanaweza kuafiki kuwa anastahili kuitwa jina analoitwa hasa wakati wa sherehe za kitaifa-Mama wa taifa. Lakini je Margaret Gakuo Kenyatta, ni nani hasa? Na amekuwa na mchango gani katika taifa la Kenya na nje?

  Soma Zaidi
  next
 3. Mzozo waibuka Burundi juu ya 'Adhana'- wito wa Sala

  Waziri aliwaomba mashekhe kupunguza sauti ya Adhana wakati wa alfajiri
  Image caption: Waziri aliwaomba mashekhe kupunguza sauti ya Adhana wakati wa alfajiri

  Viongozi wa Kiislamu nchi Muslim Burundi wamejitenga na kauli iliyotolewa na mmoja wao kumkosoa waziri wa mambo ya ndani aliyetoa wito kwa mashekhe kupunguza sauti ya adhana ya asubuhi ili isiwe kero kwa umma.

  Katika kikao cha pamoja na viongozi wa kidini, Waziri wa Mambo ya ndani wa Burundi Gervais Ndirakobuca aliwaomba viongozi kidini wasipige kelele wakati wa maombi ya usiku na kwa wenzao wa Kiislamu kupunguza sauti ya Adhana (wito wa sala) wakati wa alfajiri.

  Jumanne asubuhi Ndikumana Rashid, alisikika akimkaripia waziri na kumtaka afutilie mbali matamshi aliyotoa na kuomba msamaha.

  Bw. Rashid alisema kauli ya waziri ni shambulio la moja kwa moja dhidi ya dini ya Kiislamu.

  Wawakilishi wa Waislamu hata hivyo wamesema Bw. Rashid atawajibikia kauli yake kwa kumtukana waziri.

  Mkuu wa Baraza la Waislamu nchini Burundi Zuberi Mohamed, amesema hakuna mzozo kati ya Waislamu na serikali akiongeza kuwa wito wa sala jimbo la kawaida.