Uingereza

 1. Ndege yamwagia mtu majitaka akiwa kwenye bustani yake

  Ndege ilidondosha maji taka ya kibinadamu kote kwa mtu wakati alikuwa katika bustani

  Mwanamume mmoja na mfanyakazi wake walimwagiliwa maji taka kutoka kwa ndege, jopo la uchunguzi lafahamishwa nchini Uingereza.

  Akizungumza katika baraza la Royal Borough ya Windsor na shurika la ndege la Maidenhead, kansela Karen Davies alisema "amegutushwa" kusikia kisa hicho.

  Alielezea jinsi "yeye’’ na bustani lote "lilivyofunikwa" kwa uchafu huo.

  Kisa hicho kilitokea mjini Windsor kati kati ya -Julai.

  Vyoo vya ndege huhifadhi maji taka katika sehemu maalum, lakini yaliyomo kawaida hutupwa mara tu ndege inapotua.

  Diwani wa Clewer Mashariki aliambia kikao hicho kuwa alifahamishwa kuhusu kisa hicho cha "kuogofya" na mkazi wa eneo bunge lake, kulingana na Huduma ya Kuripoti Demokrasia ya Mitaa.

  Diwani wa parokia ya Whitfield, Geoff Paxton, ambaye amefanya kazi katika viwanja vya ndege kwa miaka 40, alitaja tukio hilo kuwa "nadra sana" na ambalo halijawahi kutokea kwa muda mrefu.

  BBC imewasiliana na Mamlaka ya Usafiri wa Angani ili kupata tamko lake.

 2. Kenya na Uingereza 'zinafanyia kazi' mpango wa usafiri wa Covid

  The WHO has been opposing vaccine passports for international travel

  Serikali za Kenya na Uingereza zinasema kuwa zinafanyia kazi mfumo wa kutambua vyeti vya chanjo ya Covid vinavyotolewa katika nchi zote mbili , ili kuwezesha usafiri kati yao.

  Haya yanajiri baada ya Uingereza kubadili mfumo wao tata wa usafiri wa kimataifa ili kuwarahisishia wasafiri kuingia nchini humo.

  Licha ya kuondolewa katika orodha nyekundu ya Uingereza, Wakenya wanaonuia kusafiri huko bado watahitajika kufanyiwa vipimo vya corona siku tatu kabla ya safari, kukaaa karantini kwa siku 10 wanapowasili pamoja na kulipia gharama ya vipimo na kutengwa.

  Chini ya sheria mpya za Uingereza kuanzia tarehe 4 Oktoba, watu waliopewa chanjo kamili kutoka nchi ambazo hazimo kwenye orodha nyekundu watasamehewa kukaaa karantini ya lazima.

  Lakini taarifa ya pamoja ya siku ya Jumanne iliyotolewa na Balozi wa Uingereza nchini Kenya na Wizara ya Afya ya Kenya inaonesha jinsi suala hilo bado linakabiliwa na utata na huenda lisitatuliwe hivi karibuni.

  Cheti hicho kilianza kutumika rasmi Julai mosi kwa awamu ya kipindi cha wiki sita

  "Kuanzisha mfumo wa kutambua vyeti vya chanjo ya kila mmoja kwa mpango wa pasipoti ya chanjo kwa kusafiri huchukua muda haswa katika janga lisilokuwa la kawaida," taarifa hiyo inasema.

  Wataalam wa afya nchini Kenya wanasema tangazo la hivi karibuni kutoka Uingereza litakuwa na athari katika utumiaji wa chanjo za Covid-19 nchini.

  Watu kutoka nchi zingine za Kiafrika ambao wamebaki katika orodha nyekundu ya Uingereza wamekosoa sheria hizo mpya za usafiri wakisema ni za kibaguzi.

  Shirika la Afya Ulimwenguni limekuwa likipinga pasipoti za chanjo kwa safari ya kimataifa kwa sababu ya kupatikana kwa usawa wa chanjo za Covid-19 ulimwenguni.

  Chanjo ya pasipoti: Cheti cha kidijitali cha Covid Muungano wa Ulaya na jinsi kitakavyowaathiri wasafiri

 3. Korea Kaskazini:Aukus inaweza kuchochea 'nchi kukimbilia kujihami na zana za kinyuklia

  Kim Jong-un
  Image caption: Picha ya Kim Jong-un kutoka maktaba

  "Korea Kaskazini imekosoa mkataba mpya wa usalama kati ya Marekani, Uingereza na Australia, ikisema unaweza kusababisha "nchi kukimbilia kujihami na zana za kinyuklia."

  Afisa wa wizara ya mambo ya nje alisema makubaliano ya Aukus "yatasumbua usawa wa kimkakati katika eneo la Asia-Pasifik."

  Mkataba huo utajumuisha Marekani na Uingereza zikiipa Australia teknolojia ya kujenga nyambizi zinazotumia nyuklia.

  Inatazamwa sana kama juhudi ya kukabiliana na ushawishi wa China katika Bahari ya China Kusini inayozozaniwa.

  Mkataba wa Aukus ulitangazwa wiki iliyopita na pia utajumuisha makombora ya meli, akili ya bandia na teknolojia zingine.

  "Hivi ni vitendo visivyofaa na vya hatari ambavyo vitasumbua usawa wa kimkakati katika eneo la Asia-Pasifiki na kusababisha kila nchi kukimbilia kuwa na silaha za nyuklia," amesema afisa wa wizara ya mambo ya nje ya DPRK akirejelea makubaliano ya usalama.

  Wiki iliyopita, Korea Kaskazini ilifanya majaribio mawili makubwa ya silaha - lile la kombora la masafa marefu na kombora la balistiki.

  China pia imekosoa makubaliano hayo na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Beijing Zhao Lijian amesema muungano huo unahatarisha "kuharibu kabisa amani ya eneo ... na kuimarisha juhudi za kujihami kwa silaha za nyuklia.

  Pyongyang ilisema ni "kawaida kabisa kwa nchi jirani [kama] China kulaani vitendo hivi kama kutowajibika kwa kuharibu amani na utulivu wa eneo hilo."

  Matarajio ya mkataba huo ni kuona Marekani ikishirikisha wengine teknolojia yake ya nyambizi kwa mara ya kwanza katika miaka 60, hapo awali ikiwa ilishirikisha Uingereza mara moja tu.

  Ni nchi gani zilizo na nyambizi?

  Nchi zilizo na nyambizi
  Image caption: Nchi zilizo na nyambizi

  Inamaanisha Australia itaweza kujenga nyambizi zenye nguvu za nyuklia ambazo ni haraka mno na ngumu kuzigundua kuliko meli za kawaida.

  Zinaweza kukaa ndani ya maji kwa miezi kadhaa na kudungua makombora ya umbali mrefu - ingawa Australia inasema haina nia ya kuweka silaha za nyuklia ndani yake.

  China haikutajwa moja kwa moja wakati wa tangazo la mpangilio wa usalama.

  Hata hivyo, viongozi wa nchi hizo tatu walitaja mara kwa mara masuala ya usalama wa kikanda ambayo "yameongezeka sana".

  Korea Kaskazini pia ilirejelea taarifa ya hapo awali iliyotolewa na Ufaransa, ambayo ilitaja makubaliano hayo kuwa "usaliti," na kusema kwamba mkataba huo umesababisha "mgogoro mkubwa" kati ya washirika.

  Ufaransa imekuwa ikikosoa mkataba wa Aukus kwasababu ilifikisha ukomo wa makubaliano yenye thamani ya $ 37bn (£ 27bn) yaliyosainiwa na Australia mnamo mwaka 2016 kwa Ufaransa kujenga nyambizi 12 za kawaida.

  Ufaransa inasema iliarifiwa juu ya makubaliano hayo saa chache kabla ya tangazo rasmi kwa umma kutolewa.