Twitter

 1. Rais wa Nigeria aamuru kuondolewa kwa marufuku ya Twitter

  Twitter

  Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameamuru kuondolewa kwa marufuku dhidi ya mtandao wa kijamii wa Twitter,ikiwa kampuni hiyo ya kubwa ya teknolojia itafikia masharti flani.

  Rais Buhari alisema Wanigeria wanaweza kuendelea kutumia mtandao huo kwa ajili ya "biashara na masuala mengine muhimu".

  Katika hotuba yake ya kuadhimisha siku kuu ya uhuru wa nchi hiyo,r ais alisema kwamba kamati maalum ya ofisi yake inajadiliana naT witte rkuhusu masuala kadhaa ya usalama wa kitaifa, ushuru wa haki na utatuzi wa mizozo.

  Serikali ya Nigeria ilipiga marufuku huduma zaTwitter tangu mwezi Juni baada ya mtandao huo wa kijamii kufuta ujumbe tata wa Rais Buhari.

  Marufuku hiyo ilikosolowe vikali na mashirika ya kutetea haki za binadamu na wanaharakati wa kutetea uhuru wa vyombo vya habari.

  Twitter Nigeria: Kampuni za simu zaagizwa kufungia mtandao wa Twitter

 2. Mkuu wa Twitter aweka bendera ya Nigeria mtandaoni- Kunani

  Mkuu wa Twitter

  Mkuu wa Twitter Jack Dorsey ameweka ujumbe wenye picha ya bendera ya Nigeria mtandaoni katika hatua ambayo vyombo vya habari nchini humo vinaashiria ni kuunga mkono maandamano ya Jumamosi dhidi ya uongozi mbaya na kulalamikia kufingiwa kwa Twitter.

  Ujumbe wa Bw. Dorsey umewavutia Wanageria wengi wanaotumia mtandao wa VPN kufikia programu hiyo tumishi.

  Twitter inajadiliana na serikali ya baada ya kupigwa marufuku nchini humo tarehe 5 mwezi Juni.

  Marufuku hiyo ilifuatia hatua ya mtandao huo kufuta ujumbe wa Rais Mohammadu Buhari lakini ofisi yake imesema hatua hiyo haihusiani kivyovyote na suala hilo.

  Raia wa Nigeria siku ya Jumamosi waliandamana kulalamikia uongozi mbaya, ukosefu wa demokrasia na kupigwa marufuku kwa Twitter.

  Polisi walitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanji na kuwakamata baadhi yao,kulingana na vyombo vya habari nchini humo.

  Maandamano ya Jumamosi ni ya kwanza tangu maandamano ya #EndSARS ya kupinga ukatili wa polisi yaliyofanywa kwa wiki kadhaa.

  Soma zaidi:

  Serikali hufanikiwa vipi kufunga au kubana mtandao?

 3. Nigeria yataka wenye mitandao ya kijamii kupata vibali vya ndani

  Nigerian authorities suspended Twitter five days ago

  Kampuni za mitandao ya kijamii ambazo zinataka kuendesha shughuli zao nchini Nigeria sasa zitahitajika kujisajili nchini humo na kupewa leseni na tume ya utangazaji.

  Waziri wa mawasiliano,Lai Mohammed, ametoa tangazo hilo kufuatia hatua ya serikali kupiga Twitter marufuki siku tano iliyopita.

  Mtandao huo wa kijamii ulifuta ujumbe wa Rais Muhammadu Buhari kwa kukiuka sheria zake lakini ofisi ya rais imepinga madai kwamba marufuku hiyo ilikuwa hatua ya kilipiza kisasi.

  Baadhi ya vyombo vya habari vya kibinafsi nchini Nigeria vimepuuza amri ya kufunga akaunti zao za Twitter na kuamua kufikia mtandao huo kupitia mtandao wa VPN.

 4. Trump aunga mkono hatua ya Nigeria kuifungia Twitter

  Bw. Trump alifungiwa na Twitter na Facebook mwezi Januari
  Image caption: Bw. Trump alifungiwa na Twitter na Facebook mwezi Januari

  Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amepingeza hatu ya Nigeria kuipiga marufuku Twitter - na kutoa wito nchi zingine zifuate mkondo huo.

  "Pongezi kwa nchi ya Nigeria, kwa kuifungia Twitter kwasababu ya kumpiga marufuki Rais wao," alisema katika taarifa.

  Rais huyo wa zamani ametoa wito kwa nchi zingine kufuata mkondo na kuzifungia Facebook na Twitter " kwa kudhibiti uhuru wa kujieleza".

  Bw. Trump alipigwa marufuku na katika mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook mwezi Januari kwa tuhuma za kuchapisha ujumbe wa kuchochea uvamizi wa bunge la Marekani. Watu watano walifariki kutokana na kisa hicho.

  Twitter

  Katika taarifa yake siku ya Jumatatu, alijita kwanini hakuzifungia Facebook na Twitter wakati wa Urais wake.

  "Wao ni nani kuamua kizuri na kibaya ikiwa wao wenyewe ni wabaya? Nadhani ningeliwapiga marufuku nilipokuwa Rais. Lakini [Mwanzilishi wa Facebook Mark] Zuckerberg aliendelea kunipigia simu na kuja Ikulu ya White House kwa chakula cha jioni akiniambia jinsi nilivyokua mzuri," alisema.

  Wiki iliyopita Nigeria ilifunga akaunti za Twitter nchini humo kwa madai kwamba "shughuli za mtandao huo zinahujumu uwepo wa Nigeria kama taifa lililoundwa shirikisho".

  Hatua hiyo ilichukuliwa siku kadhaa baada ya ujumbe wa Rais Muhammadu Buhari kuondolewa kwa kukiuka kanuni za mtandao wa huo wa kijamii.

  Ilizua ghadhabu miongoni mwa Wanaigeria na mataifa ya magharibi ambayo yalisema hatua hiyo inaminya uhuru wa kidemokrasi.

  Pande zote mbili zimesema zinajadiliana kuhusu namna ya kusuluhishi

  Soma zaidi:

 5. Nigeria 'yajadiliana na Twitter' baada ya marufuku

  Twitter

  Nigeria imesema inajadiliana na Twitter,baada ya kuufungia mtandao huo wa kijamii wikendi iliyopita.

  Baada ya kukutana na wanadiplomasia, Waziri wa Mambo ya nje wa wa Nigeria Geoffrey Onyeama amesema serikali inafuatilia jinsi mazungumzo yanavyoendelea kabla ya kufanya maamuzi yoyote ya ziada.

  Katika hatua ya hivi punde dhidi ya Twitter, mamalaka imeagiza vyombo vyote vya habari kujiondoa katika mtandao huo.

  Wanadiplomasia wa Magahribi wamekosoa marufuku hiyo wakisema uhuru wa kijieleza ni sehemu muhimu ya democrasia.

  Serikali ya Nigeria imechukua hatua ya kufungia mtandao huo baada ya Twitter kuondoa ujumbe wa Rais Muhammadu Buhari wa kutishia kundi linalotaka kujitenga.

  BBC ilizungumza na Gbenga Sesan wa Mpango wa Paradigm, ambao unatoa fursa za kidijitali kwa vijana kote Afrika, ambaye anasema marufuku ya serikali imefeli.

  Maelezi zaidi:

 6. Video content

  Video caption: Lil Wayne akerwa na Ukosefu wa Mwaliko kwa Grammys za 2021: 'Je! Sistahili?'

  Baada ya kujua kwamba hajateuliwa Tuzo za mwaka huu za Grammys mwanamziki Lil Wayne ameelezea kusikitishwa kwake kwenye mtandao wa Twitter.