Njaa

 1. Ethiopia yakanusha Jimbo la Tigray kukumbwa na baa la njaa

  Tigray

  Serikali ya Ethiopia imekanusha taarifa kuwa jimbo la Tigray nchini humo limekumbwa na baa la njaa.

  Kauli hiyo imekuja muda mfupi baada ya Umoja wa Mataifa kutoa ripoti ya utafiti wake ikionya kwamba watu 350,000 katika jimbo hilo wanakabiliwa na hali mbaya ya njaa. Ripoti hiyo imeyataja pia maeneo jirani ya Amhara na Afar.

  Jimbo hilo limekuwa kwenye mapigano kwa zaidi ya miezi saba sasa, na kusababisha maelfu ya watu kuuawa na maelfu wengine kuyakimbia makazi yao.

  Serikali ya Ethiopia inasema ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa kuhusu uwepo wa baa la njaa kwenye eneo la Kaskazini mwa Tigray si za kweli.

  Msemaji wa masuala ya kigeni amesema serikali imekuwa ikipeleka vyakula katika maeneo hayo kwa ajili ya wenye uhitaji, na kuwapatia mbegu wakulima na pembejeo zingine kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa kilimo unaotarajiwa kuanza wiki chache zijazo.

  Umoja wa Mataifa na Jumuia ya Ulaya, mara kadhaa zimeonya na kuzitaka pande zinazozozana kusitisha mapigano ili kuruhusu misaada ya kibinadamu wakifkia mamilioni ya watu wenye uhitaji na kuepusha baa la njaa.

  Mgogoro wa Tigray-Ethiopia: Baa la njaa lililosababishwa na binadamu

 2. UN yaonya kutokea kwa baa la njaa katika jimbo la Tigray

  Mzozo wa Tigray umezidisha mzozo wa kibinadamu katika eneo hilo
  Image caption: Mzozo wa Tigray umezidisha mzozo wa kibinadamu katika eneo hilo

  Maeneo kadhaa katika jimbo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia yanakabiliwa na "tisho la baa la njaa", Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa General Antonio Gutterres amesema.

  Ameonya, hali inaendelea kuwa "mbaya zaidi", endapo ufadhili hautaongezwa na njia za kufikia walioathiriwa haitaimarishwa.

  ''Hatua tunazochukua sasa zinaweza kuwaokoa watuwengi walio katika hatari ya kuangamia kutokana na ukosefu wa chakula, alisema.

  Wakazi wa magharibi mwa Tigray wameiambia BBC kwamba hawana chakula na kwamba wanakabiliwa na baa la njaa. Watu wa wilaya ya Qafta Humera waliofikiwa kwa nji aya simu wamesema majambazi wamevamia mashamba yao na kuchukua mifugo wao.

  Mark Lowcock, mkuu wake wa kibinadamu, ameiambia BBC kwamba mamia ya watu tayari wanakabiliwa na njaa katika eneo la Tigray kufuatia miezi kadhaa ya mapigano.

  Mamlaka nchini Ethiopia inasisitiza kwamba hali ya utulivu umerejeshawa katika eneo hilo na njia za kuwafikia wakaazi kufunguliwa.

  Lakini UN inasema maelfu ya watu sasa wanaelekea kukabiliwa na baa la njaa kama lile lililoshuhudiwa mwaka 1984.

  Mzozo ulizuka Tigray mwezi Novemba baada ya serikali ya Ethiopia kuanzisha oparesheni ya kijeshi ya kuondoa mamlakani chama tawala cha zamani TPLF, baada ya wapiganaji wake kuteka kambi za jeshi la muungano.

  Soma zaidi:

 3. Watoto 70,000 wanakabiliwa na njaa Afrika

  Ukosefu wa chakula

  Shirika la kimataifa linalohusika na watoto la Save the Children, linaonya kwamba watoto 70,000 katika eneo la Jangwa la Sahara wanakabiliwa na tisho la kufariki kutokana na njaa kabla ya mwisho wa mwaka huu .

  Shirika hilo pia Linasema janga la Covid-19 limezifanya baadhi ya familia kushindwa kikidhi mahitaji yao ya msingi

  Kufikia sasa shirika hilo linasema idadi ya watoto wanaokabiliwa na utapia mlo imeongezeka hasa katika maeneo ya Mashariki na Kusini mwa Afrika.

  Save The Children limeongeza kuwa amri ya kutotoka nje ilizifanya familia nyingi katika bara la Afrika kupoteza njia za kujikimu.

  Kwa mujibu wa uchunguzi wake zaidi ya watoto 67,000 huenda wakapoteza maisha yao kutokana na changamoto hizo kufikia mwisho wa mwaka 2020.

  Tahadhari kama hiyo pia imetolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula duniani likiangazia jinsi viwango vya ukosefu wa chakula ulivyopanda kutokana na janga la corona.