Ivory Coast

 1. Kiongozi wa zamani wa Ivory Coast kurejea nyumbani baada ya kuachiliwa na ICC

  Laurent Gbagbo

  Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo anatarajiwa kurejea nchini humu leo kwa mara ya kwanza tangu alipokamatwa na kufikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai (ICC), mnamo Novemba 2011 kutokana na jukumu lake katika ghasia za baada ya uchaguzi ambazo zilisababisha vifo vya maelfu ya watu. Tovuti ya Koaci imeripoti.

  Ndege ya Gbagbo kutoka Brussels inatarajiwa kutua mjini Abidjan saa 1545 gmt.

  Mamlaka za Ivory Coast zimeahidi kwamba atapokelewa "kwa heshima zote kutokana na hadhi ya ofisi aliyoshikilia nchini".

  Kurejea kwa Gbagbo kunatarajiwa kupiga jeki chama chake cha Ivorian Popular Front ambacho kinakabiliwa na mgawanyiko kwa miaka kadhaa sasa.

  Waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi wameapa kufanya maandamano atakapotejea.

  Ijapokuwa Gbagbo hatimaye aliondolewa mashtaka yote katika kesi dhidi yake ya ICC tarehe 31 mwezi Machi 2021, bado anakabiliwa na mashtaka nchini Ivory Coast kwa kuhusika na wizi katika Benki Kuu ya taifa hilo la Afrika Magharibi tawi la Abidjan (BCEAO).

  Alihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kuhusika na "wizi wa BCEAO" mnamo Januari 2018.

  Rais Ouattara alimsamehe mtuhumiwa mwenzake katika kesi hiyo lakini hakuwajumuisha "watu waliofunguliwa mashtaka katika mahakama za kimataifa ".

 2. Chuo cha kupambana na ugaidi chafunguliwa Ivory Coast

  Wanajeshi

  Chuo cha kimataifa cha kupambana na ugaidi kimefunguliwa karibu na mji wa Abidjan huko Ivory Coast.

  Chuo hicho kinachofahamika kama AILCT, kilifadhiliwa na Ufaransa na Muungano wa Ulaya ,EU, na nchini zingine kinalenga kusaidia eneo hilo kukabiliana na wanamgambo wa kijihadi.

  Hafla ya ufunguzi wake iliongozwa na Waziri Mkuu wa Ivory Coast, Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo na Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa.

  Chuo hicho ambacho kimejengwa eneo lenye minazi mingi karibu kilo mita 80 kutoka mjini Abidjan, kitatumika kutoa mafunzo ya kijeshi.

  Wanajeshi

  Tayari dola milioni 27 sawa na (euro milioni 20) zimewekezwa katika mradi huo lakini fedha zaidi zinahitajika kuukamilisha ndani ya miaka miwili ijayo.

  Malengo matatu muhimu ni:

  • Kufundisha vikosi maalum vya majeshi katika mkoa huo.
  • Kuwapa mafunzo dhidi ya ugaidi maafisa, kama mahakimu, maafisa wa forodha na wahasibu.AILCT inataka kuunda mitandao ya wataalamu wanaojuana na kufanya kazi pamoja katika mipaka.
  • Kuunda kituo cha kimkakati cha kusoma.
  Tayari dola milioni 27 sawa na (euro milioni 20) zimewekezwa katika mradi huo
  Image caption: Tayari dola milioni 27 sawa na (euro milioni 20) zimewekezwa katika mradi huo

  Uzinduzi wake unakuja siku chache baada ya Ufaransa kutangaza kwamba inakamilisha Operesheni ya Barkhane katika eneo la Sahel, ambalo linakabiliwa ukame kusini mwa Jangwa la Sahara.

  Eneo hilo linajumuisha Mali, Chad, Niger, Burkina Faso na Mauritania.

 3. ICC kutoa uamuzi juu ya kuachiliwa kwa Gbagbo wa Ivory Coast

  Bw.Gbagbo

  Mahakama ya Kimataifa ya Kesi za Jinai ICC leo inatarajiwa kuamua ikiwa itadumisha hatua ya kumuondolea mashtaka Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo.

  Bw.Gbagbo na kiongzi wake wa zamani wa Charles Ble Goude walistakiwa kwa kujihusisha na ghasia baada ya uchaguzi katika nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi zaidi ya mwongo mmoja uliopita.

  Ghasia zilizuka baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 wakai tBw Gbagbo – ambaye alikuwa madarakani kwa muongo mmoja – kukubali kushindwa .

  Waliondolewa kesi ya uhalifu dhidi ya binadamu mwaka 2019.

  Upande wa mashtaka ulikata rufaa dhidiya uamuzi wa kumuondolea makossa Laurent Gbagbo, ukihojijinsi uamuzi wa kwanza ulivyofikiwa na kusisitiza kwamba maelfu ya nyaraka na mashahidi 96 waliotoa ushahidi wao wakati wa kesi, walidhibitisha kuwa kwamba uhalifu ulitekelezwa

  Gbagbo mwenye umri wa miaka 75 amekuwa akiishi mjini Brussels lakini ana matumaini ya kurudi nyumbani ikiwa rufaa ilitowasilishwa na waendesha mashtaka itakataliwa.

  Hukumu hiyo itafuatiliwa kwa karibu Ivory Coast, ambako rais huyo wa zamani anasalia kuwa na ushawishi mkuwa, katika nchi hiyo ambayo bado inajitahidi kupata utulivu wa kisiasa.

  Mwaka jana kulitokea makabiliano makali nchini humo baada ya hasimu wa kisiasa wa muda mrefu wa Bw. Gbagbo, Alassane Ouattara kutangaza kwamba ana mpango wa kugombea urais kwa muhula wa tatu .

 4. Video content

  Video caption: Koffi N'Dri Paulin abuni pikipiki yenye winchi kwa ajili ya ujenzi

  Koffi N'Dri Paulin abuni pikipiki yenye winchi kwa ajili ya ujenzi

 5. Rais Ouattara na upinzani ‘kupatana’ wakati wa vurugu za baada ya uchaguzi

  Ouattara na mpinzani wake kuirudisha amani

  Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, na mpinzani wake mkuu, Henri Konan Bédié, wamesema wameamua kupatana baada ya wiki kadhaa za vurugu baada ya uchaguzi uliokumbwa na mzozo.

  Wawili hao wamesema wataendelea kuzungumza baada ya kukutana katika mji wa kibiashara, Abidjan, siku ya Jumatano.

  Serikali imesema kuwa watu 85 wameuawa katika vurugu za baada ya uchaguzi ambao Bw.Ouattara alishinda ili kuliongoza taifa hilo kwa muhula wa tatu.

  Viongozi kadhaa wa upinzani wamekamatwa baada ya kupinga uchaguzi na kuanzisha utawala wa upinzani.

  Maneno ya kwanza ya Rais Ouattara kwa Waandishi wa habari baada ya mkutano yalikuwa “uaminifu umejengwa upya”

  Lakini hawakupeana mikono mbele ya wapiga picha.

  Chama cha Bw. Bedie, PDCI, awali kilisisitiza masharti kadhaa kabla ya mkutano –ikiwemo kuondolewa kwa vizuizi vya kiusalama kwenye makazi ya viongozi wa upinzani na kusitisha kesi dhidi yao.

  Upinzani hauyatambui matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe 31 mwezi Oktoba.

 6. Upinzani Ivory Coast wakataa mabadiliko ya tume ya uchaguzi

  Ivory Coast
  Image caption: Wafuasi wa upinzani wamekuwa wakipinga hatua ya rais ya kugombea kwa mara ya tatu

  Upinzani huko Ivory Coast umekataa mpango wa serikali wa kufanya mabadiliko katika tume ya uchaguzi kabla ya uchaguzi utakaofanyika wiki ijayo na kusisitiza kwamba utasusia uchaguzi huo.

  Rais Alassane Ouattara anatafuta kuchaguliwa katika muhula wa tatu hatua iliyozua utata.

  Kugombea kwake kumesababisha maandamano kote nchini humo.

  Umoja wa Mataifa umeonesha wasiwasi wake kuhusu ghasia zinazoendelea ambazo zimesababisha vifo vya watu karibu saba huku zaidi ya 40 wakijeruhiwa, kwa mujibu wa serikali.

  "Wagombea wa upinzani wanasisitiza kuwa wataendelea kuasi dhidi ya utekelezaji wa sheria na kusema wanataka taasisi za kimataifa kuingilia kati," Maurice Kakou Guikahue, msemaji wa upinzani, alizungumza na wanahabari Alhamisi.

  Wagombea wawili wa upinzani – aliyekuwa rais, Henri Konan Bédié, na aliyekuwa waziri mkuu, Pascal Affi N'Guessan – walitangaza kususia uchaguzi mapema mwezi huu.

 7. Macron 'kukutana na rais wa Ivory Coast ' licha ya mzozo wa uchaguzi

  Alassane Ouattara
  Image caption: Rais Alassane Ouattara ameteuliwa na chama tawala kugombea muhula wa tatu madarakani

  Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atakutana na mwenzake wa Ivory Coast Alassane Ouattara mjini Paris leo Ijumaa, kwa mujibu wa taarifa ya shirka la habari la AFP inayonukuu vyanzo vy ahabari katika ofisi ya rais wa Ufaransa.

  Uamuzi wa bwana Ouattara kugombea muhula wa tatu wa urais katik auchaguzi utakaofanyika mwezi Octoba umezua taharuki na maandamano nchini.

  Awali alikuwa amesema hatogombea, lakini akabadili msimamu huo kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Amadou Gon Coulibaly,aliyekuwa ameteuliwa na chama tawala kuwa mrithi.

  Wapinzani wake wanasema jaribio lake la kugombea muhula wa tatu linakiuka katiba.