Gereza & Jela

 1. Idadi ya vifo katika mapigano ya gereza la Ecuador yapita 100

  Gereza

  Karibu wa 116 wameaminiwa kufariki katika mapigano kati ya magenge hasimu katika gereza la Ecuador, maafisa wanasema na kuifanya kuwa ghasia mbaya zaidi ya magereza katika historia ya nchi hiyo.

  Wafungwa wasiopungua watano walikatwa vichwa katika mapigano hayo ya Jumanne katika gereza la mji wa Guayaquil, huku wengine wakiuawa kwa kupigwa.

  Kamanda wa polisi Fausto Buenaño anasema wafungwa pia walirusha gurunedi.

  Iliwachukua maafisa 400 kudhibiti ghasia katika gereza hilo ambalo linawazuilia wafungwa wanaohusishwa na magenge ya kimataifa ya ulanguzi wa dawa za kulevya.

  Vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kuwa uasi huo uliamriwa na na magenge ya Mexico ya dawa za kulevya ambayo sasa yanafanya kazi nchini Ecuador.

  Mkurugenzi wa huduma ya magereza ya Ecuador Bolivar Garzon ameambia kituo kimoja cha radio kuwa hali ni "mbaya".

  "Jana, polisi ilichukua udhibiti mwendo wa saa nane [lsaa za hukoo], lakini usiku wa jana kulikuw ana ufyatulianaji mwingiine wa risasi, vitu vingine, emilipuko na asubuhi ya leo hali imedhibitiwa, kwa sasa tunaingia kwenye vyumba vilivyokuwa na mapigano na kukusanya miili zaidi",alisema.

  Jinsi wanawake wa Mexico wanavyotumiwa kingono na wafanyabiashara ya madawa ya kulevya Mexico