Shirika la Afya Duniani (WHO)

 1. Video content

  Video caption: Rodwell Nkomazana: Kijana wa miaka 9 anayetibu uso wake baada ya kushambuliwa na fisi

  Tarehe 9 Septemba kijana Rodwell Nkomazana alishambuliwa nje ya kanisa nchini Zimbabwe.

 2. Uchafuzi wa hewa: Hali ni mbaya zaidi kuliko tulivyodhani - WHO

  Air pollution regularly exceeds recommended safe levels

  Uchafuzi wa hewa ni hatari zaidi kuliko ilivyodhaniwa hapo awali, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeonya, kwani kunapunguza kiwango salama kabisa cha vichafuzi muhimu kama dioksidi ya nitrojeni.

  Inakadiriwa watu milioni saba hufa mapema kila mwaka kutokana na magonjwa yanayohusiana na uchafuzi wa hewa, WHO inasema.

  Nchi zenye kipato cha chini na cha kati zinaumia zaidi, kwasababu ya kutegemea mafuta yanatokana na makaa ya mawe kwa ajili ya maendeleo ya uchumi.

  WHO inaweka uchafuzi wa hewa sawa na uvutaji sigara na ulaji usiofaa.

  Inasisitiza nchi zake 194 wanachama kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi na kuchukua hatua juu ya mabadiliko ya hali ya hewa, kabla ya mkutano wa COP26 mnamo Novemba.

  Miongozo hiyo mpya iliyotolewa Jumatano, nusu imependekeza kiwango cha juu cha chembe ndogo zinazoitwa PM2.5s.

  Chembe hizi hutengenezwa na mafuta yanayowaka katika uzalishaji wa umeme, moto wa nyumbani na injini za gari.

  "Karibu asilimia 80 ya vifo vinavyohusiana na PM2.5 vingeweza kuepukwa ulimwenguni ikiwa viwango vya sasa vya uchafuzi wa hewa vitapunguzwa hadi vile vilivyopendekezwa katika mwongozo uliofanyiwa maboresho",WHO ilisema.

  Vichafuzi vingine vilivyochaguliwa katika miongozo ni pamoja na ozoni, dioksidi ya nitrojeni, dioksidi ya sulfuri na monoksidi kaboni.

  Uchafuzi wa hewa unahusishwa na hali kama ugonjwa wa moyo na viharusi.

  Kwa watoto, inaweza kupunguza ukuaji wa mapafu na kusababisha ugonjwa wa pumu.

  "Kuboresha ubora wa hewa kunaweza kuongeza juhudi za kupunguza mabadiliko ya hali ya hewa, wakati kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi kwa mazingira, kutaboresha ubora wa hewa,"WHO inasema.

  Maisha katika nyuzi joto 50: Jinsi ya kupoza jiji kubwa

  Maisha katika nyuzi joto 50: Moto wenye sumu unaochochea mabadiliko ya tabia nchi

 3. Video content

  Video caption: Chanjo ya Corona: Nini kitahitajika kwa bara hili kuanza kutengeneza chanjo zake?

  Afrika bado inakabiliwa na janga la awamu ya tatu la ugonjwa wa corona , huku maradhi mengi yakiripotiwa.

 4. Digital Covid certificate

  Cheti kipya cha usafiri kimeanza kutumika ndani ya mataifa ya EU kwa wale waliochanjwa, waliopimwa na kubainishwa hawana ugonjwa wa Covid-19, au wale waliopona hivi karibuni kutokana na ugonjwa huo. Lakini je itachangia ubaguzi?

  Soma Zaidi
  next
 5. Video content

  Video caption: Matangazo ya Dira ya Dunia TV Jumatatu 21/06/2021

  Matangazo ya Dira ya Dunia TV Jumatatu 21/06/2021 na Zuhura Yunus