Raila Odinga

 1. Waziri mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga apona Virusi vya Corona

  Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga, amepona virusi vya Corona baada ya kupimwa Jumatano na kupatikana hana ugonjwa huo.

  Chama cha ODM anachokiongiza kimeatangaza kupitia Twitter kwamba Raila hayupo hatarini tena na ataanza kuangazia masuala yanayofaa kushughulikiwa.

  View more on twitter

  Odinga alipatikana na virusi vya Corona Machi tarehe 11 mwaka huu baada ya kulalamika kuwa na uchovu alipomaliza msururu wa kampeni za mwafaka wa maridhiano (BBI) katika eneo la Pwani.

  Raila alikutana na maafisa wa chama hicho Jumatano kujadili matukio ya hivi karibuni nchini ikiwa ni pamoja na utoaji wa chanjo nchini humo na hali ya uchumi wa Kenya.

  Alithibitisha kujitolea kwa ODM kufanikisha mwafaka wa BBI uliotiwa saini kati yake na Rais Uhuru Kenyatta na vile vile Muswada wa Marekebisho ya Katiba, 2020 uliotokana na BBI.

 2. Raila Odinga amuomboleza rafiki yake rais Magufuli

  Raila Odinga

  Aliyekuwa waziri mkuu nchini Kenya na kiongozi wa upinzani Raila Odinga ametuma risala za rambirambi kwa familia ya rais John Pombe Magufuli na raia wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

  Katika taarifa kwa vyombo vya habari Raila amemtaja marehemu kama kiongozi aliyejaribu kuimarisha hali ya raia wa Tanzania.

  Amesema kwamba rais Magufuli amekuwa rafiki yake wa muda mrefu na kwamba amekuwa kando yake wakati mgumu alipomuhitaji.

  Amesema kwamba tangazo la kifo chake amelipokea na huzumi kubwa akiongezea kwamba anasimama na familia ya marehemu wakati huu wa maombolezo.

  Kiongozi huyo amesema kwamba kwa miaka kadhaa iliopita ameshirikiana na rais Magufuli haswa katika kuiunganisha Afrika mashariki kupitia miundo msingi.

  Amewataka Watanzania wote kusalia watulivu na kufuata utamaduni uliowachwa na rais wa kwanza wa taifa hilo Julius Nyerere na wa viongozi waliofuata katika kukabidhiana mamlaka kulingana na katiba ya taifa hilo

 3. Uhuru Kenyatta akiri kufujwa kwa shilingi bilioni 2 kila siku, Kenya

  Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

  Rais Uhuru Kenyatta Jumatatu ametetea matumizi ya serikali yake kuhusiana na mpango wa mchakato wa kuleta maridhiano ya kitaifa (BBI), huku akisema kuwa shilingi bilioni 2 zinafujwa na maafisa wa umma kila siku.

  Bwana Uhuru Kenyatta amesema hayo wakati alipokuwa anahojiwa na idhaa moja nchini Kenya inayopeperusha matangazo kwa kutumia lugha ya Kikuyu ambayo ni lugha asili ya rais Uhuru Kenyatta.

  “Kwani ni mara ya kwanza Wakenya watakuwa wanashiriki kura?,” Rais aliuliza, huku akisema kuwa faida itakayotokana na mchakato wa BBI ambao unalenga kupanua nafasi za utawala kushirikisha makabila yote ya Kenya, imepita matumizi ya fedha kwa shughuli hio.

  Aidha rais alinukuliwa akisema

  “Mabilioni wanayoiba ambayo sitayataja ni zaidi kuliko makadirio ya BBI”

  Bila kutaja miradi ambayo fedha zimeibiwa, Uhuru Kenyatta aliongeza,

  “Kiasi wanachoiba kila siku ni zaidi ya bilioni 2.’’

  Rais Uhuru Kenyatta na mpinzake wa kisiasa, Raila Oding

  Kura ya maoni inayolenga kupitisha mpango wa BBI inatarajiwa kufanywa mnamo mwezi Juni mwaka huu.

  Mpango huu wa mchakato wa kuleta maridhiano ya kitaifa (BBI) ulianzishwa na Rais Uhuru Kenyatta na aliyekuwa Waziri Mkuu nchini kenya Raila Odinga ambao umekisiwa kutumia zaidi ya shilingi bilioni 12.

  Tangu kuanzishwa kwa mchakato wa BBI nchini Kenya, mijadala imejikita kuhusiana na fedha zitakazo tumika kufadhili mradi huo, na pia ikiwa ni wakati sahihi kufanyika – hivyo basi nchini Kenya kumekuwa na mgawanyiko wa wale wanaounga mkono BBI na wale wanaopinga.

  Juhudi za Rais Uhuru Kenyatta kuhudhuria na kushiriki kipindi katika idhaa inayotumia lugha asili ya Kikuyu imetajwa na wadadisi wa kisiasa kama njia ya kuwarai watu kutoka jamii yake kuunga mkono mchakato huu wa BBI.

  Pia unaweza kusoma:

  Je, maridhiano ya BBI yamegeuka kuwa mpasuko wa kisiasa Kenya?

  Siasa za Kenya: Fukuto ndani ya chama cha Jubilee, nani anayelengwa?

  Je ripoti ya BBI itasaidia kutatua matatizo ya Wakenya?

 4. wafuasi wa upinzani walikabiliana na maafisa wa polisi Jijini nairobi

  Mkurugenzi wa uchunguzi wa mashtaka ya jinai nchini Kenya George Kinoti amefafanua kwana ofisi yake haina mpango wa kufufua upya kesi zilizopita za ghasia za baada ya uchaguzi wa maka 2007 kama inavyodaiwa na baadhi ya viongozo nchini humo.

  Soma Zaidi
  next
 5. Hezron Mogambi

  Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Nairobi

  William Ruto

  Naibu Rais wa Kenya, William Ruto na nia yake ya kuwania Urais mwaka wa 2022 imepandisha joto la kisiasa nchini Kenya mapema zaidi ya mwaka mmoja na nunsu kabla wakati wenyewe na kuzua maswali mengi.

  Soma Zaidi
  next
 6. Video content

  Video caption: Je ripoti ya BBI ndio suluhisho la amani na umoja wa kudumu Kenya

  Ripoti hiyo iwapo itapitishwa italeta mabadiliko makubwa katika mfumo wa uongozi wa kitaifa

 7. Hezron Mogambi

  Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Nairobi

  Raila Odinga

  Matamshi ya hivi karibuni ya Naibu mwenyekiti wa chama cha Jubilee na ambaye pia ni mwandani wa Rais Kenyatta na Katibu Mkuu wa chama kikuu cha wafanyikazi nchini Kenya(COTU) Francis Atwoli yanaonekana kuchochea fikra hizi ingawa kinara wa chama cha ODM mwenyewe hajalivalia njuga suala hili.

  Soma Zaidi
  next