Instagram

 1. Instagram wakabiliana na watu wazima wanaowasiliana na vijana

  Instagram

  Mtandao wa kijamii wa Instagram unaongeza hatua za kiusalama kulinda vijana dhidi ya ujumbe usiohitajika kutoka kwa watu wakubwa ambao wanawasiliana nao.

  Watuamiaji wa kitambo wataweza kuwasiliana na vijana ambao wanawafuata pekee kwa njia ya kibinafsi.

  Na ujumbe wote utakuwa na ilani inayokumbusha vijana kuwa wanahitajika kuripoti ikiwa kuna lolote linalowafanya wahisi hawako sawa.

  Hatua hizo zitafanikiwa ikiwa watumiaji wa akaunti wameweka umri wao sahihi, jambo ambalo vijana wakati mwingine huwa wanadanganya ili kukwepa masharti ya kile wanachoweza kuona.

  Vilevile, wanaowanyatia wanaweza kujifanya kuwa ni vijana wadogo kumbe ni uwongo.

  Mtandao wa Instagram umesema unaunda "programu yenye akili isiyo ya asili, na teknolojia ya kujifunza ya mashine" kusaidia kukabiliana na tatizo la kudanganya umri wa mtu hasa katika visa ambapo wenye akaunti sio waaminifu.

  Akaunti Binafsi

  Umri wa chini zaidi kwa anayeruhusiwa kuwa na akaunti kwenye mtandao huo ni miaka 13.

  Pia mtandao huo umesema kuwa sasa unatoa ofa kwa watumiaji vijana chaguo la kufanya akaunti yake ya kibinafsi wakati wanafungua akaunti.

 2. Video content

  Video caption: Madonna aweka video ya kutatanisha kuhusu tiba ya Covid 19 kwenye mtandao wa Instagram.

  Video ya mwanamziki Madonna kwenye mtandao wa Instagram kuhusu 'tiba' ya Corona imewekwa ujumbe wa 'False Information'.

 3. Video content

  Video caption: Wazee wapata umaarufu kwenye mtandao wa Instagram

  Kwa miaka 70 bi Hsu Hsiu-e na mume wake Chang Wan-ji,wamekuwa wakioshea watu nguo mjini Taichung, katikati mwa Taiwan.

 4. Video content

  Video caption: The Rock ndiye 'mtu tajiri zaidi' kwenye mtandao wa Instagram.

  Muigizaji maarufu Dwayne "The Rock" Johnson amekuwa nyota ambaye anaweza kulipisha malipo ya bei ya juu Zaidi kwa matangazo ya biashara kwenye ukurasa wa Instagram.

 5. Video content

  Video caption: Matamshi ya Muigizaji Vanessa Hudgens kuhusu Corona yakera wengi

  Muigizaji Vanessa Hudgens ameomba msamaha baada ya kusema kuwa kila mtu atakufa hata kukiwa hakuna virusi vya Corona.

 6. Video content

  Video caption: Bendi ya muziki ya Sautisol yatamba kimataifa

  Kundi la Sauti sol kutoka Kenya wametangaza kupitia mtandao wa Instagram kuwa wamesaini mkataba na kampuni yakurekodi ya Universal

 7. Video content

  Video caption: Madonna avunja tamasha ya Lisbon

  Habari mbaya kwa mashabiki wa mwanamziki Madonna baada ya nyota huyo kupiga marufuku tamasha iliyokuwa ifanyike huko Lisbon, dakika 45 tu kabla ya tamasha hiyo.