Idadi ya watu waliofariki kote duniani kwa ajili ya janga la corona ni kubwa sana: zaidi ya watu milioni mbili unusu wamepoteza maisha, mamilioni ya wengine kuwachwa bila kazi, na mamilioni ya dola za utajiri zimeharibiwa.
Soma ZaidiUrusi
Yusuf Jumah
BBC Swahili
China na Urusi kujenga kituo cha anga za mbali mwezini
Copyright: EPAShirika la anga za mbali la Urusi Roscosmos limesema kuwa limesaini makubaliano na kituo cha taifa la China cha utawala wa anga za mbali ili kutengeneza vifaa vitakavyosaidia kufanya utafiti wa sakafu ya mwezi, kwenye uzio (orbit) au eneo lote la mwezi.
Mzozo wa Tigray: Baraza la Usalama la UN lashindwa kukubaliana
Copyright: Getty ImagesImage caption: Mamia ya watu waliuawa mzozo ulipozuka mwezi Novemba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kufikia tamko la pamoja kuhusu mzozo wa Tigray kaskazini mwa Ethiopia, baada ya Urusi, China na India kuchukualia mgogoro huo kuwa suala la ndani.
Wanadiplomasia walionukuliwa na shirika la habari la AFP wamesema nchi tatu za Afrika katika baraza hilo- Kenya, Niger na Tunisia - zimeunga mkono rasimu ya taarifa iliyoandikwa.
Kamishena wa kutetea haki katika Umoja wa Mataifa katika awali alisema kulikuwa na ripoti za kusikitisha zinazoashitia huenda uhalifu wa kivita ulitekelezwa katika jimbo Tigray.
Michelle Bachelet aliangazia visa vya unyanyasajji wa kijinsia, mauaji ya kiholela na uharibifu mkubwa ulifanywa katika eneo hilo.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kutetea haki inataka kupewa idhini ya kuchunguza ripoti za ukatili uliotekelezwa na majeshi ya Ethiopia na Eritrea, wapiganaji wa Tigray People’s Liberation Front na vikosi vya jimbo la Amhara.
Maelezo zaidi: