Liberia

 1. Kamanda wa zamani wa waasi Liberia ahukumiwa kifungo cha miaka 20

  WAASI

  Mahakama nchini Uswisi imemhukumu kamanda wa zamani wa waasi wa Liberia kifungo cha miaka ishirini jela mashitaka kadhaa ya uhalifu wa kivita ikiwemo ubakaji na mauaji aliyohusika katika miaka ya tisini.

  Majaji walidumisha mashitaka ishirini na moja kati ya ishirini na tano dhidi ya Alieu Kosiah ambaye ana kibali cha kuishi Uswisi.

  Ni Mliberia wa kwanza kushitakiwa na kuhukumiwa kwa uhalifu luliofanyika wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza Liberia mwaka 1989 na kumalizika mwaka 2006.

  Takriban watu laki mbili na elfu hamsini waliuawa katika vita hivyo ambavyo watoto walilazimishwa na waasi na majeshi kuwa wapiganaji.

 2. Weah ampongeza mwanawe kwa kushinda taji la Ligi Kuu ya Ufaransa

  President George Weah (L) has continued to play football since being elected president in 2017

  Rais wa Liberia mwanasoka wa zamani wa kimataifa George Weah amempongeza mtoto wake wa kiume, Timothy Weah, baada ya klabu yake ya Lille kushinda taji la Ligi Kuu ya Ufaransa.

  "Mimi mwenyewe kama mshindi wa taji la Ligue 1, nafahamu fika kwamba unahitaji kujitolea na kufanya kazi kwa bidii kila wiki ili kupata ushindi ,” Rais Wear alisema katika ujumbe uliowekwa katika tovuti yake rasmi ya urais.

  “Licha ya kuumia mara kadhaa na kucheza mechi 28 , hiki ni kitu ambacho kimekuwa ndoto ya Tim.

  “Tunashukuru kwamba akiwa mshambulizi wa kikosi chake , alichangia kwa kiwango kikubwa ufanisi wa Lille kuwa mabigwa kwa mara nyingine,” Bw. Weah aliongeza.

  Rais Weah alichezea klabu kadhaa za Ulaya, Ikiwemo Paris Sainte Germaine, Monaco, AC Milan, Chelsea na Manchester City kabla ya kustaa mwaka 2004 kwuenda kujitosa katika siasa za kitaifa.

  Mwaka 1995 alitunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Fifa na hatimaye kuchaguliwa kuwa rais wa nchi yake mwaka 2017.

  Pia unaweza kusoma:

 3. Police had locked the hut but items used in rituals can be seen through a crack in the door

  Visa kama hivyo vimetokea katika nchi za DRC, Liberia na hata Sudan Kusini . Hata hivyo kunavyo visa vya kuogofya ambavyo watu walipatikana na hatia ya kula nyama ya binadamu nchini Afrika kusini ,na kuzua hofu nchini humo miaka minne iliyopita .

  Soma Zaidi
  next
 4. WAASI

  Ni mauaji ambayo yaliushangaza ulimwengu tarehe 9 septemba mwaka wa 1990. Hakuna aliyewahi kufikiria kwamba rais wa nchi angeweza kukamatwa na waasi ,wampige risasi ,wamnyanyase kwa saa kadhaa ,wamkate masikio na kisha wamuue katika hali ya kutatanisha .

  Soma Zaidi
  next
 5. MNYIKA

  Tume ya uchaguzi nchini Tanzania imelaani taarifa zilizotolewa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na Katibu mkuu wa chama cha upinzani nchini humo Chadema, Bw John Mnyika kuhusu mchakato wa zabuni ya uchapishaji wa makaratasi ya kupigia kura pamoja na jina la mzabuni.

  Soma Zaidi
  next
 6. " Habari mbaya ni kwamba kila mmoja anaweza kuwa muathiriwa," amesema Bobi Wine katika wimbo wake kuhusu corona

  Tangu mlipuko wa coronavirus ulipoanza juhudi mbali mbali za kuzuwia kusambaa kwa virusi hivyo zimekua zikifanyika, lakini baadhi ya wanasiasa hawa wamejitosa kutumia usanii kuwaelemisha raia juu ya kuepuka virusi.

  Soma Zaidi
  next