Uholanzi

 1. Video content

  Video caption: Virusi vya corona: Wanandoa wa Uholanzi waliotoroka karantini wakamtwa

  Wenzi hao walifanikiwa kupanda ndege kuelekea Uhispania lakini walikamatwa kabla tu ya kupaa.

 2. Tazama daraja la watembea kwa miguu lililo refu zaidi duniani

  Video content

  Video caption: Ilichukua miaka miwili kujenga daraja hili kwa gharama ya dola milioni 2.8
 3. Simba ahasiwa baada ya kuzalisha watoto wengi

  Simba

  Simba mmoja katika hifadhi ya wanyama nchini Uholanzi amehasiwa baada ya kuzaa watoto watano mwaka jana.

  Simba huyo mwenye umri wa miaka 11, anayeitwa Thor, aliwapachika mimba simba wawili. Wa kwanza alizaa mapacha, wakati wa pili alikuwa na watoto watatu.

  "Kwa nini tunafanya hivyo? Kwa sababu yeye ni ‘mzaaji’ aliyethibitishwa," daktari mkuu wa Zoo ya Royal Burgers huko Arnhem alisema.

  Hazina ya utunzi wa wanyama wa pori duniani imesema idadi ya samba walio porini imepungua kwa asilimia 20-30 katika miaka 20 iliyopita Lakini daktari wa wanyama Henk Luten, ambaye alifanya upasuaji huo Alhamisi, alisema hifadhi hiyo ya wanyama sasa ilikuwa na DNA ya kutosha kutoka kwa Thor.

  "Tuna watoto wengi wake na hatutaki kuzidisha DNA yake," aliliambia shirika la habari la Reuters.

  Ingawa sio jambo ambalo halijawahi kusikika , kufanyia simba vasektomi ni jambo nadra sana kutokea "Ni mara ya kwanza katika miaka 35 kuwa daktari wa mifugo hapa kumfanyia simba operesheni hii'' Bw Luten alisema.

  Aliamua kutumia vasektomi badala ya kuhasiwa kwa simba huyo kwa sababu utaratibu wa mwisho ungemfanya apoteze kidevu chake.

  Ukosefu wake wa testosterone baada ya kuhasiwa pia ungemfanya Thor apoteze nafasi yake katika uongozi wa kundi la kijamii na Simba katika Hifadhi hiyo Simba wametajwa kama waliopo hatarini ya kuangamizwa na WWF, ambayo inamaanisha wanakabiliwa na hatari kubwa ya kutoweka porini.