Lishe & Chakula

 1. Watu 35 wafariki baada ya kula 'mimea ya porini' Msumbiji

  Ramani

  Watu 25 wa familia moja ni miongoni mwa watu 35 waliofariki kaskazini mwa Msumbiji baada ya kuripotiwa kula mimea na matunda ya mwituni, mamlaka zinasema.

  Maafisa wanasema hivi karibuni kumeripotiwa visa vya watu katika eneo hilo kula matunda ya mwituni, mizizi na hata nyasi.

  Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na televisheni ya kitaifa , TVM, wakazi wamekua wakisaga nyasi kupika xima – uji wa kienyweji wa Msumbiji, ambao hutengenezwa kutokana na unga wa mahindi.

  Uhaba wa chakula katika mkoa wa Nampula umechangiwa na ukosefu wa mvua.

 2. Burundi yapiga marufuku uagizaji wa mahindi kwa miezi sita

  Mahindi

  Wizara ya biashara ya Burundi imepiga marufuku uagizaji mahindi kutoka nje kwa miezi sita kuanzia tarehe 8 Machi.

  Katika taarifa wizara hiyo imesema mahindi yaliyoingizwa nchini humo hivi karibuni ''hayakua mazuri'' na huenda yakadhuru afya ya watu.

  Haikubainisha mahindi hayo yaliagizwa kutoka nchi gani.

  ''Wakati nafaka hii na unga inakataliwa na nchi jirani… tunahitaji kuhakikisha hayaingizwi nchini'', alisema Jeremie Banigwaninzigo, katibu wa kudumu wa wizara ya biashara na utalii wa Burundi.

  Mahindi

  Hatua hii inakuja baada ya Kenya kupiga marufuku ununuzi wa mahindi kutoka Uganda na Tanzania kutokana na hofu ya usalama ya nafaka hiyo.

  Uagizaji mwingi wa mahindi wa Burundi unatoka Uganda na Zambia - lakini haijulikani ni kwa kiwango gani nchi hiyo inategemea uagizaji ili kukidhi mahitaji yake.

  Soma zaidi:

 3. Video content

  Video caption: Umuhimu wa kula mboga kwa afya yako

  Ni mwanzo mpya mwaka huu ambao watu wengi wanautaja kama mwezi wa Veganuary ambapo watu wanajaribu kula vyakula vya mboga kwa mwezi huu wote.

 4. Video content

  Video caption: Utafiti wabaini kuwa utapiamlo na Uzito kupita kiasi unaathiri nchi za kipato cha chini

  Utafiti uliochapishwa katika jarida la matibabu la Lancet unaonya nchi zenye kipato cha chini zinakabiliwa na ukosefu wa lishe bora na shida ya uzito kupita kiasi.